Safari ya Rais Magufuli kwa barabara yawatumbua mameneja wa TANROADS Lindi na Pwani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,779
141,664
Waziri wa ujenzi mh Kamwele amewaondoa madarakani mameneja wa Tanroads wa mikoa ya Lindi na Pwani kufuatia kushindwa kuifanyia matengenezo barabara ya Dar hadi Mtwara.

Maamuzi hayo ya mh Kamwelwe yanafuatia maagizo yaliyotolewa jana na Rais Magufuli ya kutaka hatua zichukuliwe kutikana na ubovu wa barabara alioushuhudia kwenye takribani zaidi ya km 90 .

Source Channel ten

Maendeleo hayana vyama!

=====

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Issac Kamwelwe ametengua uteuzi wa meneja wawili wa Wakala wa Barabara (TANROADS) wa Mikoa ya Lindi na Pwani kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi ya kusimamia miundo mbinu ya barabara kwenye maeneo yao.

Uamuzi huo wa Waziri Kamwelwe umefanyika ikiwa ni siku moja tangu Rais John Magufuli alipopita kwenye barabra za mikoa hiyo akitoka mkoani Mtwara kuhudhuria maziko ya Rais mtaaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na kukerwa na uharibifu mkubwa wa barabara za mikoa hiyo.

Kamwelwe alichukua uamuzi huo jana alipokuwa akikagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami yenye kilometa 1.6 inayotoka Kibaoni kwenda Makao Makuu ya Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoani Katavi.

Alikuwa njiani kutoka Mji Mdogo wa Inyonga uliopo wilayani Mlele kwenda mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Waziri Kamwelwe, mameneja aliotengua uteuzi wao ni Issac Mwanawima, Meneja wa Lindi na Yudas Msangi aliyekuwa Kaimu Meneja wa Tanroads wa mkoa wa Pwani.

Waziri Kamwelwe alisema Rais Maguguli alipita juzi kwenye barabara hizo na kushuhudia lami ikiwa imeharibika na barabara imekuwa kama ya vumbi wakati zipo fedha za matengenezo kupitia Mfuko wa Barabara zipo.

Alisema Tanroads walikuwa na sifa nzuri lakini wameanza kuharibiwa na watumishi wachache. “Kwa hiyo watambue kuwa kipindi hiki siyo cha kufanya mchezo kila anayebainika kushindwa kutekeleza majukumu yake atambue kuwa atawajibishwa,” alisema.

Aliwataka mameneja wa Tanroads kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu barabara zote zilizoharibiwa na mvua za msimu huu zinakarabatiwa na zinakamilika.

Akifafanua, Kamwelwe alisema wizara yake imetoa zaidi ya Sh bilioni 35 kwa matengenezo ya barabara hizo na kwamba meneja atakayeshindwa kukamilisha, ajihesabu kuwa umeneja wake utaishia tarehe hiyo.

Alisema kabla ya kutoa agizo, aliwaita mameneja wa Tanroads wa mikoa yote kwenye kikao kilichofanyika jijini Dodoma na kuwaelekeza wahakikishe wanafanya matengenezo ya barabara zote zilizoharibika kwa mvua za masika.
 
Fedha zipo? Pole zao mameneja.

Btw, hivi mawaziri nyazifa zao zinakoma lini? Au mpaka baraza jipya liundwe?
Ingeliwezekana kabisa kwa kipindi hiki kazi zikafanywa na makatibu wakuu. Kwa kuendelea kuwa mawaziri hakuwezi kuleta usawa katika uchaguzi hata kidogo.
Wasimamizi wenyewe ndio hawa wanaotakiwa kutangaza matokeo ya ushindi tu na sio kushindwa.
Mawaziri = Rais
 
Katiba hii ni ya kiboya sana. Huwezi kuelewa ni kitu gani waliokuwa wanatunga hii katiba walifikiria nini? Yaani iko hovyo haifai kutumika hata kwenye familia tu
Hakuna kitu cha ajabu nchini kama Katiba, inasema ili uwe Waziri lazima uwe Mbunge. Bunge lilivunjwa Juni, 28 kwa maana hiyo hakuna Mbunge aliyeadarakani. Sasa hawa mawaziri ni Wabunge kwa mujibu wa katiba ipi!?
 
Hizi nafasi zilipashwa sasa ziwe zinatangazwa watu wanaomba, wanafanyishwa usaili na kupewa kazi ili mwisho wa siku tuwape target na tuanzie kuwahukumu hapo...tujitahidi sana kupunguza nafasi za uteuzi ili tuweze kuwa na uwanja mpana wa kuajiri watu makini na wenye akili waliojaa huku mtaani...
 
Back
Top Bottom