Safari ya Serikali Dodoma izingatie haya...

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,104
7,857
Nadhani mbio za kuhamia Dodoma ni nafasi nzuri na pekee ya kurekebisha kasoro mbalimbali zilizokuwepo muda mrefu katika kuhudumia wananchi. Ni ushauri wangu kwamba mchakato huo uzingatie haya mambo yafuatayo:
  • Kila idara na wizara ya serikali iwe na mfumo mzuri, wa uhakika na wenye kumjali mwananchi wa huduma kwa wateja na hii inajumuisha kuwa na mawasiliano ya uhakika ya simu. Ikiwezekana kila idara iwe na toll free number kama ambavyo makampuni ya simu yanafanya. Huduma hiyo ya simu iwe na watu wenye uelewa wa mambo yote yanayohusiana na idara hiyo na nashauri iwe wazi kwa masaa 10-12 kila siku, kwa siku 6 kila wiki. Mawasiliano yote ya simu yarekodiwe ili kupima ufanisi wa wafanyakazi na ili kujua mapungufu yalipo.
  • Shirika la Posta lihakikishe kila idara ya serikali, makampuni binafsi yanayoenda kufungua ofisi Dodoma na hata makazi ya watu yanapewa anwani ya posta mara moja na barua zipelekwe moja kwa moja kwa wahusika katika maeneo yao kila siku (siyo katika mabox).
  • Usafiri wa umma uboreshwe. Utafiti ufanywe kujua mahitaji ya mji kwa miaka 5-10 ijayo na hiyo huduma na miundombinu iendane na makadirio hayo sasa hivi badala ka kusubiri mpaka mji umeelemewa! Hiyo itapunguza watu kushawishika kutumia usafiri wao binafsi ambao utaleta misongamano kama ya Dar es Salaam.
  • Ujenzi wa majengo uzingatie mipango ya mji lakini pia uzingatie kwamba Dodoma inapata matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.
  • Tovuti zote za idara na wizara za serikali ziwe updated kila siku. Kila fomu na taarifa zote muhimu zipatikane kwenye tovuti hizo. Kwa kuwa watu sasa waan vitambulisho vya kitaifa, vitambulisho vya kupiga kura, passport, nk. umuhimu wa watu kuja maofisini upungue kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuhakiki taarifa za watu.
Mwananchi
 
Back
Top Bottom