Safari za viongozi kwa kigezo cha kuvutia wawekezaji: Wazo mbadala

everybody

JF-Expert Member
Oct 30, 2010
337
103
Kumekuwa na safari nyingi zikimhusisha mkuu wetu wa nchi, waziri mkuu, mawaziri na viongozi wengine wa serikali na safari hizi tunaambiwa zina malengo ya kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania. Kwa mawazo yangu ninaamini kwamba kabla kiongozi hajaondoka Tanzania kwenda hiyo nchi anayokusudia atakuwa amekwishafanya mawasiliano na wenyeji wake na anajua anakwenda kukutana na nani na tayari watu atakaokutana nao wana walau hint (tetesi) ya kitu anachotaka kuongea nao. Tukijaribu kuangalia misafara ya viongozi hawa wanapokwenda huko nje nahisi gharama yake ni kubwa (nasema nahisi kwakuwa sina figure kamili) ukilinganisha na return zilizotokana na safari zilizokwishafanywa.
Hivyo basi, kwa mtazamo wangu naona ni bora hizo fedha wanazotumia hawa viongozi wetu kwenda huko nje zitumike kuwalipia hao prospective investors waje hapa Tanzania na mazungumzo yafanyikie hapa hapa. Nasema hivi kwa sababu zifuatazo:

1. Itasaidia kupunguza gharama. Kumlipia mtu hoteli Tanzania inaweza kuwa cheap kulinganisha na gharama ambazo msafara wa Rais unatumia kwenda nje ya nchi. Gharama ya msafara mmoja wa rahisi nahisi unaweza kuwalipia hata wafanyabiashara wakubwa watano kutoka Marekani au Ulaya wakaja Tanzania na tukafanya nao mazungumzo
2. Kufanyia mazungumzo ya uwekezaji Tanzania inaweza kuwa productive zaidi kwa kuwa huyo mwekezaji anaweza kuomba kujionea hizo fursa za uwekezaji na hata akitaka kufanya maamuzi anafanya akiwa anaelewa mazingira yenyewe. Hi ni tofauti na kama Rais anafunga safari kwenda Marekani, anakutana na wafanyabiashara wa Marekani, then hao wafanya biashara wafunge tena safari kuja kujionea hizo fursa Tanzania kabla ya kufanya maamuzi ya kuwekeza. Hii ni gharama mara mbili kwa mtazamo wangu na hasa pale huyo mwekezaji anapoona mazingira hayafai kuwekeza.

Hivyo basi, kama madhumuni ya safari za Rais na viongozi wengine ni kuwavutia wawekezaji na sio kukusanya per diems (around $400 per day) kwa siku wanazokaa nje ningependekeza wajitahidi hayo mazungumzo yafanyikie Tanzania kwa kuwalipia hao wawekezaji gharama za kuja Tanzania.

Sijui wana JF mnaonaje?
 
Hao wawekezaji watawekeza nini wakati umeme hakuna???? akae ashughulikie umeme
 
Waziri wa Uwekezaji anafanya nini? Prime Minister anapanda ndege kwenda kuongea na mfanyabiashara Brazil? bad taste to say the least.
 
bunge limeahirishwa, hakuna ishu ya Zitto kudaiwa ushahidi ila m'bunge mwingine wa upinzani (Ms. Sakaya, CUF) ametakiwa kuleta ushahidi.
 
Waziri wa Uwekezaji anafanya nini? Prime Minister anapanda ndege kwenda kuongea na mfanyabiashara Brazil? bad taste to say the least.

Sijui tuseme ni dalili za kutokuaminiana. Unampa mtu aongoze wizara halafu bado unataka wewe ndo uwe mtendaji hapo hapo
 
Back
Top Bottom