Safi Rubani awashusha Mawaziri kwenye Ndege

Aug 2, 2007
61
6
Ndugu wananchi, mimi nikiwa kama abiria kwenye ndege yetu ya AirTanzania, kulitokea vibwenga vya ajabu ambavyo watu wengi tulilalamika kuhusu tukio. Baada ya kujua chanzo, tulifurahi kile kilichotokea, "kushushwa abiria" kwenda sehemu ya kupumzikia. Tukio zima lilikuwa hivi: tulipopanda, abiria walishakaa muda, unaenda, tukaanza kulalamika. Nini kinaendelea hapa? Rubani alikuwa amechemsha kutotuambia mapema. Ghafla wafanyakazi wakaanza kupishana. Nikamuuliza mmoja wao nini kinaendelea, kuna abiria harusiwi kupanda AirTanzania? Tukauliza, nani kumbe ni Bwana Nyitti, yule mfanyabiashara wa madini Arusha? Tukalamika kwanini ashushwe, jamani. Ndipo dada mmoja akatueleza yafuatayo, na hili liwe fundisho kwa wafanyabiashara: pesa hainunui utu.

Bwana Nyiti siku moja akitokea Dar kwenda Arusha alipata kuwadhalilisha wafanyakazi wa ndege, akishirikiana na polisi mkuu wa kituo, ambaye yupo uwanjani hivi sasa. Akadai ameibiwa madini, wakachukuliwa na kusachiwa mpaka nguo za ndani, wote wakiondolewa na Defender ya polisi pale uwanjani. Hakuna aliyekutwa na kitu chochote. Wakaachiwa baada ya kupigiwa simu na mkuu wa mkoa, aliyeamuru waachiwe waende hotelini. Baada ya kuulizwa kwa undani, dada mmoja mfanyakazi wa ndege alipata kupendwa na Bwana Nyiti. Akatumia njia nyingi kumpata, ikiwemo kudanganywa na wafanyakazi wa ndani, watamsaidia na hivyo kugawa fedha ovyo kila safari. Baada ya kuona hakuna mafanikio, ndipo siku ya siku wakamkuta yuko ndani ya ndege na kuamua kumaliza matatizo yake. Huu ni uonevu wa hali ya juu, kama si unyanyasaji wa kijinsia. Tunasikitika na kulaani Gazeti la Majira.
 
jamani haya magzeti inabidi wawe makini na wanachoandika maana kilichoandikwa jana hata uwezi amini
wanahabari msikubali kununulika,pesa ni makaratasi utu aununuliki wakubwa,,nyie ndie wakuelimisha jamii si kudanganya jamii
 
waliandika nini?manaake niko huku kijijini kwa sasa na siwezi kupata hilo majira
 
Toka Mkurugenzi wa Majira aukwae ubunge huko Mbeya, gazeti hilo linaboa kinoma. Limekuwa na mtizamo wa utawala kuliko hata gazeti lenyewe la serikali - Daily News.

Climax ni pale walipoweka habari ya Wanafyare kuikoromea ze Comedy front page! Habari yenyewe ilikuwa ya kufikirika na iliwekwa purposely kuziba zomea zomea ya Wanyakyusa pale Mbeya.
 
Liko kwenye gazeti Jumapili, kwamba rubani awashusha mawaziri, kwa hili tunampongeza kama ameona usalama wake ni mdogo kwanini asimshushe, safety kwanza, cha kushangaza aliyeshushwa ni Hyu Bwana Nyitti, majira acheni udaku, baada ya kuona jamaa hataki kushuka ndipo rubani akatuomba tushuke tuelekee kwenye sehemu ya kupumzikia, ndipo jamaa aliposhuka tukaambiwa wengine turudi wakiwemo hao mawaziri, waache kuandika udaku waulize kwanza.
 
