Safiri Na Celtel

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
211
kuna wakati unaweza kwenda katika mghahawa fulani kwa ajili ya kujipatia chakula dulani au huduma fulani nzuri nzuri , mhudumu anakuja kukuhudumia pale unafurahia huduma ile pengine unaamua kumuachia salio la hela zako kidogo kama ahsante < siku ingine utakuja na rafiki yako mwingine pale kwa kuwa huduma ni nzuri >

pia kuna wakati unapotaka huduma za mawasiliano unapata kwa ufasaha na kwa urahisi zaidi , ungekuwa unajuana na yule jamaa wa customer care ungeweza kumpa salio kidogo la simu yako ama kumpa ka zawadi kama ingekuwa inawezekana >

kwa kuwa wato huduma za mawasiliano wanafanya kazi kwa timu sina budi kuwapongeza wote kabisa kwa kusimama kidete kuhakikisha wateja wao karibu nusu ya afrika nzima wanapata huduma za uhakika za mawasiliano >

mwaka jana mfano nilianzisha mailing list moja ina watu wengi zaidi ya alfu kumi hii ni karibu wilaya nzima wengi wao wako nje ya nchi watu hawa wanahitaji kuhabarishwa kujua habari zinazoendelea nchini mwao kila baada ya masaa kadhaa >

nilifanya kazi hii kuwapa watu habari za uhakika na kwa haraka zaidi lakini nilitakiwa kwenda kijijini moshi kusalimia ndugu jamaa na marafiki , sehemu yenyewe kulikuwa hakuna huduma ya uhakika ya mawasiliano >

mfano mimi nikitaka kujua hali ya hewa kule mazingira na mambo mengine huwa natumia google earth kwenda mpaka kijijini kupata hizo habari lakini siku hiyo nilitakiwa kwenda kule >

niende kijijini watu katika mailing list yangu wasijue kama nimesafiri walitakiwa wapate habari zile zile nilizokuwa nawapa wakati nikiwa mjini na kwa wati ule ule .

nikamua kwenda celtel nikaonana na rafiki yangu mmoja anaitwa david niliongea nae kuhusu huduma zao pale akanishauri kifaa cha kununua lakini sikumwambia kama nitasafiri nacho mimi nilimwamini kwa kuwa celtel nao wamemwamini ndio maana yuko pale >

nilinunua hii modem nikaunganisha na laptop yangu na baada ya siku mbili nilisafiri kuelekea kijijini kwa kweli wakati niko njiani niliweza kupata habari kupitia simu ya mkono na kusoma zingine kupitia laptop iliyokuwa imeunganishwa na mtandao wa celtel >

nilifika mpaka kijini kule niliishi kwa wiki 1 hivi nilikuwa nakaa ndani kwa sababu kuna milima milima sikuwa napenda kutoka nje nikawa nakaa pale nawapa watu yanayojiri kijijini kwangu na pande zingine za tanzania >

hapo hapo niliweza kupiga na kupokea simu kupitia hii namba yangu ya celtel kwa uhakika na bila wasi wasi wowote ule na hakuna mtu aliyehisi kama nimesafiri au nimeenda kokote kule kwa sababu habari zilikuwa ni zile zile .

kwa upande mmoja napenda kuwashuhuru celtel kwa kutuweka karibu zaidi na jamaa zetu wengine popote tunapokuwa katika tanzania na afrika mashariki kwa ujumla kwa huduma zao sasa tunaweza kuhama na office zetu kama walivyosema kama promosheni yao moja ya mwaka jana >

najua watu wengi wanaogopa kujiunga na celtel kwa sababu ya gharama hiyo ndio sababu yao kuu < lakini kumbuka katika celtel kuna huduma ambazo zinaweza kuendana na gharama zako wewe nenda uulize .

mfano kuna bonga longa pamoja na sasa hivi kuna ndoto 2 ambayo unaweza kushinda ndoto yako na kupata gari mpya kifahari

nani kama celtel ? fikiria upya halafu fanya uamuzi wa busara

kuna wale wazee hawawezi kutuma sms kupitia tovuti ya celtel unaweza kuandika sms zako na ukazituma kwenda kwa watu wako unaowapenda unaweza hata kuhifadhi hizo namba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom