Safari ya Mwisho ya Prof. Waangari Mathaai-Tz Tumewakilishwa Vema!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Wanabodi,

Leo ndio safari ya mwisho ya mwanamazingira maarufu, Prof. Waangari Maathai, ambayo inafanywa kwa 'creamation'.

Tanzania imewakilishwa na Prof. Anna Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete.

Heshima hizo za mwisho, zinafanyikia katika viwanja vya Freedom Corner, jiji Nairobi, na zinaonyeshwa live kupitia, televisheni za KBC, KTN na Citizen, zimemonyesha Prof. Tibaijuka akitoa salamu za Rambirambi kwa lugha ya Kiingereza safi, (Queen English) ila alitangulia kwa salamu ya Kiswahili na kumalizia kwa pole ya Kiswahili.

Anayezungumza sasa ni Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, na atafuatiwa na Makomo wa Rais, Kilonzo Musyoka na ndipo Rais, Mwai Kibaki atazungumza, zitafuatie heshima za mwisho na safari ya kuelekea Kariakoo creamarium itaanza.

Endelea nami...

Pasco.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Raila Kamaliza kuzungumza, sasa anazungumza Makomo wa Rais wa Kenya Kilonzo Musyoka.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Makamo rais, Musyoka amemaliza kuzungumza, sasa anayezungumza ni rais Mwai Kibaki.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Miongoni mwa wasifu wa Prof. Wangari Maathai ni ndiye Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel. Ndie Mwanamke wa kwanza eneo la Afrika ya Mashariki kupata Udakitari wa Falsafa , Ph. D.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Rais Kibaki amemaliza kuongea, Prof. Mbaya ameitwana apeane vote of thanks.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Watu wote wamesimama, Ule wimbo wa bigula wa heshima za mwisho unapigwa.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Watoto wake wameitwa mbele na kusimama mbele, sala ya mwisho ya Kanisa Katoliki imesaliwa. Padri amemalizia kwa kibagizo na kuwekwa kwa mwili wake kwenye makao ya milele, utakaposhushwa kaburini, na kufukiwa na udongo, kuwa yeye ni udongo, na tarudi tena kuwa udongo!.

Sala ya Katoliki, haitaki kabisa kutambua kuwa kuna mazishi ya creamation, wao mazishi ni kabuni tuu.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,425
92,698
Baada ya sala, umefuatia wimbo wa taifa, na safari ya kuelekea creamatorium imeanza.

Naombeni nami niwaage kwa sasa, kwa sababu sitaki kuagalia hilo zoezi la creamation.

Asanteni na kwaherini.
 

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,601
1,225
Miongoni mwa wasifu wa Prof. Wangari Maathai ni ndiye Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel. Ndie Mwanamke wa kwanza eneo la Afrika ya Mashariki kupata Udakitari wa Falsafa , Ph. D.
Mzee Pasco, licha ya kutoa pongezi zangu za dhati kwa kutuhabarisha, ningependa kuchukua fursa hii kurekebisha mambo flani. Prof Wangari Maathai sio Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel. Listi nzima ni kama ifuatayo:

Peace:
1905 Baroness Bertha von Suttner
1931 Jane Addams
1946 Emily Greene Balch
1976 Betty Williams
1976 Mairead Corrigan
1979 Mother Teresa
1982 Alva Myrdal
1991 Aung San Suu Kyi
1992 Rigoberta Menchu Tum
1997 Jody Williams
2003 Shirin Ebadi
2004 Wangari Maathai
2011 Ellen Johnson Sirleaf, Leyman Gbowee, Tawakkul Karman
 

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,802
9,918
Baada ya sala, umefuatia wimbo wa taifa, na safari ya kuelekea creamatorium imeanza.

Naombeni nami niwaage kwa sasa, kwa sababu sitaki kuagalia hilo zoezi la creamation.

Asanteni na kwaherini.
Wataonesha live?
 

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,802
9,918
Miongoni mwa wasifu wa Prof. Wangari Maathai ni ndiye Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel. Ndie Mwanamke wa kwanza eneo la Afrika ya Mashariki kupata Udakitari wa Falsafa , Ph. D.
Mwanamke mwafrika wa kwanza
 

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
987
Miongoni mwa wasifu wa Prof. Wangari Maathai ni ndiye Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel. Ndie Mwanamke wa kwanza eneo la Afrika ya Mashariki kupata Udakitari wa Falsafa , Ph. D.

Asante kwa taarifa. Naomba nami nirekebishe kidogo. Prof. Maathai siye mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kupata PhD. Siwezi kuwaorodhesha lakini kuna wanawake wengi waliokuwa tayari na PhD kabla ya Prof. Maathai. Sina hakika lakini nafikiri hata Prof. Tibaijuka alipata PhD yake kabla ya Maathai. Inawezekana labda unamaanisha kuwa ni wa kwanza kupata PhD kwenye hiyo fani yake ya masuala ya Mazingira. Miaka niliyokuwa Mlimani mwishoni mwa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini tayari tulikuwa na wakina mama waliokuwa na PhD wakifundisha pale. Mmojawapo ni Dr. Ruth Meena (PhD) wa Political Science ambaye sasa hivi ni Prof. Sidhani kama Prof. Maathai alishakuwa na PhD wakati huo.
 

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,601
1,225
askari kanzu, pasco amesema ni mwanamke wa kwanza afrika mashariki.
Never give up, hata sio kweli. Ukisoma vizuri utaona yeye ameandika "Mwanamke wa Kwanza kupokea tuzo ya Nobel" halafu "Mwanamke wa kwanza eneo la Afrika ya Mashariki kupata Udakitari wa Falsafa , Ph. D." Hivyo ni vitu viwili tofauti, ndo maana baada ya kumpongeza nimemwomba fursa ya kumkosoa!
 

Kiminyio

Member
Sep 25, 2011
38
4
Kwakweli amejitahidi, Dr. Samiji, University of dar es Salaam ndiye mwanamke wa kwanza kupata PhD ya cryistal physics.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom