Safari ya Sudani Kusini

Inaonekana wazi wazi kuwa hii ni safari yako ya mwanzo kutoka nchini Tanzania.Afadhali umekuwa mkweli katika uandishi na kuonesha sura yako halisi. Pale ulipoambiwa watanzania kuingia kule hakuna shida ulitafsiri hakuna visa wala masuala yoyote.Hivyo ulipodaiwa dola 50 ukaanza ubishi.Una bahati sana wale watu walikupenda na kukuwachia uingie bure.

Ujuwe kila nchi mpakani ina masuala ya uhamiaja na aina ya visa ya kituo unachoingia bila kupata mwaliko ni aina moja ya viza rahisi lakini sio bure.

Umeanza kutoka nje ya nchi kwa kutumia mabasi uliyoyazoea kule Tabora.Ungesafiri kwa kutumia ndege za kimataifa na ikawa safari yako ni ya kubadilisha ndege kwenye miwanja mikubwa ya kimataifa na sio kama ule wa Dar es salaam au ule wa Juba basi nadhani ungeaachwa uwanjani na ndege ukajitafutia balaa jengine. Ungekuwa unashangaa shangaa na usipate hata wa kumuuliza kwani kule huwa wanatumia mifumo ya kielektronic tu hata spika hawazitumii tena isipokuwa kwa dharura kubwa itakapokuwa kuna mtu kapotea hajaingia kwenye ndege.

Halafu tangu mwanzo umeshaambiwa ile nchi haina usalama, wewe umeshikilia kupiga piga picha na kutembea na kamera kwapani.Hiyo kamera kuporwa ni adhabu ndogo.Ungepigwa kabisa sijui ungmlaumu nani.

Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu urudi tena huko na siku moja ufike angalau London.Ukiniona utanishtua nitakuwa pamoja nawe lakini mambo ya kuingia mabaa kupata kinywaji itakuwa ndio mwisho wa urafiki wetu.
Ulikua hauna haja ya kukosa.
 
View attachment 1601322
Uwanja fulani wa ndege niliowahi kutua. Hapo dereva wako wa teksi lazima awe ni mzoefu.Akiwa mshamba akafuata hiyo ya kulia au ya katikati ndiyo keshakupotezea safari kwa sababu zote zinafika uwanjani lakini hakuna njia ya kupinda kurudi wala kukatisha kuelekea kule Arrivals na departure na masafa yake huko ndani kwa ndani ni kilomita kadhaa.Kuna vitreni vidogo vya glasi lakini hata ukifika lango ulilokusudia muda umekwenda sana.Utakuwa umesubiriwa sana na ndege imepitisha muda wa kusubiri abiria aliyepotea na kuondoka zake.
Nakupa picha tu siku utakayotua kwenye mchi yenye viwanja kama hivyo
Badala ya kutulingishia vya wazungu, Basi ungetupa na ww story ya huko kwa uzi wako.
 
Mkuu ulichosahau Kampala askari wa barabarani wanaongozea magari kwa filimbi nilitumia hiyo ruti ya mwanza Kampala friends ndo mfalume wa hiyo njia ukiingia Uganda mfalume ni bus za link zina rangi ya kijani zinaenda mikoa yote ya Uganda.
 
Umeishia Juba unasema kuna Amani kuliko ulivokua unasimulia ungetembelea Jonglei,Bentiu,Bor Unity,Heglig,state South Kordofan( iko mpakani na Sudan) bahr el Ghazal huko ungekuja na stori ingine
Hayo ni majina ya miji au species 🤔🤔🤔
 
Mkuu mi nataka niingie kampala. Natakiwa niwe na vitu gani wakikagua pale mpakani?
 
Inaonekana wazi wazi kuwa hii ni safari yako ya mwanzo kutoka nchini Tanzania.Afadhali umekuwa mkweli katika uandishi na kuonesha sura yako halisi. Pale ulipoambiwa watanzania kuingia kule hakuna shida ulitafsiri hakuna visa wala masuala yoyote.Hivyo ulipodaiwa dola 50 ukaanza ubishi.Una bahati sana wale watu walikupenda na kukuwachia uingie bure.

Ujuwe kila nchi mpakani ina masuala ya uhamiaja na aina ya visa ya kituo unachoingia bila kupata mwaliko ni aina moja ya viza rahisi lakini sio bure.

Umeanza kutoka nje ya nchi kwa kutumia mabasi uliyoyazoea kule Tabora.Ungesafiri kwa kutumia ndege za kimataifa na ikawa safari yako ni ya kubadilisha ndege kwenye miwanja mikubwa ya kimataifa na sio kama ule wa Dar es salaam au ule wa Juba basi nadhani ungeaachwa uwanjani na ndege ukajitafutia balaa jengine. Ungekuwa unashangaa shangaa na usipate hata wa kumuuliza kwani kule huwa wanatumia mifumo ya kielektronic tu hata spika hawazitumii tena isipokuwa kwa dharura kubwa itakapokuwa kuna mtu kapotea hajaingia kwenye ndege.

Halafu tangu mwanzo umeshaambiwa ile nchi haina usalama, wewe umeshikilia kupiga piga picha na kutembea na kamera kwapani.Hiyo kamera kuporwa ni adhabu ndogo.Ungepigwa kabisa sijui ungmlaumu nani.

Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu urudi tena huko na siku moja ufike angalau London.Ukiniona utanishtua nitakuwa pamoja nawe lakini mambo ya kuingia mabaa kupata kinywaji itakuwa ndio mwisho wa urafiki wetu.
Duh!
 
Sijaona ukizungumzia kile kilichokupeleka huko.

1. Uligundua nini kuhusiana na uhusiano wa wasudani na wamasai?

2. Lengo la kufundisha kiswahili liliishia wapi?

Nimeona tu umetoa maelezo mengi ambayo hayakuwa msingi hasa ya ulichoanz simulia. Historia ya wamasai na kufundisha kiswahili. Zaidi zaidi umekazia tu kuwa umeona watu weusi,warefu,wenye sura za kutisha. Sudani hawana wanachotisha. Nenda Somalia ndo uje usimulie. Ngoja nikupe uzoefu wangu wa Somalia uone.
 
Back
Top Bottom