Safari ya Pinda, ratiba ya zua hofu bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya Pinda, ratiba ya zua hofu bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dik, Nov 18, 2011.

 1. D

  Dik JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  SAFARI ya ghafla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mabadiliko ya ghafla ya ratiba ya vikao vya Bunge, jana vilizua hofu miongoni mwa wabunge, huku kukiwa na taarifa kwamba huenda muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ukaondolewa bungeni leo.

  Jana alfajiri Pinda aliondoka kwa ndege kwenda jijini Dar es Salaam, ikielezwa kwamba safari yake ilikuwa ni kuitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete. Baadhi ya wasadizi wa Pinda walioko mjini Dodoma walithibitisha Pinda kuitwa na Rais, lakini hakuna aliyekuwa akifahamu kuhusu kiini cha wito huo.

  "Amekwenda Dar es Salaam na atarudi jioni leo (jana), kaitwa na bosi wake, lakini ndio hatujui ila ni safari ya kawaida,"alisema mmoja wa wasaidizi wa Pinda ambaye hakuwa tayari kutajwa gazetini.

  Safari ya Pinda ilisababisha kutokuweapo kwa kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu bungeni jana na badala yake kuwapo kwa kipindi cha maswali ya kawaida ambacho kilifuatiwa na mjadala wa muswada huo.

  Baadhi ya wabunge wa CCM walisikika wakihoji sababu ya Pinda kuitwa ghafla na katika mazungumzo ambayo Mwananchi liliyasikia, walikuwa wakihofu kwamba huenda Rais akataka muswada huo urejeshwe kwa umma kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

  Mmoja wa wabunge hao alimhoji mwandishi wa gazeti hili akisema: "Eti nyie waandishi huwa mnafahamu mambo mengi, hivi ni kweli kwamba Pinda kaitwa na Rais ili kuondoa muswada…..! Kama ni hivyo basi itakuwa imekula kwetu".

  Hofu hiyo ilisikika kwa zaidi ya wabunge sita wa CCM ambao walizungumza na Mwananchi huku wengine wakihusisha suala hilo na hatua ya kubadilishwa kwa ratiba ya Bunge.

  Mbunge mwingine alisema: "Hili jambo linawezekana ni la kweli, kwanza ratiba imebadilishwa ghafla bila kuitishwa kwa Kamati ya Uongozi, halafu PM (Waziri Mkuu) hayupo, lakini hebu tusubiri tuone kitakachotokea kwani kesho siyo mbali".

  Kikwete aendesha kikao Ikulu

  Hata hivyo, taarifa ambazo Mwananchi imezipata kutoka Ikulu jijini Dar es Salaam zinasema kwamba Rais Kikwete jana alikuwa na kikao nyeti na Pinda, Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

  "Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wana kikao cha ghafla Ikulu, nahisi wanazungumzia muswada ulioko bungeni," kilisema chanzo cha habari.

  Chanzo hicho kilisema kwamba huenda Rais Kikwete akaliongelea suala hilo leo.


  Mabadiliko ya ratiba
  Juzi jioni mmoja wa wenyeviti wa Bunge, Sylivester Mabumba alipokuwa akiahirisha kikao cha Bunge, alitangaza mabadiliko ya ratiba ya vikao vya Bunge yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, mabadiliko yaliyoongeza siku moja zaidi katika mkutano huu wa tano.

  Badala ya kumalizika leo, tangazo hilo lilisema kuwa mkutano huo utamalizika kesho Jumamosi, huku mjadala wa Muswada wa Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2011 ukiongezewa muda zaidi.

  Katika ratiba ya awali, muswada wa marekebisho ya katiba ulipaswa kuhimitishwa juzi jioni, lakini katika ratiba iliyotangazwa na Mabumba unatarajiwa kuhitimishwa leo katika kikao cha asubuhi, baada ya wabunge kumaliza kuchangia jana mchana.

  Ripoti ya Jairo kusomwa leo

  Mabadiliko hayo yanaonyesha kuwa, ripoti ya Jairo ya Kamati Teule ya Bunge itasomwa leo baada ya kuhitimishwa kwa muswada huo, na kesho Bunge litapokea ripoti ya kamati ya Nishati na Madini kuhusu sekta ya gesi kisha Bunge kuahirishwa.

  Jana hakukuwa na kikao cha jioni baada ya Bunge kukutana asubuhi, hali ambayo iliwafanya wengine kuhoji sababu za muswada huo kuwekwa kiporo hali kulikuwa na muda wa kuhitimisha jana.

  "Kama wachangiaji hawapo kwanini wanaendelea kutuweka hapa sasa, maana leo (jana) jioni hakuna Bunge, wachangiaji wameisha tunasubiri nini?," alisikika mmoja wa wabunge wa Viti Maalum (CCM), akiwauliza wenzake katika viwanja vya Bunge jana.

  Lukuvi na Kashililah
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema: "Lazima mfahamu jambo moja, sisi Serikali hatuna mamlaka na ratiba ya vikao hivi, kazi hiyo ni ya ofisi ya Bunge. Lakini tumefurahi kwamba leo (jana) jioni hakuna Bunge kwasababu tunapata fursa ya kujibu hoja na kuzingatia majedwali ya mabadiliko yaliyoletwa na wabunge".

  Lukuvi alisema hadi jana jioni hakukuwa na mabadiliko yoyote kwenye ratiba iliyotolewa na Bunge juzi na kwamba Serikali ilikuwa ikijadiliana na wabunge waliowasilishwa majedwali ya mabadiliko katika muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ili kuona jinsi ya kuyazingatia katika sheria hiyo.

  "Sisi tunadhani kwamba ofisi ya Spika imefanya vizuri, maana kama tusingepata muda wa leo ingekuwa ni vigumu sana kujibu hoja zote za watu zaidi ya 70 katika muda wa saa 2 au tatu za mapumziko ya mchana, lakini sasa tuna imani kwamba kila kitu kitakwenda sawa maana tutapata muda wa kujadiliana na wabunge na mambo yote kesho (leo) yatakwenda sawa,"alisema Lukuvi.

  Kwa upande wake, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema mabadiliko ya ratiba ya Bunge yalizingatia wingi wa majedwali ya marekebisho ya muswada huo yaliyowasilishwa na wabunge.

  Awali kulikuwa na taarifa kwamba majedwali hayo (schedules of amendments) yalikuwa yamefikia 29, lakini Dk Kashilila aliliambia Mwananchi kwamba majedwali hayo yalikuwa yakikaribia 40.

  "Lazima tufanye kazi hii nje ya Bunge, tunataka Serikali ikutane na hawa wabunge ili kufanya majadiliano ya awali kupunguza kazi hii maana ni vigumu sana kushughulikia majedwali haya bungeni, inaweza kutuchukua siku nzima,"alisema Katibu huyo wa Bunge.

  Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ilitarajiwa kukutana jana saa saba mchana, lakini kikao hicho kiliahirishwa hadi saa 10 jioni kutokana na Serikali kuwa na mzigo mkubwa wa hoja za wajumbe.

  Kuwepo kwa idadi kubwa ya majedwali yanayopendekeza marekebisho ya muswada huo, ni dalili kwamba hata wabunge wengi wa CCM wamebaini kasoro nyingi licha ya kwamba wote waliochangia waliuunga mkono.


  CHANZO: Mwananchi
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  apande ndege sijui aende sumbawanga sijui mpanda sijui wapi katiba mpya ipo pale pale
   
 3. I

  Ismaily JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunataka KATIBA mpya iliyobora na inayodhamini haki na utu wa mwanadamu,tutapigania haki yetu kwa gharama yoyote tupo tayari kumwaga damu kutafuta haki yetu ya watoto wetu,vizazi vyetu vitakavyokuja huko mbeleni.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kazi ipo mwaka huu
   
 5. Shut Down

  Shut Down Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hiyo kweli ime-eat kwenu!!
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Patachimbika! Twataka katiba mpya bora!
   
 7. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heri MIMI Mbunge wangu hakuchangia hoja kwenye huu muswada legelege, Hongera sana kamanda wangu kura yangu haikupotea bure. Tutahakikisha 2015 unarudi Bungeni kumbe unatufaa.
   
 8. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kama wana akili, wafanye tu kuwa huo muswada umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni ili wananchi wapate naafasi ya kuujadili. Pia mabadiliko yaliyopendekezwa yazingatiwe kwa maslahi ya taifa na sio kuendekeza uchama.
   
 9. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ccm wanafikiri nguvu na ubabe walokuwa nan mwanzo watu tungeendelea kuuvumilia? La hasha hauvumiliki hata kidogo sasa watz tumeelimika na tutahakikisha anguko kuu kwao
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  hawajui wafanyalo! Mtu anasafiri nyie mnapata hofu!! Hawajielewi hawa!
   
 11. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor"- Rev. Desmond Tutu

  so imekula kwako wewe uliyemchagua mtu huyo
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,832
  Likes Received: 10,143
  Trophy Points: 280
  Vilaaaaaza tupu na wana taarabu ndio waliobaki kujadili wasichokijua wala kukiamini
   
 13. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tumewaweza eeeeeeeeeee sijui watatumia njia gani kugeuza maneno
   
 14. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  YAngu miguu kuelekea dsm ili mapambano yaanze
   
 15. only83

  only83 JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Danganya toto hiyo..hao wabunge wamefanya mabadiliko wapi?
   
 16. m

  mkweli1961 Senior Member

  #16
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Jamani huu ndio wakati muafaka kuandamana. Baada ya wenzetu Zanzibar kusema wataandamana imebidi kiitishwe kikao ikulu na kunatetesi kwamba mkuu wa kaya atakutana na wazee wa Dar es Salaam leo. Hakuna polisi anayeweza kuzuia maandama hayo, mimi naona 2015 mbali nchi itakuwa imeliwa na kwisha. Ikibidi maandamano yafanyike tarehe. 09.12.2011 hiyo ni siku nzuri.
   
 17. m

  mkweli1961 Senior Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Pamoja tutashinda, Vijana wa Chuo Kikuu wamefanya kweli.
   
 18. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #18
  Nov 18, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Madodoki yameanza kuogopa vivuli vyao! Ha ha haa haaaa!! Peoples................................... Power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. C

  Campana JF-Expert Member

  #19
  Nov 18, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Majedwali Majedwali Majedwali - Hayana kazi hayo na ni batili. alazima kazi hii ianze upya
   
 20. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  jana sikuona TBC hewani kutupatia session za bunge waht happened wakuu??
   
Loading...