Ndugu wanaforums, kutokana na tendo la kutangaziwa kushushwa na baadae kurudishwa kwa ndege, tulipofika Arusha ilibidi tujue nini kimefanya tushuke. Walishindwa kuomba polisi, ndipo tulipoambiwa kuna polisi walienda kuitwa. Walipofika ndani wakaambiwa ni Bwana Nyitti. Wote wakarudi na walipoulizwa kwa nini hamkumshusha, walijibu huyo bwana mpaka tupate ruhusa kwa top. Si rahisi kushushwa. Jamaa wakakimbilia kwa bosi wao, kumbe ndio muda tunawekwa wanajadiliana jinsi ya kumshusha. Ndipo wakaja na kuwambia marubani kuchukua toka kwa ndege ni ngumu. Sisi tutoleen nje ya ndege, tutajua cha kufanya. Nyie ma polisi, acheni kuwa miungu mtu. Wakiwa walalahoi, wenzenu mnakuwa wa kwanza kurusha makofi ili muongezewe vyeo na maboss wenu. Mnawapa shida marubani kufanya kazi za ziada wenu, wanablog.
 
Breaking news: Nimetoka kuuliza kwanini awakumtoa na police. Mwema, soma mambo ya wanao. Kumbe mabwana walienda kuombwa kumshusha. Walipofika ndani wakaonyeshwa wote wakasambaratika. Walipoulizwa vipi ati mpaka TOP mwenyewe atupe go ahead. Mwema, unayajua haya? Mbona siku nilishuka na precis kulikuwa na mlevi ndani, akaja police kumtoa kama mwizi kijana wa watu. Jamaa ana noti, wana mwogopa haya. Wandugu, mnasemaje?
 
Mzee Mavituu. Nakuheshimu sana mkuu wangu, mbona hautuelezi huyo nyitii alifanya kitu gani. umemgusia lakini hujasema kwanini wali muogopa? na je mlielezwa ni kwanini hiyo ndege ilirudishwa uwanjani.mkuu hiyo ndio bongo jambazi ana haki kuliko raia mwema. nakumbuka kulikuwa na magari yaendayo tanga yalikuwa yameandikwa yarabi salama. hivyo tuombe mungu tutafika salama huko tunapo elekea.
 
Ndugu wanaforums,,kutokana na tendo la kutangaziwa kushushwa na baadae kurudishwa kwa ndege,,tulipofika arusha ilibiidi tujue nini kimefanya tushuke,,walishindwa kuomba police,,ndipo tulipoammbiwa kuna police walienda kuitwa walipofika ndani wakaambiwa ni bwana nyitti,,wote wakarudi na walipoulizwa kwa nini hamkumshusha walijibu huyo bwana mpaka tupate ruhusa kwa top,,si rahisi kushushwa,,jama wakakimbilia kwa bosi wao kumbe ndio muda tunawekwa wanajadiliana jinsi ya kumshusha,,ndipo wakaja na kuwambia marubani kuchukua toka kwa ndege ni ngumu,,sie tutoleen nje ya ndege tutajua cha kufanya,,nyie ma police acheni kuwa miungu mtu,,wakiwa walalahoi wenzenu mnakuwa wa kwanza kurusha makofi ili muongezewe vyeo na maboss wenu,,mnawapa shida marubani kufnya azi za ziada wenu wanblog,,

Mzee wa Mvituzii
Mbona umeanzia katikati kuelezea tukio hili. Naomba uanze upya kwa kweli inaelekea nistori nzuri lakini umeanza kama vile sote tunajua ilikoanzia, yaani umeanza umeanzia karibu na mwisho.
 
Yah ni hivi bubu msema ovyo, kama uliona thread ya safi rubani niliotuma hii ndio muendelezo wake ila kwa wale waliochelewa ni hivi,

Mzee wa Mawe (Nyitt), tulipanda wote kama abiria tukielekea Kilimanjaro, tulipishana jamaa alikwaa na mawaziri (first class) nkaelekea kwetu (daraja la kawaida). Baada ya abiria wote kupanda ndege aikuonodka, mwisho rubani akasema samahani tunaomba kwa usumbufu kutokana na swala la usalama, tunaitaji kumshusha abiria mmoja kwa usalama wetu wote. Gafla wakaja police, walipoingia wakaonyeshwa huyu ndiye anaekataa kushuka, walipomwona wakageuka wote, watu wakawauliza mbona hamumshushi, ndipo bila aibu wakajibu huyo mpaka tupate ruksa kwa boss, huyo mtu mkubwa bwana. Rubani alipoenda kuambiwa hivyo akasema sasa naomba abiria wote washuke, wakipoanza kushuka jamaa alipotoka tu ndipo wengine wakaarudishwa, police wakaambiwa haya msimamisheni tushatoa ndani, maana walisema hawawezii kumtoa, ilikuwa ni kichekesho maana bado jamaa akataka kurudi, watu wote tukaanza kuogopa.
 
