Safari za JK zamuudhi Filikunjombe

basi kwa miaka ya JK bajeti ya ikulu imekosewa, watampangiaje safari raisi mwaka mzima kwani yeye ni katibu mkuu ya UN??

Kama Filikunjombe sio Mnafiki basi alitakiwa apinge kwa nguvu zote Bajeti ya Ikulu inapowasilishwa Bungeni na kutamka hayo aliyonena.

Kwani itakuwa kichekesho wakti kaipitisha kwa aslimia zote ndani ya Bunge kisha anatoka nje ya Bunge na kulalama.

Huo ni Unafiki.

 
Hapo sielewi yaani anafunguka mara moja ndo anakuwa mpiganaji?

Hapo anajikosha kama ni mpiganaji kweli mwambie aendelee kufunguka na mengine sio
kusema mara moja then anafunga mdomo

Huyo jamaa kufunguka anajitahidi sana hata huku ludewa tunamkubali sana huyo kijana, ameleta changamoto kubwa sana yeye binafsi, ila ccm inamdondoshea cv huyu kijana, kwani wakiwa kama ccm wanalazimishwa kutetea ujinga kwa nguvu zote
 
huyo mb ni mbunge wangu namkubali sana ingawa yupo kwa magamba, aliwahi kupinga pia matumizi ya mabilioni ya pesa kutumika kwenye sherehe za uhuru akidai kuwa wananchi wa jimbo la ludewa hawana umeme wala barabara ya lami kwa hiyo bado hawajapata uhuru ndani ya miaka 50 wakati serikali inatumia pesa nyingi kuazimisha sherehe hizo,pia alisema atahamasisha wanaludewa waandamane kama barabara ya jmboni kwake haitawekwa kwenye budget. naamini siku moja ataungana na makamanda kupigania haki maana ameshaujua ukweli
 
WAKUU, Nimefuatilia kipindi cha TBC Jana, Deo filikunjombe Mh. Mbunge wa Ludewa aliilaumu serikali kwa kuua viwanda, Polisi kupiga mabomu wanafunzi wakiandamana kudai mikopo wakati wanaostahili kupigwa mabomu ni wezi wa pesa hizo pamoja na uongozi wa Mkwawa University, aliongeza pia, kuna uzembe mkubwa serikalini unaosababisha viwanda vife, alitaja bodi chafu na dhaifu mbaya kabisa ni badi ya pamba, alimtaja CEO Dhaifu, Mbadhirifu, na asiyefaa kabisa ni wa TBS, Alisema hayo pamoja na mambo mengine yamesababisha CCM kupigwa Arumeru. Alifupisha kwa kusema, "Tatizo ni Serikali ya Tanzania ikiwa mfano wa Timu ya wachezaji 11 wa mpira imeshindwa kabisa kufunga magoli". Alisema kuna matatizo makubwa serikalini kushindwa kufanya maamuzi muafaka wakati unaofaa, mfano alisema soko la kariakoo halina bodi kwa zaidi ya miaka minne, alisema pia, kuna mashirika mengi Tanzania yana udhaifu mkubwa kiutendaji na yatakufa kwa uzembe wa serikali kutochukua hatua.

Naona kama huyu kijana ana Mawazo ya kuungwa mkono.
Je. CCM itaweza mwelewa na kuleta mabadiliko au.......
 
Mh.Deo Filikunjombe huwa namkubali sana kati ya wabunge wa magamba.Michango yake huwa inatia hamasa sana.Sasa pamoja na yote hayo nina wasi wasi na weledi wake kuhusu kama kweli ana dhamira halisi katika hicho anacho kiamini na kukipigania.

Ni ukweli usio pingika kuwa meli anayo safiria(magamba) haito mfikisha aendako.Sera anazo simamia ni mbovu,raisi,mawaziri,na viongozi wote wa serikali wabovu.Kwa hiyo hafiki kokote.Namshauri awe kama Bw.Millya ajivue gamba kwa kutoka aliko ili ajiunge na makamanda.
 
Tatizo lao ndo hilo.
Huku wanapinga, kwenye eneo wanalotakiwa kutetea nchi kwa kuweka sheria za kulinda haya,
'Wanaunga mkono hoja'

Hii si akili.
huyu jamaa kidogo ni tofauti nimemftilia muda mrefu ni mashine
 
alama za nyakati...Senegal fundisho zuri utaona wengi sana sasa wanaongea kana kwamba wanaanza kujitenga. Sally alipoona Mzee Kagoma alihama, let us see kama wanajifunza...mmoja mmoja anatengeneza mazingira ya upenyo. ili ikilazimu wakubalike CDM
 
jamaaaa anajitahidi kwa kweli ila jimbo lake kule noooma ......si ndo kwa KOLIMBA kule ...naona itakuwa ngumu kujivua gamba labda anaogopa hahahahahahaha
 
Akielezea utumiaji mbaya wa madaraka serikalini na mashirika ya umma filikunjombe amesema nchi nyingine raisi hawezi kusafiri bila ya bunge kuidhinisha safari. Amesema kipigo magamba walichokipata arumeru ni fundisho tosha jinsi wananchi walivyokata tamaa na ccm. Source-kipindi cha jambo leo tbc1

Yupo Brazil anakula bata!
 
Back
Top Bottom