BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,148
Tambwe, Akwilombe, Mbeya hakuna wajinga
Christopher Nyenyembe
Tanzania Daima
KAMA unataka kujua historia ya mkoa wa Mbeya kuhusu elimu, ustaarabu na uelewa wa wakazi wa mkoa huo ni vyema utafute njia nyingine ya kuwafanya Watanzania wengi wajue kuwa huko kuna mambumbumbu.
Mbeya katika historia yake sio mkoa wa kubezwa katika maeneo yote muhimu, mkoa huo una historia ya kutoa wasomi wengi na waelewa, mkoa huo una utashi mkubwa wa kisiasa kwa watu wake na mkoa huo unajitosheleza kwa kila idara ndani ya jamii.
Lakini cha kushangaza na pengine kimenivuta zaidi niwaeleze hawa ndugu zangu wanaojiita wanasiasa na makada maarufu wa propaganda, ndugu yangu Shaibu Akwilombe na Richard Tambwe Hizza, kuwa kazi waliyopewa ndani ya CCM si ile waliyoifanya ndani ya upinzani walikotoka.
Inashangaza na inahuzunisha kuwaona makada wanaojiita kuwa wakomavu wa siasa za upinzani wakihama kutoka nyumba moja hadi nyingine kwa misingi ya kubomoana badala ya kushawishi ujenzi wa taifa la haki na demokrasia.
Ni ajabu na kweli hawa ndugu zetu walipopewa nafasi ya kuwasalimia wakazi wa Mbeya katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Ruanda Nzovwe jijini humo, walitoa siri ambayo pengine isingepaswa kuelezwa na mtu yeyote mwenye akili na utashi wa kibinadamu, pale mtu anapotamka matamshi ya kejeli kuwa wao ndiyo wauaji.
Wanatamka hadharani kuwa walipokuwa kwenye kambi ya upinzani ndio waliokuwa wapika majungu wakubwa na ndio waliofinyanga propaganda nyingi za uongo za kuichafua CCM ili ichukiwe pande zote mbili Bara na Visiwani.
Ndiyo makada hao wanavyozungumza kwa vinywa vyao, wakipaza sauti kuwa wameamua kuondoka upinzani na leo wanakuja kukiri madhambi yao kwa wakazi wa Mbeya ili waonekane kuwa wanafaa na walifanya hivyo kutokana na ujinga wa kisiasa.
Bila kujali uchungu na madhara waliyoyapata Watanzania wa Zanzibar, Hizza anatamka bayana kuwa ndiye aliyekuwa kinara wa kuwashawishi wana CUF wafanye vurugu visiwani humo wakipinga matokeo ya uchaguzi na kusababisha wananchi wapatao 27 wapoteze maisha.
Leo Mbeya anakuja akidai kuwa anawaomba radhi kwa kazi mbaya aliyokuwa akiifanya ya kuwashinikiza wananchi wafanye vurugu kwa kuwajaza mori na jazba za kisiasa ili waichukie CCM na kuiona kuwa ni cha mauaji na si chama cha mapinduzi ya kweli kwa maisha ya Watanzania.
Akwilombe na Tambwe wanatamba waliyoyafanya CUF huko Zanzibar. Wanawakumbusha Watanzania machungu ya vifo vya wenzao waliokufa kwa shinikizo la kupinga ushindi wa Rais Amani Abeid Karume, lakini hivi leo wapo CCM ndiyo waziri wao.
Wanadiriki kuweka wazi msimamo wao wakiwageuza wananchi kuwa viraka vya kujazia maslahi yao ili waonekane wema mbele ya watu na kuuonyesha uongo walioupika na kuukiri ugeuke kuwa ukweli na CCM wanawafurahia.
Sikutarajia uzito wa hoja hizo zinapotolewa bendi ya muziki wa dansi ya TOT Plus inaposimama kidedea kubariki maneno yao, wakiwashangiliwa kuwa lazima wapinzani 'washikishwe' adabu, Watanzania wenzao kwa kushindwa kusimamia maslahi ya nchi hii, inashangaza.
Kwa kauli zao inaonyesha ndiyo waliyoifanya CCM na CUF huko Zanzibar kusikalike na mwafaka usifikie mwisho, kumbe walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya kuwaghilibu wananchi sasa wanajiweka hadharani kuwa hayo yote yaliyotokea wao ndio walikuwa wapika majungu wakuu.
Leo wanasimama majukwaani wanataka kuwafanya wakazi wa Mbeya kuwa ni mbumbumbu 'mzungu wa reli' na kuwafanya Watanzania kuwa kurudi kwao CCM kumetokana na vyama vingi vya upinzani kuongozwa katika mfumo wa kifamilia.
Wanasahau kuwa walipokuwa upinzani ni jinsi gani waliitukana CCM na kukibeza chama hicho kuwa ni Chama Cha Mauaji, lakini leo hii wamekisafishia wapi kutokana na historia ya Zanzibar, ili waonekane kuwa wasafi na wanapaswa kupewa sauti ya kurudi upya kuwabeza wananchi wakiwaomba radhi.
Ndiyo maana nasema hivi wasidhani kuwa mkoa huo una wajinga. Hebu warudi nyuma waangalie kwenye orodha ya watumishi wa serikali tangu nchi hii ilipopata Uhuru waangalie na kujiuliza ni wananchi wangapi wa mkoa huo walioona fahari ya kuwasomesha watoto wao.
Lakini kikubwa ni pale wanapodiriki na kuwaeleza wananchi kuwa walishindwa kuhimili mikikimikiki kwenye kambi za upinzani kwa madai kuwa Chadema ni chama cha kifamilia ndiyo maana Tambwe aliamua kuondoka huko bila kujiuliza ni nani asiyeijua historia ya CCM na vizazi vyao.
Wakati wanampinga Rais Karume huko Zanzibar wakiwa CUF na leo wamerejea tena CCM, hawajui kuwa rais huyo ni kizazi cha familia ya uongozi kutokana na historia ya baba yake mzazi aliyekuwa Rais wa Kwanza Zanzibar , wanajifanya wamesahau.
Tambwe na Akwilombe leo hii wanamuona Dk Hussein Mwinyi, Waziri wa Muungano, kuwa ni kada mwenzao ndani ya CCM. Wamesahau walipokuwa wakimtupia makombora kuwa kizazi hicho kinapeana uongozi na hawakumbuki kuwa huyo ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu wa Pili, Mzee Ruksa, Ali Hassan Mwinyi - hayo hawasemi.
Hawawaambii wananchi ukweli jinsi viongozi waliopo madarakani wanavyopeana vyeo na kazi wao kwa wao kwa mfumo wa kifamilia. Hayo yote na makubwa zaidi yamejitokeza kwenye kugombea nafasi ndani ya chaguzi za CCM familia nzima inalilia kuingia NEC, hawayasemi hayo wanataka kuwafanya wananchi wajinga.
Leo ndugu yetu Makongoro Nyerere ndiye aliyekuwa kijana wa kwanza kutoka kwenye familia yenye heshima na kujiunga na upinzani hadi akaukwaa ubunge, na leo hii amesimama upya amepewa heshima ya kuwa mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara. Hayo hamyasemi wala hamkumbuki kuwa Rose Nyerere alikuwa Mbunge wa Viti Maalum bila kutaja aliupataje.
Tanzania ya jana si ya leo, huwezi kujenga nyumba kabla hujaishi unaamua kuwapa watu waishi bure kwa madai kuwa nyumba hiyo isionekane kuwa ni ya kifamilia, sijui hiyo falsafa imetoka wapi nikiamini kabisa mshikamano na itikadi za kichama pia kuanzia ngazi ya familia ni nani asiyejua hilo.
Watu wa Mbeya na Watanzania wote wanajua hivyo wakiamini kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alipokuwa akipigania uhuru wa nchi hii familia yake haikubweteka na kumwachia mwenyewe aifanye kazi hiyo, ni wazi kuwa pia alipata mchango mkubwa kutoka kwenye familia yake na kisha kuungwa mkono na watanzania wote waliokuwa wakiitakia mema nchi hii, hilo lipo wazi.
Sasa hawa ndugu zetu wanasimama wanataka kuwasahaulisha Watanzania wenzao mifumo ya kiutawala ilivyo wakidhani kuwa utawala unaweza kusimama wenyewe bila mhimili wa pamoja. Kama wamekimbia upinzani ni wazi pia wamekimbia na familia zao kwenda CCM kwani huko ndiko wanakoshibia.
Kama waliona kuwa kwenye kambi za upinzani kuna sisimizi kama anavyodai ndugu yetu Akwilombe, na ujuzi wao wa kuzihamisha propaganda za upinzani kuziingiza CCM kwa kuwa huko kuna shibe, ni wazi kuwa hawawezi kuziacha familia zao zikifa na njaa.
Wanawaeleza wana wa Mbeya na Watanzania wenzao kuwa wao si wahimili wa kweli katika ulingo wa kisiasa kutokana na historia yao ya kuhama kutoka chumba kimoja hadi kingine wakiwa na sababu tele za kuuponda upinzani, wakiwaona wapinzani kuwa si Watanzania na hawana haki ya kuwa viongozi. Hawa ndiyo wale kule Zanzibar tunaowaita "Vinuka mito".
CCM imewapokea kwa mikono miwili ikiamini kuwa imewapata makada safi wa propaganda waliokimbia upinzani na sasa kazi hiyo wanaweza kuifanya kwa ufanisi mkubwa wakiwa ndani ya CCM.
Napenda kuwashauri na wayatafakari kwa kina maneno ya hekima ya Mbunge wa Jimbo la Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, aliyoyasema wakati wa mkutano wa viongozi wa CCM walioufanya Mbeya, kuwa ili chama hicho kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kwa kishindo, ni vyema kitekeleze kwa vitendo ilani ya uchaguzi.
Hilo ndilo jukumu kubwa lililopo mbele ya CCM na watendaji wake wakuu wa serikali. Hakuna haja ya kupanda majukwaani na kuusakama upinzani wakati jukumu kubwa mlilo nalo ni lile la kutekeleza ilani yenu ya uchaguzi. Watu wanataka kuona mambo kwa vitendo na sio maneno.
Watu wanataka kuona umasikini unatoweka kwa kupata elimu bora, huduma za majisafi, afya, barabara nzuri na zinazopitika kipindi chote cha mwaka, kilimo cha kisasa na soko nzuri la mazao ya wakulima. Mambo hayo ndiyo yatakayoijibu falsafa ya Rais Jakaya Kikwete ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
Bila kutekeleza hayo lazima msome nyakati, ziangalieni sura za watu, watu wamechoka wanahitaji mapinduzi makubwa ya kiuchumi badala ya bla bla za kisiasa majukwani, wanalalamikia makali ya maisha na bajeti ya mwaka 2007/2008 waelezeni kuhusu hayo.
Hebu jibuni maswali yao kuhusu tuhuma za ufisadi zinazotolewa kwa baadhi ya watendaji ili mjisafishe mapema kuliko kusimama mbele ya wananchi mkiwaeleza kuwa wapinzani hawana ushahidi, wananchi wamejazwa upepo wa mabadiliko ya kweli na hawapo tayari kudanganywa, tekelezeni ilani yenu.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu: 0754 301 864 au barua pepe; cnyenyembe@yahoo.com