Tulipo toka Zanzibar kuelekea Kia, ndipo mmoja wa wafanyakazi wa ndani akanipa dondoo. Jamaa wamemkataza kupanda ATC. Hapo nyuma aliwaaibisha wafanyakazi wa ndege alipofika Kia. Akapiga simu kwa mkuu wa kituo bila kujua nini. Wafanyakazi wote walichukuliwa kwa Defender, wakaenda kupelekwa. Cha kusikitisha akiwa anasimulia, jamaa kumbe alimpenda mtoto mmoja siku nyingi. Vijana wa ndege wakawa wanakula hela yake, kila mara wanamwambia hana noma tupe njuru. Ndipo jamaa akaona demu hana mpango nae. Siku alipopanda akamwona, akakata tamaa akaanza kumwambia unajua we ni mzuri sana. Alipoona hana dira nae, mzee wa mawe ilipotua ndege, akapiga simu kwa mkuu wa polisi nimeibiwa Tanzanite. Kaka si unamjua Nyitti aongei mara mbili, Defender ikazama uwanjani, wakachukuliwa kama walivyo, wakaambiwa mizigo yenu baadae. Niliumia sana kusikia mtu wa heshima Arusha nzima tunamheshimu anafanya uhuni kama huo.
 
Jamani, lini hawa mapolisi wataacha huu uungu mtu? Nilisikitika sana. Na cha kusikitisha, yule dada mule ndani akaniambia siku wanasachiwa rubani mhusika ni yule alietuendesha. Cha kushangaza, Gazeti la Majira, likaandika mawaziri washushwa kwenye ndege si kweli. Kama walishushwa, waliifikaje uko Kilimanjaro? Muwe na mawazo ya kufikiri na kupanda ukweli pande zote. Na walivyosikitisha, wako nyuma kielimu. Wakaandika juhudi zinafanywa kuongea na mkuregenzi wa ATC. Niliwahi kufikiri kusoma uandishi wa habari, nkaogopa, nkaona ni bora nikawe konda wa malori ya Njombe. Huyu bwana alikuwa safi kumshusha. Kama wana kesi mahakamani, ilichompandisha nini? Na nasikia akinywa, anawasumbua kweli wafanyakazi wa ndege, wa kike. Kaka labda ndege za zamani, sasa hivi watoto wana elimu zao humo ndani. Hawagawi chai kwa shida. Ajira ndio adimu, wanablog kwenu hili.
 
mzee kidumeso nimetuma nondo kama 3,,jaribu kuzisoma utaelewa jamaaa anavyotaka kununua watanzania wote kama anavyowanunua mapolice kule kia
 
Mheshimiwa mwema, hawa watu wako inabidi uwafundishe adabu za kuishi na binadamu wasione watu wote hawaana maana. Nilifurahi kuona mawaziri walikuwemo ndani. Na cha kusikitisha, kuna jamaa alikuwa karibu na Mheshimiwa Buruani. Mama yetu akawa anawaita wafanyakazi wa ndege kuwaambia kuna vitu wanaenda kufungua yule bwana wako nae. Nikasema.
 
Kidumeso kaka walichomogopea unakijua kaka "M....A.....W...E". Huyu bwana anamwaga pesa police kama mchanga, na yule alieagiza gari Defender kule Kia, breaking news, ndio amehamishiwa hapo airport yenu ya Julius Nyerere. Eee Mungu, mnatumia majina ya watakatifu kwenye uwanja uliojaa mafisadi. Haya, yarabi salama kaka, ipo siku tutafika.
 
sasa Mwema ana ubavu gani wakati leo hii anapeleka majina ya watuhumiwa madawa ya kulevya Ikulu ati kwa vile ni Kigogo!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom