Safari za Kwenda kwa Babu Loliondo: Viongozi na Mashangingi ya Serikali Walalahoi na FUSO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari za Kwenda kwa Babu Loliondo: Viongozi na Mashangingi ya Serikali Walalahoi na FUSO

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimbunga, Apr 3, 2011.

 1. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  WanaJF nimekuwa nikifuatilia mambo mbalimbali tangia ujio wa Babu wa Loliondo. Ufuatiliaji wangu umejikita zaidi juu ya watu wanaoenda kwa Babu. Ni jambo ambalo haliwezi kupingika kwamba makundi ya watu wanaoenda kwa Babu yanadhihirisha kwamba hamkani si shwari Tanzania; Watanzania karibu wote tu wagonjwa: Si Mawaziri, viongozi wa Serikali, Majaji, Wabunge, Madiwani, nk. Wote ni wagonjwa, si tumewaona ama kusikia kuwa wameenda kwa babu na kupata kikombe kinachoaminika kuponya magonjwa sugu yakiwemo UKIMWI, Kansa na Kisukari. Kuna wengine wanasema wamekunywa kwa sababu ya curiosity tu!!! Siamini kama ni curiosity kwa kuwa Babu alishasema kwamba dawa yake si kinga bali wainywe wagonjwa tu: Hii imenifanya niamini kwamba wanaoenda na kunywa kikombe basi wote ni WAGONJWA!
  Suala langu hapa sasa ni kwamba kama sote tu wagonjwa, inakuwaje viongozi wenye mamlaka watumie rasilimali za serikali (Mashangingi na huenda Per diem) kwenda kunywa dawa ilihali wafanyakazi wengine wa serikali na wananchi wengine ambao si wafanyakazi wakihangaika ki vyao kujitafutia usafiri (FUSO hayaaa, Mabasi mikweche, hayaaa) kwa gharama zao kuelekea Loliondo? Kama serikali imeamini (Mimi siamini) kwamba ile ni tiba kama ilivyo ya Muhimbili na viongozi wake wanaenda kupata tiba hiyo kwa gharama za serikali, ni kwa nini isiandae utaratibu wa kiwafikisha wagonjwa huko kwa babu kwa gharama za serikali kama ambavyo viongozi wanaenda kwa gharama za serikali? TUTAFAKARI
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mods plz fungueni jukwaa la babu wa loliondo!!

  tumechoka, kila kona babu babu!!!
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Kwa tz ilishazoeleka mali za walipa kodi kutumiwa na wakubwa kwa mambo binafsi.
   
 4. L

  Leliro Member

  #4
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unadhani kwanini tz ni maskini? ni kwa sababu ya mambo kama haya. Hainijii akilini nchi yenye raslimani lukuki wakiwemo maprofessa na amani ya kuishi tele kuzidiwa na nchi kama Rwanda. Perdiems na mafuta ya magari yasiyotenganisha shughuli binafsi na za kikazi ndo chanzo kikuu cha umaskini. Usishangae hata hawala za hawa wakubwa kutumia mashangingi na perdiem za serikali; wakati fulani hata plate number za magari yanayoenda loliondo zikawa zimebadilishwa na kuweka za pikipiki au buldozer zilizokufa. Bado safari ya kuutupa umasikini tz haijaanza!!!
   
Loading...