Safiri salama, safiri kwa usalama kati ya Arusha Dar via Korogwe

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Nipongeze idara ya hali ya hewa kwa kazi kubwa wanayoifanya,

Kwa hali ya hewa ilivyo kwa hapa Korogwe na kulingana na uzoefu wa hivi karibuni juu ya athari za mvua zinazoendelea kunyesha, ni vema wasafiri wanaotumia barabara kuu ya Arusha Dar kupitia Korogwe wakachukua tahadhari kutokana na mvua ya leo.

Hali ikiendelea hivi huenda maji kutoka maeneo ya milima yakafurika kwenye mito nia kusababisha barabara kutopitika.

Ni vema mkapata ushauri juu ya usalama wenu, familia zenu na mali zenu juu ya hali ya usalama kupitia kwa mamlaka zinazohusika hasa kwa hapa Korogwe maana ndipo kumekuwa na shida kwa hapa karibuni.

Kwa uzalendo na nidhamu tunaweza kuuliza hali ya usalama kwa kikosi cha zimamoto 0688918877/0718528958 au mwakilishi wa jeshi la polisi 0652449324.

Lakini pia ni muhimu kufuatilia mitandao mbalimbali kwa ajili ya taarifa sahihi.
 
Hivi hakuna namna ya kujenga miundombinu ya kupitisha maji hapo koogwe/aka. korogwe ya kuweza kuhimili maji kutoka kule milimani, lushoto
 
Hivi hakuna namna ya kujenga miundombinu ya kupitisha maji hapo koogwe/aka. korogwe ya kuweza kuhimili maji kutoka kule milimani, lushoto

Kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa maeneo haya kutokea nadhani mamlaka husika zitachukua hatua kwa ajili ya kuepuka maafa baadae
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom