Safari yangu katika jimbo la HAI (Jimbo la Mh Mbowe)

Mbowe anapesa wewe Nenda kijijini kwao Nshara ukaone wanavyomsujidia halafu nasikia kuna shamba baba yake alimrusha mtu yeye mwenyewe anajua na wanalingania mpaka leo
 
Duh Mkuu umenena, kabla hujafika pale Msoga fanya tathmini pale CHALINZE MZEE uone watu walivyochoka!

chalinze1.jpg.scaled.1000.jpg
 
Nikiwa nimepata likizo fupi, niliamua kwenda mkoani kilimanjaro kwa ajili ya kupanda mlima wetu maharufu wa kilimanjaro, nikiwa huko niliweza kupata fursa ya kutembelea majimbo ya mkoani kilimanjaro ila nilitaka kuona kwa macho yangu jimbo la HAI la MH MBOWE MWENYEKITI WA CDM TAIFA! kwakweli niliyoyaona huko hayaendani kabisa na mbwembwe za huyu jamaa anayetembea nchi nzima kuhubiri maendeleo na demokrasia, vijana wa pale machine tools wamekata tamaa na maisha, mbunge wao anashindwa kufanya yale aliyowahidi, wakazi wa kimashuku mnadani wanalia shida ya maji, wakazi wa uroki hali yao kiuchumi na kipato iko mbaya, wengi wao wanalia na wanajuta kumchagua Mbowe! wengi walisema kuwa Mbowe sio kiongozi mbaya ila ni kwamba yupo bize sana na mambo ya taifa na kuwasahau wapiga kura wake! walisema kama Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti wa chadema, basi 2015 watachagua mtu mwengine atakayekuwa karibu nao

nilifika hotelini kwake AISHI-PROTEA HOTEL... kwakweli Mbowe ni Bepari kwa mtanzania wa kawaida kumiliki ile hoteli sidhani kama ni rahisi....wakazi wa maeneo ya pale hawawezi kwenda kuingia kwa ile hoteli, wengi niliyowaona ni wazungu na raia wengine wa kigeni, kulikuwa na umuhimu gani kujenga hoteli kubwa kule kijijini kwake ilhali wapiga kura wake hawawezi kwenda hata kununua soda au chai?



Mkuu, usimalizie hasira zako kwa jimbo hilo moja. nenda majimbo mengine, anzia kwa Pinda, kwa Membe, kwa Magufuli etc uone iwao kunaahuweni kwa wananchi, hususan vijana. halfu urudi humu ndani utueleze.
 
Mbowe sio mtz wa kawaida kama jk, mkapa au lipumba yeye amezaliwa kwenye uwezo sio siri labda hujui ukisema hana uwezo wa kujenga hotel?

kupata kiwanja tu cha billicanas ni bei gani?au wewe wa juzi Mbowe sio mtu wa njaa mimi sio msemaji wake ila kwa namna navyomjua.

Juzi nilikuwa naangalia wanawake live kipindi kinachorushwa ch 5 nikamuona mke wake na biashara alizo nazo hana shida billls,media nk acha hizo sie wengine tunakula kwa jasho letu bila kupewa kama wewe.

Ni lini ulimpa pesa za ujenzi wa shule akazila kazi zote ulizo sema mtekelezaji ni ser ya CCM kupitia kodi yako na yangu.
 
Kwa taarifa yako Hotel anayomiliki Mbowe ilijengwa na marehemu baba yake.Yeye anaiendeleza tu.
Mbowe si mbinafsi wa kujilundikia maendeleo na kuwaacha watanzania wengine.Ingekuwa ni hivyo
butiama kungekuwa kama Ulaya.
 
Imekaa kimajungu zaidi, nonsense. Nakubaliana na wale wanaosema JF siku hizi imeshuka thamani na mvuto
 
hivi machine tools kuna vijana wanafanya nini pale??mimi najua pale ni njia panda ya machame'hao vijana wana hali mabaya kivipi?wanaishi pale?tukipita pale tunaona vibanda na vioski wenye navyo hawaishi pale'kajipange upya jimbo la hai ni mfano wa kuigwa toka enzi za babu zetu
 
Nakushauri nenda tembelea na geita au kahama kwenye dhahabu na ziwa victoria samaki unavua tu ziwani bure na maaneo ooevu kwa kilimo halafu uje na hoja hapa kuzungumza hapo hai kwenye jangwa
 
i gess hamjanielewa na post yangu

Mkuu Mujumba umeongelea kuhusu Mh. Mbowe kuhubiri demokrasia..then hoja ukajenga katika haya;

1. Vijana kuwa na mausha magumu
2. Yeye kujenga/kuwa na hoteli.

Hapo ndipo usipoeleweka, kwani ni viongozi wengi wenye kumiliki Biashara kubwa na haimaanishi kuwa kiongozi(hata kama kiongozi mzuri namna gani) kuboresha maisha kwa wote(believe me kuna watanzania ni wabishi kufanya kazi..namaanisha hawataki kujishughulisha au ni wavivu).

Sasa hebu fafanua mkuu ulikuwa una maana ipi.
 
Mleta mada nenda kajipange vizuri kwa kuanza kufanya tathmini kwenye majimbo haya; Chalinze, Monduli, Urambo, Mtama, Mtera, nk.
 
Chama dhaifu, Mwenyekiti dhaifu, wanachama dhaifu na mawazo yao dhaifu. Pilenii sana sijui ulitaka ajenge genge kijijini?
 
Mleta uzi ameleta majungu,Mbowe hapa HAI wanamwita KAKA alikataa kuitwa muheshimiwa.kweli amebanwa na majukumu ya kitaifa lakini yupo karibu na wapiga kura wake na wanampenda
 
Inaonekana mtoa uzi hajawahi kutembelea vijjini na itakuwa mara yake yakwanza kutoka,njoo Liwale,Nachingwea,Nanjilinji,uone maisha bora kwa kila Mtaganyika.we sema unachuki bnafu na Mh. Mbowe
 
Politics aside:

1. Vijana wa machine tools uliwauliza lolote au na wewe ni kati ya wale walotutenga wanao-judge watu kutokana na mavazi au muonekano??? Ulikaa nao mpaka wanapofunga siku ujue wanarudi home na bei gani mfukoni apart from manunuzi????
- Wana Mashamba yao
- Pale wako kijasiriamali, wanapakia mizigo.
- Fly Catchers
- Mountain Climbers
- Toyo Riders
- Mama/Baba Ntilies.

2. Kuna aliekuibia kutokana au aliekukimbiza?? Mpaka useme wana tabu???

3. Kimashuku wale ni mountain Climbers na Fly Catchers.

4. Mbona usiseme miradi waliowekeza Boma??? (Ulikuwako au fanikiwa kuiona Boma enzi za CCM?).

5. Unajua Aishi Protea imewaajiri (ajira rasmi na zisizo rasmi, watanzania wangapi?).

6. Unajua Aishi inachangia kiasi gani kwa akiba ya Pesa za kigeni??
- kodi?
- mapato mengine yatokanayo na Utalii???
- we need Hotels kama hizo.

7. MOSHI MJINI. Unajua personally Ndesa kawasaidia wanajimbo na wageni wangapi??

8. Keys Hotel. (Rejea Namba 6 hapo juu) faida zinafanana.


Popote pale lazima kutakuweko wavivu, na maskini. Lakini pia usisahau Con-Artists. So hizo siku chache hazitoshi wewe kupata conclusion kama hii.

Hata mimi leo ukijileta nikaona unaleta tambo za ileri(pesa) ukiniuliza nakuambia maisha magumu ili unitoe ileri nikapige wari.


Nakushauri rudi tena kafanye utafiti wako halafu uje hapa na Jimbo lingine lililo chini ya CCM ama The Swahibaz CUF ufananishe.
 
Mkuu Mujumba,
kiwanda chako kinaitwaje vile?? kwa hiyo tathimini ni kama una kiwanda alichokisema Dhaifu wakati anazindua daraja kigamboni, ok Vipi mlima uliupanda?
 
Last edited by a moderator:
Kipimo kikuu cha kujua jimbo lina maendeleo ama la ni kwa kupima kiasi cha mwamko wa wananchi kuichukia CCM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom