Albert Mangwea (Special Thread)

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
Safari ya Mwisho ya Albert Mangwea (RIP) katika picha


Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Addo Novemba kushoto akijadiliana jambo na viongozi wa Kamati ya Mazishi katika shughuli yaa kumuaga marehemu Albert Mangwea, katika viwanja vya Leaders Club leo.




Wasanii wanaaga




Mbunge Idd Azzan anamuaga Ngwea



Watu wanamlilia Ngweaa
Sehemu ya waombolezaji waliokwenda wakimuaga marehemu Ngwea katika viwanja vya Leaders Club




Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan kulia, akijadiliana jambo na mjukuu wa Julius Kambarage Nyerere, Sofia Nyerere na ndugu yake kushoto kwake katika viwanja vya Leaders Club leo.
Waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea wakijadiliana jambo katika viwanja vya Leaders Club

............Historia ya Albert Mangwea kimziki..............
Albert mangwea (R.I.P ) ni moja kati ya wanamuziki wa kizazi kipya ambao nitawakumbuka daima katika siku za uhai wangu,sio kwamba namjua vizuri hapa ila kwa kiasi fulani ni moja ya wanamuziki ambao naweza kukaa na kumuelezea mbele ya watu hasa wasiomjua.

Huyu mwanamuziki namkumbuka sana mara ya kwanza kumuona ilikuwa 1999 ambapo kaka yangu alikuja nyumbani na album yao ya kwanza ambayo walirecord kwenye studio moja mkoani Morogoro chini ya udhamini wa mwalimu mmoja wa kikorea bila kukosea aliyekuwa anafundisha pale mazengo enzi zile masomo ya ufundi. Kipindi hicho ngwea alikuwa anaunda kundi lililokuwa likijulikana kama CFG(Chamber fleva guys) ambapo hilo kundi lilikuwa likiundwa na ngwea,mez-b ambapo kipindi kile alikuwa akijiita QG na jamaa mmoja alikuwa anaitwa maloga ambaye ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambaye yeye alikuwa akijiita malo-star.

Hapa ifahamike kuwa chamber squard imekuja baadaye baada ya maloga amajina jigine nzeku kuendelea na masomo,hapa noorah alikuwa kidato kimoja chini ya kina ngwea na dark master yeye aliwatangulia kumaliza alimaliza shule sema ndio vile kishule shule baadaye wakakutana dar na kuunda chamber squard.(nimjuavyo noorah ntaelezea siku nyingine).

Enzi hizo mez-b ambaye alikuwa anajiita QG alikuwa bishoo sana mwenyewe chini alikuwa anavaa viatu fulani kama timberland lakini vilikuwa vya manyoya kama ya mbwa hivi.hawa CFG katika hiyo album yao ya kwanza ambayo ndio ilikuwa kama mwanzo wa safari yao ya muziki iliitwa HESHIMA KWA WOTE ambao kulikuwana nyimbo kama heshima kwa wote kiburi maisha,enzi hizo mezb anarap.

Walifanikiwa kuzindua album yao katika ukumbi wa NK dodoma enzi hizo nakumbuka na miminikiwa mmoja wa watu nilioshuhudia show. Hapa ileleweke kuwa ngwea sio muasisi wa EAST ZOO sema ni mwanamuziki aliyeitangaza vilivyo kutokana na mapenzi yake kwa wana east. East zoo ilianzishwa na jamaa mmoja alikuwa anaitwa amani masinga sasa ni mkaguzi pale duwasa dodoma ambapo alianzisha EAST ZOO kutokana na bifu lake na G-SOLO ambaye yeye ndio alikuwa mwanamuziki mkubwa kipindi hicho Dodoma.siku nikipata muda nitaiongelea East zoo kadri niijuavyo.

Baada ya haponakumbuka marehemu ngwea muziki hakuwa sana alikuwa anacheza sana basket ball ambapo mwaka 2000 alifanikiwa kwenda mpaka kitaifa jijini Mwanza katika mashndano ya UMMISETA. Muda mwingialiutumia yeye kufanya mazoezi ya basket tofauti na malo star ambaye ndio alkuwa kichwakwenye kundi hilo na mez b ambaye alikuwa muuza sura enzi hizo anatembea kila siku na cd mkononi ambapo akikutana na mwanamke lazima amuonyeshe cd yao.

Baada ya ngwea kuja dar ndipo alipoanza sasa kuhustle kwenye muziki hasa baada ya matokeo yake ya form 4 kuwa sio mazuri kwani alipata divion 4 wakati darasani alikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi vichwa sana. Bwana malo star ama nzeku yeye aliendelea na masomo hapo ndipo kundi la chamber fleva guys liliposambaratika. QG ama mez b akapata zali la kufanya chorus kwenye nyimbo ya d-knob ambayo walifanya na video ITV enzi hizo za misanya bingi, ile dili ndio ilimpelekea mez-b kupata shavu la kufanya ngoma kwa majani iliyotoka kwa jina la fikiria 2001.

Hapa 2001 noorah baada ya kumaliza shule na yeye akakacha kwenda kwao shinyanga akaja dar ambapo akapata shavu la kufanya verse kwenye nyimbo ya shega tu remix ambapo ndipo chamber squard ikaundwa baada ya kukutana wanafunzi waliomaliza mazengo miaka mbali mbali. Nakumbuka majani akawapa shavu la kutengeneza nyimbo ingine hapa walifanya nyimbo iliyoitwa ahadi ya boss ambayo majani ndipo aliponyoosha mikono kwa ngwea na kuamua kumpa mkataba.japo mkataba wenyewe ulikuwa wa kihuni (MAJANI NA VENTURE NDIO WALIOFAIDI JASHO LA NGWEA) .

Noorah alipata zali yeye la kuwa chini ya sebastian maganga ambapo ndipo alitoa nyimbo ya vijimabo. Miezi 2 kabla ngwea hajatoa geto langu . Mwezi wa 3 mwaka 2003 ambapo majani aliiachia ili ipate kuhit ngwea na yeye awe mmoja wa wanamuziki ambapo walimsindikiza juma nature katika uzinduzi wa ugali hapa ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda kwenye maonyesho makubwa.ikumbukwe katika historia ya bongo fleva 2003 ndio mwaka waliotoka wanamuziki wengi zaidi ya 20 ambapo siku hizi kwa mwaka wakitoka wanamuziki wengi ni 5 (ntakuja kuwataja wanamuziki waliofanikiwa mwaka 2003).

Ngwea ntamkumbuka sana baada ya hapo alifuata na nyimbo ya napokea simu ft dullysykes. Akatoa ndani ya club akiwa amichange kiswahili ikumbukwe ngwea ndio mwanamuziki wa1 kubadilisha nyimbo ya kiingereza kuimba kiswahili.

Baada ya hapo ndipo alipotoa mikasi iliyokuwa kwenye albumya a.k.a mimithe best album up to now ikiwa na nyimbo kumi:
> Mikasi,
> a.k.a mimi ft tid
> Zawadi
> dakika 1
> weekend
> she got a gwan
> geto langu
> mademu zangu
> sikiliza
> napokea simu

Album iliuza sana ambapo kupitia ujanja wa venture aliyekuwa meneja alifanikiwa kununua gari na kujenga hapa ndipo bifu la majani na clouds lilipoanza.

Kwa leo niishie hapa maana naweza andika mpaka kesho ila ngwea ni mwanamuziki ambaye amefanya featuring na wanamuzik wengi sana karibia wote waliokuwa hot enzi hizo

Mungu amlaze maha pema ngwea mfalme wa muziki wa kizazi kipya (moyoni mwangu). Huyu ndio mwanamuziki aliyekuwa anaweza kurap,kuimba kila aina ya muziki uujuao na pia mkali wa mitindo huru na kuimba kiingereza

Kama kuna maswali wapi pa kurekebisha nilipokea unakaribishwa

************* Kumbukumbu ya miaka 2 ya kifo cha Mangwea*****************
Leo ni miaka miwili tangu kutokea kwa kifo cha mmoja wa Wanamuziki bora zaidi kuwahi kutokea katika Bongo Fleva, Albert Mangwea.

Mengi yamezungumzwa kuhusu kifo chake, na hakika ameacha pengo kubwa katika muziki huu .

Pumzika kwa amani, Albert Mangwea.

View attachment 255274


************** Kumbukumbu ya miaka 3 ya kifo cha Magwea****************
Leo ni miaka mitatu tangu bingwa wa michano na mkali wa muziki wa kizazi kipya mwenye kipaji cha kipekee Albert Mangwea atutoke.

Ni mazuri yapi unayokumbuka kutoka kwake?


Mimi nakumbuka siku anachukua tuzo ya Kili akatoa speech kwa mtindo wa freestyle.

Pia, nakumbuka wimbo wake remix ya Marques Houston, Clubbin aliufanyia cover ya kiswahili.

RIP CowObamma

************* Kumbukumbu ya miaka 7 ya kifo cha Magwea*********
Imetimia miaka 7 leo tangu amefariki Dunia Mwanamuziki nyota wa muziki wa kizazi kipya(Bongofleva) Albert Mangwea.Mangwea alifariki nchini Afrika Kusini alipokwenda kwa shughuli za muziki, Taarifa ya Daktari ilieleza kuwa Bingwa huyo wa Hip Pop na 'Free Style' alifariki kwa sababu ya matumizi ya Dawa za kulevya na Ulevi yaliyopita kiwango( Alcohol and Drug Overdose).

Ghetto langu na Mikasi ni nyimbo zake zilizotamba sana.
 

Sehemu ya waombolezaji waliokwenda kumuaga marehemu Ngwea ikiwa kwenye pilikapilika za kutaka kumuona kwa karibu msanii Diamond, hivyo kuvunja utaratibu mzima, wakati shughuli hiyo inaelekea mwishoni katika viwanja vya Leaders Club leo.
 

Jay Moe, akizungumza Live na kituo cha Redio kutoka viwanjani hapo.....

Wasanii wakipita kutoa heshima za mwisho.....

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..

Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa Filamu, waliojitokeza kwenye shughuli hiyo..

Dj Choka, akimshikilia msanii wa muziki wa kizazi kipya, Q-Chillah, aliyekuwa akiangua kilio baada ya kupita na kutoa heshima zake za mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mangwea...
 

Hii ndiyo Kamati ya maandalizi ya kufanikisha shughuli hiyo.....

Wengine pia walikuwa ni vituko kwa aina ya mavazi, kama mwandishi huyu alionekana akiwa ametinga nguo inayomuonyesha mwili wake.....

Heshima za mwisho....
 

Vijana wakifukuza gari la Msanii Mr. Blue wakitaka asimame ili wamzonge kama walivyofanya kwa Diamond....
 


Askari Polisi wakituliza ghaasia zilizokuwa zikitokana na wananchi waliokuwa wakijaribu kuwahi foleni...

Mbunge wa Konondoni, Idd Azan, akiongoza kuaga......na kutoa heshima za mwisho.....

Wasanii wakiwa kwenye foleni ya kwenda kuaga......

Msanii Keisher, akipita kutoa heshima za mwisho.....

Gadna G Habash, akiongoza shughuli hiyo....

Mzee Magari na wasanii wa Filamu wakipita kutoa heshima za mwisho......

Mheshimiwa Temba akipita kuaga....

Polisi Jamii wakiranda na mbwa kudhibiti vurugu.....

G Habash akizungumza .....

Wasanii wakipita kuaga.....

Msanii Dogo Hamidu, akipiga saluti ........

Msanii wa kundi la The Comedy, Joti, akipita kutoa heshima zake za mwisho...
 
DSC_0520.JPG
Askari akiongoza msfara uliobeba mwili wa Mangwea mara baada ya kuwasili Mikese Morogoro amb ulpokelwa na wasanii wa fani mbali mbali pamoja na mashabiki wa marehemu
Mashabiki wa Mangwea wakiwa wanakimbia sambamba na gari liliobeba mwili wa marehemu
Msafara wa magari yaliyokuwa yanaelekea msibani kutoka Dar
Msafara ukiendela
DSC_0570.JPG
Umati wa watu kando kando ya barabara wakiusubiria mwili wa mpendwa wao
DSC_0565.JPG
Mashabiki wa Mangwea wakiwa kando kando ya barabara katika mzunguko wa Msamvu Morogoro wakati msafara ukielekea nyumbani kwao Kihonda
Mapokezi ya mwili wa Mangwea eneo la Mazimbu road Kihonda
Mwandishi na mpiga picha wa Abood Media Salum akiwa kikazi zaidi
Basi la Abood likiwa limesima Mikese wakisubiria msafara wa wa gari liliobeba mwili wa marehemu Mangwea. Basi hiloambalo lilwabeba wasanii wa fani mbali mbali
Gari lilio beba mwili wa marehemu Mangwea liliingia nyumbani kwao Kihonda Morogoro
Watu ni wengi sana na wengi ikawalizamu kupanda ju ya mti ili wapate taswira nzuri
Mwili wa marehemu Mangwea ukirudishwa kwenye gari tayari kwa kupeleakwa mochwari kwaajili ya kuhifadhiwa
 
[h=2][/h]




Siku moja baada ya kifo cha marehem Ngwea, Dully alikuwa na safari ya kuelekea Mwanza, ambapo alikaa huko kwa muda wa siku mbili na kurudi, kwakuwa alikuwa akiendesha mwenyewe gari lake kuelekea Mwanza na kurudi, Dully aliamua kubaki Morogoro tangu siku ya juma tatu kuusubiri mwili wa Ngwea, ambapo kwa sasa yupo na afande sele na wananchi kibao maeneo ya nane nane, wakisubiri kuusindikiza mwili wa marehem kutoka maeneo hayo




 
Hizo sefuria za ubwabwa mbona kama utani?
Inasikitisha ambavyo kijana huyu amethaminiwa baada ya kifo. Kati ya haoashabiki ukiuliza wangapi walishawahi kuhudhuria show ama kununua genuine album, utachoka. Sijui tukoje.
 
Dah Kinacho nikeraga siku zote ni mavazi ya waombolezaji misibani aisee!! Ivi kioo cha jamii kinamreflect nani? Mtu anawezaje kuvaa nguo mikono mikato bila hata kujitanda msibani? Mwingine anavaa trouser imembana na miwani mikubwaa eti kajisitiri!! Wanaendaga kumuonyesha nani? Mbona %kubwa Ya wasanii wetu wamezaliwa vijijini tu? vipi leo wajidai eti nao wanaishi kinje. Aaaaah wananiboa sana.
WebRep

line-dark-horizontal.png
Overall rating
line-dark-horizontal.png




line-dark-horizontal.png
 
Mmmhh
Sauda Mwilima hapo tena na nguo yenye
kuonyesha maungo ni nini msibani.
 
Hizo sefuria za ubwabwa mbona kama utani?
Inasikitisha ambavyo kijana huyu amethaminiwa baada ya kifo. Kati ya haoashabiki ukiuliza wangapi walishawahi kuhudhuria show ama kununua genuine album, utachoka. Sijui tukoje.
Yani sisi wanadamu tumejaa unafiki mkubwa
 
Hizo sefuria za ubwabwa mbona kama utani?
Inasikitisha ambavyo kijana huyu amethaminiwa baada ya kifo. Kati ya haoashabiki ukiuliza wangapi walishawahi kuhudhuria show ama kununua genuine album, utachoka. Sijui tukoje.
Binadamu kwa kuigiza nimenyanyua mikono juu...Sasa hivi wana uchungu sana na kikubwa zaidi ni kujionyesha.....embu watu wabadilike, upendo wa dhati uonekane mtu akiwa hai .
 
Ni safari ya mwisho dah!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom