Safi sana wabunge wa UKAWA

Kama ni hivyo kwanini wasirudi majimboni basi wakawaambie wananchi sababu ya kutokaa bungeni?

Sasa kule kwenye mabaa wanamuwakilisha nani
Sasa watawaambiaje na Polisi juzi tu wameagiza maji mengine ya kuwasha?
 
Kama ni hivyo kwanini wasirudi majimboni basi wakawaambie wananchi sababu ya kutokaa bungeni?

Sasa kule kwenye mabaa wanamuwakilisha nani
Wanawaambiaje wananchi wakat mikutano ya kisiasa imezuiliwa, usiwe unakula viporo mkuu, viporo vinapunguza uwezo wa kufikiri.
 
Wabunge wa upinzani almaarufu UKAWA waendelea kususia vikao vya bunge wakiongozwa na kiongozi wao Mh. Mbowe.

Inasikitisha sana kwa wapiga kura wetu wito wangu wakae meza moja ya mazungumzo kumaliza mgogoro huu.

Wanaopaswa kusikitikiwa ni wapiga kura Wa Lusinde, goodluck na the likes.
 
Mungu halindi wanafiki. Anaendelea kupigwa bao kwani sasa sheria mbalimbali zinafanyiwa marekebisho bila ya uwepo wao
halafu hizo hizo sheria zitakuja kukukandamiza wewe, kwani hakuna mbunge wa CCM aliye kwa ajili ya maslahi ya wananchi na Taifa zaidi ya maslahi yao na CCM. Kwa hiyo ni vema ukawaza zaidi ya mara mbili kuliko kuwaza hapo ulipo nyuma ya key board.
 
Nimejitengea muda,najitahidi nione mwanzo wa kikao cha bunge,lengo ni kuwaona UKAWA wanavyotoka. NS amekuwa pekee anaongoza vikao, hivi hana hata udhuru wowote kama binadamu awapishe wenyeviti?
 
MAMBO HAYA TUSIYACHEKELEE TUJIFIKIRIE KABLA YA KUTAMKA naona tumeanza kujisahau wengine watasifu wengine wanakejeli TUELEWE HII NI NCHI YA KIDEMOKRASIA
 
Leo hii tena wametoka mara tu baada ya dua ya kuliombea Bunge kukamilika.Haina haja ya kuongozwa na mtu msie na imani nae.Walizani posho ndio zingewarudisha Bungeni.

Mbunge mzalendo hawezi kuweka mbele posho kuliko maslahi ya anaowawakilisha.

Wabunge wa UKAWA hawawezi kuishi kwa posho bali kwa kila neno la kizalendo la kuwaunga mkono.

UKAWA mnavaa viatu vya mzee Mandela ambae alivumilia mengi ila mpaka leo hii dunia nzima inamuheshimu.

Pambanane mkitambua the end justifies the means.
HAWANA IMPACT! Wananchi hawaguswi UKAWA wamepoteza mvuto...... SAFI SANA TULIA! ALUTA CONTINUA!
 
Hakika Dr. Slaa alikuwa ni mwanaume katika kutafuta na kutetea haki za wanyonge. Zitto pia huwa harudi nyuma katika kutetea maamuzi sahihi. Miaka ya nyuma wawakilishi wa upinzani bungeni walikuwa ni wachache lakini wenye ueledi katika kazi yao. Kinachoendelea saa hizi ni kama maigizo tu. Kwenye awamu iliyopita kuna maneno yalisikika kuwa Mama Makinda ameshindwa kulimudu bunge Kutokana na kutokujua sheria na kama ni lawama alizipokea sana na hakuna mbunge aliyetoka nje kwa wakati huo. Iweje leo kutoka nje kumekuwa kama fasheni? Je, huyu Dr. Tulia nae hazijui sheria? Vipi kuhusu wabunge wanaotoka nje nao hawazijui sheria ili wakazitafute haki zao kwenye vyombo husika? Nawasilisha.
 
Mungu halindi wanafiki. Anaendelea kupigwa bao kwani sasa sheria mbalimbali zinafanyiwa marekebisho bila ya uwepo wao
Hata wangekuwepo wangezuia nn hao akina ndiooo wasipitishe sheria hizo. Wenye akili zetu tunawaelewa. Wooote waliodai haki duniani hawakueleweka mwanzoni baadae mambo yalipokaa sawa kila MTU alipiga makofi. hata
ww usieelewa sasa. Utaelewa tuu. time will tell
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom