Safari yangu Jijini Arusha na niliyoyakuta

Nachomaanishia hao mangi si ndo wameishika mji huo.
Kama haulizwi samahani labda hauna impact kwao yoyote ile kiuchumi.
Kuwa na duka kubwa la Mali Fulani hapo town utaona labda utauzia chasaka wenzako.
Huo mji una ukabila sema hauujui vizuri.
Ukienda soko kuu hata wale wanunuzi wa samaki wabichi wananunua kwa wao tu. Wale wakuja wananunua kwa wauzaji wakuja ambao sio wenyeji.
Ukiwa hata na hiace pale Moshi mjini wakishaijua hakuna mchaga wa kuipanda.
Nipige uniue Ila mchaga hawezi akakuletea kabisa dili la Mana asipelekee wa kwao. Inaonekana wewe bado hujawajua hao kiuchumi na huku watanzania wanawachoroga walivyojazana kwa miji ya wengine na wao wananunua kwao.
Yaani mie naweza nikaipeleka hela kwa mtanzania yeyote yule ila sio mangi mkuu.
Kila mtu anavuna analopanda.
Hata Mbowe vikao vyake vyote vya kisiasa kila mkoa anaofikia lazima aende kwenye hotel ya mtu wa Kilimakyasharo.
Ama hukumbuki viti maalumu walivyojazana dada zao mpaka mtwara Mara babati huko anatoka manka viti maalumu.
Atakuja kununua Mali ya hela ndogo Kama kukuzuga kuwa sio hatuna ukabila Ila Sasa kubabake awe Ana bars hata tano afu unauza via jumla eti kila siku awe ananunua kwako vinywaji Kama vya 2M kwako wewe kyasaka.
Yaani jua linachomoza from West to East geography nimeisahau.
Hao ni Kama wakenya mkikuyu hanunui kwa mkalenjini ama mwalimu mjaluo akafundishe kwa wameru kila mtu anabaki kwao
Hizi mada za ukabila sijajua mnaziendekeza ili iwe nini?

Binafsi sijashuhudia hilo labda kwa vile ulikuwa muda mfupi. Lakini kwa wingi ule wa watu na hizo mambo haiwezi kuwa rahisi.

Tuache ukabila. Mbona kwenye papuchi hamuulizi ukabila wa udini?
 
Hizi mada za ukabila sijajua mnaziendekeza ili iwe nini?

Binafsi sijashuhudia hilo labda kwa vile ulikuwa muda mfupi. Lakini kwa wingi ule wa watu na hizo mambo haiwezi kuwa rahisi.

Tuache ukabila. Mbona kwenye papuchi hamuulizi ukabila wa udini?
Iko ivi ukikaa mji wowte muda mrefu afu ukiwa kibiashara unawajua wafanyabiashara wote na mizigo wanayoiuza. Unalijua ilo lakini mnajuana Kama vile mmesoma wote olevo afu boarding mkuu.
Pia Kuna muda mnaweza mkakutana so mkikutana hapo hapo mipango inawekwa.
Mangi hawezi kuja yard akachukua Kama ist Kama 3 Ivi na kuendelea
 
Hii ndio bara la Arusha, nilimkuta huyu mrembo moyo ukadunda kudung kudung

Kwakweli alikuwa na umbo zuri sana, wallah vile
IMG_20210606_001028.jpg
 
Alikuja kiongozi mmoja wa CCM kutoka DSM wakati wa kampeni wakati anaongea kijana mmoja wa Arusha akamwambia

'''Aisee hatutaki LOMONI nyingi, we ng'oa zako''

Hakuelewa chochote na hata wenzake wakawa wanaukiza wamesemaje? Lomoni ni nini?

Kumbe Lomoni ni Maneno mengi

 
Alikuja kiongozi mmoja wa CCM kutoka DSM wakati wa kampeni wakati anaongea kijana mmoja wa Arusha akamwambia

'''Aisee hatutaki LOMONI nyingi, we ng'oa zako''

Hakuelewa chochote na hata wenzake wakawa wanaukiza wamesemaje? Lomoni ni nini?

Kumbe Lomoni ni Maneno mengi

Tena siku hizi wanaita lomoni lomoni
 
Karibuni chugga,hatunaga shobo na MTU,km msaada wa mchongo tunakusaidia ila tu kuna wasio wazur pia,njoo Olmatejoo,ungaltd,ngarenaro,majengo,morombo,kisongo,sakina hadi ngara,unaeza pia kuja mwanama,njiro,ukiweza unakuja hadi usa river.karibuni sana,weekend inayokuja j moc ntakuwepo club d,na jpili ntakua the don,atakaekuwepo mitaa hio anicheki nimpe bucket moja ya windhock
 
No. 3 Si kweli kabisa.
Asilimia kubwa ya waendesha magari wanatii sheria vizuri. Isipokuwa Asilimia kubwa ya waendesha bodaboda ndio ovyo na hii ni kawaida kwa mikoa yote.

Karibu tena chuga!
Arusha waendesha magari wababe sana hasa akiwa na gari nzuri kidogo na hakuna fair kwa sisi tulioendesha magari mikoa tofauti tunajua hilo na pia ukitoa fair kwa mtu aingie na gari kwanza anashangaa wengi wanawasubirisha gari ziishe ndio aingie bara bara kubwa wakati gari haziishi mjini..unakuta mtu ana pick up harafu anawaacha wanafunzi na muda mwingine mvua inanyesha mimi kabla sijauza ford walishazoea nikipita mida wanayotoka nikisimama wanapanda kwa adabu nawaacha mjini..
 
Arusha waendesha magari wababe sana hasa akiwa na gari nzuri kidogo na hakuna fair kwa sisi tulioendesha magari mikoa tofauti tunajua hilo na pia ukitoa fair kwa mtu aingie na gari kwanza anashangaa wengi wanawasubirisha gari ziishe ndio aingie bara bara kubwa wakati gari haziishi mjini..unakuta mtu ana pick up harafu anawaacha wanafunzi na muda mwingine mvua inanyesha mimi kabla sijauza ford walishazoea nikipita mida wanayotoka nikisimama wanapanda kwa adabu nawaacha mjini..
Nina uhakika ulipita Arusha ila hujaishi wala kuendesha barabara Za arusha. Yaani huku kwanza hakuna purukushani za magari mji mdogo sana huu. Kama unaona Arusha kuna ubabe barabarani basi wewe ni dereva mchanga sana. Karibu tena uendeshe hata angalau wiki moja
 
Nilikua Chekereni mitaa ya Neema house. Nilienda kumla manzi Sakina, kwa 40k bao 3. Nishatoka baada ya migodi ya Moramu, Kwaru, kufungwa. Nimekula sananyama Rokii siku za ijumaa. I'll be back there.
Watoto wazuri Arusha wanapatikana wapi
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Kazi iendelee.

Ilikuwa ni furaha kutoka Nyanda za Juu Kusini na kuja Ukanda huu wa Kaskazini mwa Tanzania.

Jiji maarufu kabisa kwa harakati za utalii.

Yafuatayo ndiyo niliyoyaona na mengine yamenishangaza.

1. Covid 19 imeutesa sana huu mji. Mishe zilizotegemea utalii zilikumbwa na pigo kama lile la afande moroto. Ingawa hali kama inarejea.

2. Ulaji nyama na unywaji wa pombe hufanyika kwa kiasi kikubwa mnoo. Si dhani kama kuna mkoa unawazidi hawa jamaa.

3. Utii wa sheria kwa watumiaji wa vyombo vya moto ni kama haiwahusu. Madereva wapo rafu mnoo. Watu pekee wanaojitahidi ni toyo/boda ingawa ni wapo wahuni wachache.

Uendeshaji magari ni tatizo katika hili jiji. Trafiki inabidi wafanye kazi ikiwa ni pamoja na kuchora upya namna ya matumizi ya barabara.

4. Watembea kwa miguu hawa ndiyo viburi waliopitiliza. Wanajiona nao ni kama magari/pikipiki.

5. Tabia za kibepari ni nyingi mno kuliko ujamaa. Wepesi pia kupeana michongo, wanaamini nao wanaweza tokea humo.

6. Bei za milupo nadhani bado bei elekezi inafanya kazi. Ila ukiwa mgeni unaweza pewa bill kubwa. Kuwa makini, wengine bado ni wezi hawaheshimu kazi zao.

7. Changamoto katika meno ya hawa watu ni shida. Demu mkali unakuta meno yameharibika, rangi zilizopitiliza. Sijajua chanzo hasa ni nini, je ni maji wanayotumia ama ulaji nyama uliopitiliza?

Iweje mamlaka ya maji safi wanashindwa kulitatua hili,wala madaktari wetu pia wameshindwa.
Hata kama linawapa identity bado ni mbaya pale inapodhidi,ingawa inaleta urembo kwa wengine.

8. Jamaa ni waoga sana wa baridi.

Asanteni Ara Chuga, masela wa Njiro, Moshono, Chekeleni, Ngaramtoni, Unga Limited, Sakina, Morombo, Ngarenaro, Makao Mapya hata wale nilio wasahau.

Vijiwe vyenu nilivyopita ni The Don, Mopao, Kokoriko, Uzunguni, Bills River, Picnic, Empire, Annex, Redwood.

Hakika zimekuwa siku 8 za purukushani nyingi na muda mchache wa kulala.

Fantastic stay in your city.

Karibuni pia kwa wanalizombe.
Picnic ulifata malaya
 
Back
Top Bottom