Safari yangu katika jimbo la HAI (Jimbo la Mh Mbowe)

safi saaaaaaaaaaaaana umeongeza idadi ya watalii wandani,vp ulifanikwa kuonja mbege ya Hai,sasa jitahdi ufike na uku kwetu Liwale,Nachingwea,Nanjilinji ili ufananiushe.
 
Mleta mada yawezekana hata mlima hakupanda kilimanjaro alifuata majungu Mbowe sie aliyeua viwanda na sie aliharibu uchumi wa nchi hii na sie aligawa vitalu na migodi wa wageni kienyeji swala la vijana kukosa ajira ni chama kilichopo madarakani.Msaidien kutofautisha kati ya guest huse na hotel.Swala la maji je mbowe ana wizara.Je vipi kuhusu majimbo yanayomzunguka.
 
mi nimetokea machame, kijiji kimoja na mbowe cha nshara.
Utajiri wa mzee aikaeli babake mbowe hakuna asieujua.
Suala la kujadili hoteli ni majungu na fitna.

Suala la msingi ni kuwa mbowe yuko bize sana na masuala ya chama kitaifa, kalisahau jimbo.
Kampuni ya maendeleo jimboni alio ianzisha inasuasua, ameshindwa kui fumd na baadhi ya wafanyakazi ikiwemo mkurugenzi wake amesha acha kazi.
Kuna tatizo la ajira kwa vijana na hiyo kampuni ilianza vizuri kwa kutoa mafunzo ya kuongoza watalii kupanda mlimani kwa vijana wasio na ajira.
Wakulima wengi wamekuwa wakipata hasara kila mwaka kwakuwa mvua zinakatika wakati mazao (mahindi) yakiwa ktk hatua za mwisho huku mito inatiririsha maji mengi.

Hilo ni tatizo la wabunge wengi, sio ccm wala cdm, wengi wametelekeza majimbo.
 
Yeye kajenga MAHEKALU yanakaa MAPANYA mwenziye kajenga HOTELI inakaa watalii:


msoga.jpg

na inatoa ajira kwa Watanzania na kununua mbogamboga kwa wanavijiji wa Machame
 
Haujafanya survey yoyote bali ni chuki binafsi na majungu tu hapa. Njoo ujionee hali ilivyo mbaya huku Iramba mashariki.
 
Post imejaa wehu mtupu,mbowe ni tajiri tangu enzi za ujio wa vasco da gama.Njoo sumbawanga na pumba zako hizo urudi uchi maaana hata lami ni mafumbo
 
Nikiwa nimepata likizo fupi, niliamua kwenda mkoani kilimanjaro kwa ajili ya kupanda mlima wetu maharufu wa kilimanjaro, nikiwa huko niliweza kupata fursa ya kutembelea majimbo ya mkoani kilimanjaro ila nilitaka kuona kwa macho yangu jimbo la HAI la MH MBOWE MWENYEKITI WA CDM TAIFA! kwakweli niliyoyaona huko hayaendani kabisa na mbwembwe za huyu jamaa anayetembea nchi nzima kuhubiri maendeleo na demokrasia, vijana wa pale machine tools wamekata tamaa na maisha, mbunge wao anashindwa kufanya yale aliyowahidi, wakazi wa kimashuku mnadani wanalia shida ya maji, wakazi wa uroki hali yao kiuchumi na kipato iko mbaya, wengi wao wanalia na wanajuta kumchagua Mbowe! wengi walisema kuwa Mbowe sio kiongozi mbaya ila ni kwamba yupo bize sana na mambo ya taifa na kuwasahau wapiga kura wake! walisema kama Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti wa chadema, basi 2015 watachagua mtu mwengine atakayekuwa karibu nao

nilifika hotelini kwake AISHI-PROTEA HOTEL... kwakweli Mbowe ni Bepari kwa mtanzania wa kawaida kumiliki ile hoteli sidhani kama ni rahisi....wakazi wa maeneo ya pale hawawezi kwenda kuingia kwa ile hoteli, wengi niliyowaona ni wazungu na raia wengine wa kigeni, kulikuwa na umuhimu gani kujenga hoteli kubwa kule kijijini kwake ilhali wapiga kura wake hawawezi kwenda hata kununua soda au chai?

Ulitaka ajenge Dar?
Huoni kuwa kapeleka ajira kule, watalii wanaacha dola pale?
Hujui kuwa kapeleka soko kwa bidhaa za chakula kwa wananch wa kule?
 
Mzigo wa mpumbavu kumtua yahitaji timing, vinginevyo anaweza kukutwisha ngumi akidhani unamwibia. Hivi umeona ukileta upuuzi huu hapa, kuna watu wataamini kuwa Mbowe hafai??? Umechelewa sana.
 
Ungefikiria Ulicho andika kabla...
1.Ajira Tanzania
2.Umaskini
3.Pato la Taifa na Maendeleo
4.Elimu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Mkuu, usimalizie hasira zako kwa jimbo hilo moja. nenda majimbo mengine, anzia kwa Pinda, kwa Membe, kwa Magufuli etc uone iwao kunaahuweni kwa wananchi, hususan vijana. halfu urudi humu ndani utueleze.
Umenena! Kama Mujumba anao Jimbo la Hai hakuna cha maana basi amezaliwa Ulaya au Marekani
na ndio mara ya kwanza kuja TZ. Namshauri atembelee majimbo mengine ya mashambani nje ya Kilimanajro ndipo atajua umasikini tulionao.
 
Duh Mkuu umenena, kabla hujafika pale Msoga fanya tathmini pale CHALINZE MZEE uone watu walivyochoka!

sio wamechoka yaani pwani kwa ujumla ongelea ngono na umbea ndio utawapata kwenye kunema watoto na cheleko ndio zao yaani kwa kifupi ni wafu walio hai
 
Politics aside:

1. Vijana wa machine tools uliwauliza lolote au na wewe ni kati ya wale walotutenga wanao-judge watu kutokana na mavazi au muonekano??? Ulikaa nao mpaka wanapofunga siku ujue wanarudi home na bei gani mfukoni apart from manunuzi????
- Wana Mashamba yao
- Pale wako kijasiriamali, wanapakia mizigo.
- Fly Catchers
- Mountain Climbers
- Toyo Riders
- Mama/Baba Ntilies.

2. Kuna aliekuibia kutokana au aliekukimbiza?? Mpaka useme wana tabu???

3. Kimashuku wale ni mountain Climbers na Fly Catchers.

4. Mbona usiseme miradi waliowekeza Boma??? (Ulikuwako au fanikiwa kuiona Boma enzi za CCM?).

5. Unajua Aishi Protea imewaajiri (ajira rasmi na zisizo rasmi, watanzania wangapi?).

6. Unajua Aishi inachangia kiasi gani kwa akiba ya Pesa za kigeni??
- kodi?
- mapato mengine yatokanayo na Utalii???
- we need Hotels kama hizo.

7. MOSHI MJINI. Unajua personally Ndesa kawasaidia wanajimbo na wageni wangapi??

8. Keys Hotel. (Rejea Namba 6 hapo juu) faida zinafanana.


Popote pale lazima kutakuweko wavivu, na maskini. Lakini pia usisahau Con-Artists. So hizo siku chache hazitoshi wewe kupata conclusion kama hii.

Hata mimi leo ukijileta nikaona unaleta tambo za ileri(pesa) ukiniuliza nakuambia maisha magumu ili unitoe ileri nikapige wari.


Nakushauri rudi tena kafanye utafiti wako halafu uje hapa na Jimbo lingine lililo chini ya CCM ama The Swahibaz CUF ufananishe.

Precise analysis. Thanks pal.
 
mbowe ni kiongozi..Tunamuona

i wish Tanzania kungekuwa na akina mbowe milioni moja tusingekuwa na tatizo ajira kama yeye mwenyewe ana wafanyakazi zaidi ya mia moja, nani tanzania hii angekuwa bila ajira. wako watanzania wenye pesa kuliko yeye lakini wamezificha uswis wazungu wanazitumia kuwekeza kwenye mashirika yao(private equity) na yanawafaidisha wao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom