Safari ya Rais Samia Dubai: Viwanda vinne kujengwa nchini, kuzalisha ajira zaidi ya 3500

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Historia ya uchapakazi na kujituma ni kati ya mambo mengi yanayotoa tafsiri ya uongozi wa Rais Samia Suluhu. Baada ya ziara yenye mafanikio makubwa Barani Ulaya na katika Falme za Kiarabu, Haya ni baadhi ya makubaliano ya ujenzi wa viwanda nchini kufuatia juhudi za Rais Samia kuvutia wawekezaji nchini;

1. Makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kiwanda cha Fujian Hexingwang Steel Factory.

Makubaliano haya yamesainiwa na kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park Ltd na Fujian Hexingwang Industry Tanzania Ltd. Mradi huu una thamani ya USD Milioni 100 na unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa 2000.

2. Makubaliano ya utekelezaji wa mradi wa kiwanda cha Zion Aluminium Profiles Manufacturing.

Makubaliano haya yamesainiwa kati ya kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park Ltd na Wenzhou Zion Decoration Engineering Co. Ltd. Mradi huu una thamani ya USD Milioni 10 ukilenga kutengeneza ajira za moja kwa moja 500.

3. Makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vifaa vya ujenzi.

Makubaliano haya yamesainiwa kati ya kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park na Group Six International Ltd. Mradi huu una thamani ya USD Milioni 5 na unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 100.

4. Makubaliano ya ujenzi wa kiwanda cha nguo cha Yelete Clothing.

Makubaliano haya yamesainiwa kati ya kampuni ya Yelete Group na Sino Tan Kibaha Industrial Park. Mradi huu wenye uwezo wa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1000 una thamani ya USD Milioni 20.

Pasipo na shaka yoyote ile adhma ya kuhakikisha ajira zinatengenezwa kwa wingi kupitia sekta binafsi inatekelezwa kwa vitendo. Kongole Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada hizi zenye tija kwa wananchi wako.

Sisi Tumekubali
Kazi inafanyika

IMG-20220303-WA0004.jpg
 
Ni Vema na Haki, So long as hawatapewa Favor na some Tax Heavens to the detriment ya viwanda vilivyopo (namanisha iwe fair ground)

Sio kiwanda cha nguo hicho kipewe afueni wakati tumeshindwa au tuzidi kuua viwanda vya nguo vilivyopo (in short tuangalie kuvifufua na hivyo)

Tutafute wawekezaji ila hizi minor jobs / viwanda vidogo vidogo ambavyo hata kina Pwagu na Pwaguzi wanafanya tungewawezesha wadau wafanye hizo kazi, Nadhani tunakoelekea hili Taifa linakwenda kuwa Taifa la Madalali na Middle Men.
 
Historia ya uchapakazi na kujituma ni kati ya mambo mengi yanayotoa tafsiri ya uongozi wa Rais Samia Suluhu. Baada ya ziara yenye mafanikio makubwa Barani Ulaya na katika Falme za Kiarabu, Haya ni baadhi ya makubaliano ya ujenzi wa viwanda nchini kufuatia juhudi za Rais Samia
Uwekezaji wa dola milioni 5, milioni 10, milioni 20!!! Mbona ni hela kidogo sana? Mradi wa dola milioni 10, hakuna kabisa uwezekano wa kutoa ajira ya watu 500, ni uwongo mkubwa.
 
awamu ya tano ilizalisha ajira milions 8 na viwanda 8000 kwa mika 4 na huyu mama alikuwa makamu wa Rais nyie mnatuletea hivi vihoja
 
Back
Top Bottom