Safari za wanaume kuelekea nyumba ndogo zinavyoanza…….!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Huwa haitokei tu kama ndoto, bali kuna mahali inaanzia, ambapo kwa maana hiyo huwa kuna mabadiliko pia. Ingawa sio kweli kwamba mabadiliko yote ya namna hiyo yanaashiria safari hiyo, lakini bado kwa sehemu kubwa ndivyo ilivyo.
Kuna wakati mwanamke anaweza kuhisi kuwa mumewe anamkwepa kwa kiasi fulani kimwili, na kuhisi kwamba hapendwi tena, hivyo kunamfanya awe na ghubu ambalo ndilo linalomfanya mumewe aendelee kumkwepa na kumkimbia kimwili.

Kwa kuwa hajui kwamba ghubu lake ndilo linalomfanya mumewe awe anamkwepa na kupoteza muda wake nje ya nyumbani kwake, kinachoenda akilini kwake ni kwamba mumewe ana nyumba ndogo wakati sio kweli. Hali kama hii huwakuta wanawake wengi kwenye uhusiano. Kama mwanamke yuko kwenye uhusiano wa aina hii inabidi akague utaratibu wake wa kufikiri ili kujenga uhusiano hai na wa kuaminiana zaidi. Mwanaume anapohisi kwamba anadhibitiwa, anafundishwa, anashinikizwa kuonyesha upendo, huwa anahisi kwamba amekataliwa na kutoeleweka.

Kama asipokuwa na busara ya ziada (wengi hawana hata hivyo) huona njia muafaka kwake ni kutafuta ambaye atamkubali na kumwelewa. Hapo ndipo safari ya kuelekea kwenye nyumba ndogo huanza.

Mtambuzi it is not that simple... Pamoja na kusema Uloongea ni kweli kabisa - kwamba mke akiwa committed kwa mumewe aweza epusha nyumba ndogo... Bado ni in most cases ni kazi saaana wakati mwingine ku deal na mume ambae kapoteza mapenzi kwako.... waweza jitahidi kwa kila hali na asilione.... Pia kuna ile ya kusema huyo mwanaume ni hulka yake... kwamba hata uoneshe mapenzi na kumjali namna gani, yeye bila nyumba ndogo hawezi kabisa... (ni tabia mbaya kabisa- but ukweli unabaki pale pale) tena cha ajabu waweza kuta anakupenda saaana tu... but hapo hapo na nyumba ndogo kakuwekea.... Sad.

Nina Mfano ambao nilishuhudia... kuna kaka middle aged ana mke mpoleeee mno - jamii huwa hawawaelewi hawa watu... Mke wake alikuja fanyiwa fujo saloon na nyumba ndogo... What the wife did ni kupiga simu kwa mumewe kua kuna mwanamke anamsumbua hapo saloon... Mda sio mrefu the hubby kafika pale na kweli kamkuta mkewe ndani ya drier (katulia utafikir yule hawara wa mumewe hamtukani yeye - huku rafiki wa huyo dada kaingilia kati na kumtukana kumdefend huyo dada ambae ni mke)... What the hubby did ni kupitisha kipigo kwa hawara pale pale!!! Watu wakajaa pale... Na kumuambia amkome mkewe!! Yaani yule mkewe hata hakutikisika wala kutoka katika ile drier.... Nilijifunza saaana tokana na hilo tukio... For I was impressed!

ashadii,im also impressed na huyo dada. nadhani sio sahihi hata kidogo kum-confront mtu ambae ana uhusiano na mwenza wako. nimeshuhudia kinyume,mdada kaenda kufumania. akapigwa mbele ya hawara.
my take is, u lov something,let it go.if it was urs it will come back.if it doesnt,maybe u ar better off without it! unapoona mwenza anabadilika,ni sahihi kumuuliza kama yuko ok. na akisema yuko sawa, nagging doesnt help. give space, endelea kufanya ur dues na time will tell. huhitaji manati kuwinda,i believe hata shetani akimchoka mtenda ubaya anamfunua mchana kweupee!lakini pia kwa kumpa nafasi mwenzako atatafakari na kuamua kama kweli ana haja ya kufunga kitabu alichoandika kwa miaka kadhaa ama bado. sometimes silence is the best answer (inatuhusu wadada zaidi!)

Unajua ukimfuatilia mwanaume ni kama unamwambia aongeze speed.Dawa ya mme anaechiti ni ku cool down.Ukimfuatilia anaona kama huwezi ishi bila yy,kaa kimya ataanza kujisogeza mwenyewe

ashadii,im also impressed na huyo dada. nadhani sio sahihi hata kidogo kum-confront mtu ambae ana uhusiano na mwenza wako. nimeshuhudia kinyume,mdada kaenda kufumania. akapigwa mbele ya hawara.
my take is, u lov something,let it go.if it was urs it will come back.if it doesnt,maybe u ar better off without it! unapoona mwenza anabadilika,ni sahihi kumuuliza kama yuko ok. na akisema yuko sawa, nagging doesnt help. give space, endelea kufanya ur dues na time will tell. huhitaji manati kuwinda,i believe hata shetani akimchoka mtenda ubaya anamfunua mchana kweupee!lakini pia kwa kumpa nafasi mwenzako atatafakari na kuamua kama kweli ana haja ya kufunga kitabu alichoandika kwa miaka kadhaa ama bado. sometimes silence is the best answer (inatuhusu wadada zaidi!)

Mungu Wangu King.... imeniuma hapo blue... yaani wanaume sometimes.... Yaani unashindwa saa ingine kuelewa moyo wako kwa nini unapenda such a guy... it is so degrading.... alafu na haya mambo ya kufumaniana haya.... Dah!

Yaani hio paragraph umeelezea vizuri na nimeipenda King... Mie najua akifanya kitu kama hicho alafua anajua unajua (na huna mpango wa kuondoka) it is better kweli ukae kimya - akae aking'ang'a macho kutafakari when you will ask... Mwingine ataogopa hata kula chakula kuona utamuwekea sumu...lol.. But ni vizuri apata internal pressure... Ingawa kuna waume hata hatajali

lakini yataka moyo si kidogo!kuogopa kupigania kilicho chako is it easy na sisi ni binadamu? Nakubali hata wake wanachangia kumshawishi mume kutafuta pumziko. Shida ni kitchen party zisivyo na tija katika kumuandaa binti.

Maria... kupigania chako inahitaji utumie intelligensia na usikurupuke for ukitumia pupa waweza kikosa pia....

Duh! Huku kupigania changu mnakozungumzia hapa ni kupi? Yaani Mr ana hawara, afu hawara anakuja saluni kunifanyia fujo nami nanyanyuka nafunga kibwebwe npigana na hawara au?! Sijawaelewa

laiti wanawake wangejua....
hakuna kitu kinachotisha kama mwanamke anapokaa kimya kabisa
huku unajua umemtendea visivyo.....

her silence speaks so loud.....

huyo dada wa saloon aliyetulia tuli,labda aliogopa kudundwa hahaaaaaaaaaaaaaaaa maana kupigana unaangalia na unayepigana naye kwanza kama una kifua....lol

huyo dada wa saloon aliyetulia tuli,labda aliogopa kudundwa hahaaaaaaaaaaaaaaaa maana kupigana unaangalia na unayepigana naye kwanza kama una kifua....lol

lol............ Waswahili kwa maneno.... Umenichekesha kweli.... Dah!

laiti wanawake wangejua....

hakuna kitu kinachotisha kama mwanamke anapokaa kimya kabisa

huku unajua umemtendea visivyo.....

her silence speaks so loud.....

Hii ndo dawa japo wengi hawaiamini

laiti wanawake wangejua....
hakuna kitu kinachotisha kama mwanamke anapokaa kimya kabisa
huku unajua umemtendea visivyo.....

her silence speaks so loud.....

The Boss ni kweli kabisa but it only workks kwa wanaume ambao ni magentlemen kama wewe, mwingine ukimkalia kimya ndo anaona umetoa green light!! .............Nilikuwa naye mie wa hivyo loh!! Yule alikuwa wa aina yake kwa kweli......ukikaa kimya anarudia tena kusudi, ukisema anakuja juu yeye ah!!

Ahaa!! Afadhali maana MWJ1 mie nsivyojua kupigana ah aku...............ntamtizama tu afanye vibweka vyake ikisha tutaongea vizuri na Mr. anieleweshe nimuelewe!!

Basi huyo alokaa hapo ndio definition ya MJ1.... Hakufanya kitu zaidi tu ya kutaarifu the hubby (naona anamjua mumewe kua pamoja na kusema kiwembe kwake hafurukuti...)

Kweli inataka moyo. Swala la kupigana au ku ignore ni hulka ya mtu. Mimi sina nguvu lakini nikimjua mwizi wangu kwa kweli siwezi kum ignore japo nakubali yaweza kuwa ni best strategy.

lakini yataka moyo si kidogo!kuogopa kupigania kilicho chako is it easy na sisi ni binadamu? Nakubali hata wake wanachangia kumshawishi mume kutafuta pumziko. Shida ni kitchen party zisivyo na tija katika kumuandaa binti.

........... sometimes silence is the best answer (inatuhusu wadada zaidi!)

hii ni kweli kabisa na kina mama wengi wangekuwa wanalielewa hili kusingekuwa na matatizo mengi kama ilivyo sasa. nijuavyo mimi wanaume wengi hawapendi kelele (GHUBU) wanatamani warudipo nyumbani wapakute pako cool endapo wakifika na kukumbana na kelele basi hupanga safari ya kwenda kupumzika nje ya nyumbani na ndio huko hukutana na midogo yenye asali ya mahawara na mwisho wa siku wanajenga vibanda huko na kutelekeza familia. naamini kila jambo ambalo couples wanadhani linaweza kuhatarisha uhusiano wao ni vema kuliweka wazi, kujadili na kutafuta way forward. in most cases amani inavunjika kwa sababu ndogo tu - communication brakedown. ukiona tatizo husemi unabaki nalo rohoni unalimbikiza mambo mwisho wa siku ni chuki, magomvi n.k.

Back
Top Bottom