Safari ya Mwalimu Bukoba wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na Ramadhani Kingi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,910
30,253
Ramadhani Kingi anachangia makala yangu kuhusu safari ya Mwalimu Nyerere UNO 1955 hapo chini ndiyo aliyoandika:

''Hapa kuna kitu kikubwa sana hakijatajwa.

Ili kufanikisha safari hii ya Mwalimu michango ilipitishwa kwenye majimbo! Jimbo la Ziwa: MZEE ALHAJ SUED KAGASHEKI alichanga shs 90/= kwa safari hii.

Ikumbukwe pia katika safari ya Mwalimu Jimbo la Ziwa Wakoloni nina maana Waingereza walihakikisha Mwalimu hapati mahali pa kulala akishafika Bukoba.

Ilikuwepo Hoteli moja ya maana Bukoba. Waingereza walihakikisha Booking inafutiliwa mbali.
Meli iliimfikisha Bukoba MV. USOGA saa 12.00 alfajiri.

Walipokekelewa hapo Kastamu kwa gari ya Sued Kagasheki na moja kwa moja hadi Lake Hotel (Hotel ya Paul Lohnberg) na hapo walikuta booking hamna.

Mzee Sued Kagasheki hakushangazwa na hilo na ilibidi akitumie kichwa chake na kupata jibu la haraka.

Alikuwa na nyumba mbili Uswahilini Bukoba.
Waingereza wakiwa na shauku ya kujua Mwalinu atafikia wapi walifuatilia sana nyendo hizi.

SUED alimpeleka mgeni wake nyumba yake ya mjini hapa Bwana Hamza Mufundi anapotengenezea gah-wa (maeneo haya sambamba na nyumba ya kulala wageni ya Lugusha) na humo alimpumzisha mgeni wa TANU.

Mipango ya maandalizi ya staftahi na chakula ilifanywa sawia.

Mama Nujaka, Mama Maua, Mama Hawa, Mama Ramia, Bint Mwinyi, Mama Boi, Mama Kimwinyi, Bint Kaijage, Mama Ramia na Mama wengine wa Kimanyema walikwishaandaliwa kwa maandalizi ya mapokezi.

Mipango ilibadilishwa kwa siri na akina mama hawa kwa siri ya hali ya juu wote walihamisha kambi yao hadi Rwamishenye kwenye jumba la Sued Kagasheki na kuanza kuandaa vilivotakiwa.

Kumbukumbu ziko wazi! Waziri Mkuu Rashid Kawawa baada ya kulitembelea hili jumba alitoa ahadi kuwa TANU ingelifanyia ukarabati kama Kumbukumbu ya TANU, leo miaka 50 na ushei hamna lolote.

Ulifanywa mpango akina mama kwenda Rwamishenye kwa usiri mkubwa.

Waliandaa mambo huko na safari za Mwalimu kuanzia huko Kanyangereko Maruku na hii ikiwa ni mbinu za kuwakwepa makachero wa kikoloni waliokuwa wakifuatilia nyendo za ugeni huu.

Wakitokea Maruku walipitia Rwamishenye na kujipatia stafutahi na baadaye kuteremka mjini.

Makachero waliingiwa taharuki kwani hawakuweza kufahamu nyendo hizi.
Akina mama waliendelea kuandaa hata mlo.

Waingereza hawakajua kituo cha Mwalimu.

Alikaa kwa mapumziko Uswahilini na baadaye kuanza safari za vijijini.
Hakuna aliyejua Mwalimu angelilala wapi.

Hii ilibaki ni siri ya Waandaaji.
Mzee Sued akiwa na makazi sehemu tatu nne hivi aliwachanganya sana Waingereza.

Marehemu Salum Juma Karwani dereva wa Mwalimu pekee ndiye aliyebeba dhamana ya kujua nyendo, malazi na makazi ya ujio huo.

Siwezi nikakuambia Mwalimu alilala nyumba gani bali mpango uliosukwa uliwachanganya Waingereza.

Hadi anaondoka Jimbo la Ziwa(Lake Province) Mwalimu alikuwa benet na Sued Kagasheki. (Chei naremwa hadithi hii ni ndefu) kwani inakwenda zaidi kuangalia wafungwa wa kwanza wa Kisiasa Tanganyika nzima ni Marehemu Mzee Ally Migeyo na Mzee Ayoub Rubai.

Kuna mambo mengi ya kusimulia katika harakati za kuutafuta uhuru Jimbo la Ziwa.

Jimbo hili ndilo lililoongoza nchi nzima kuichangia TANU pamoja na kuwa wengi nje ya Jimbo hufanya dharau kwa Kagera kama wanavyojaribu kudharau historia sahihi anayoitoa Mohamed Said.''

Ramadhani Kingi anaongeza kufafanua:

Marehemu Alhaj Sued Kagasheki alikuwa beneti na Mwalimu. Waingereza walimwinda sana Nyerere.

Mzee Sued akitumia gari yake mwenyewe alimpeleka kwanza Uswahilini baada ya dakika kadhaa walimpeleka Kanyangereko Maruku kijijini kwa Sued.

Hakukaa sana huko akamrejesha mjini huku akina mama wa Kiswahili walikwishapandisha mlima kwenda Rwamishenye na kuendelea na maandalizi ya stafutahi na chakula kwa mgeni wao.

Kutokea Kanyangereko Mwalimu alianza safari vijijini.

Ni bahati mbaya hawa wazee Salum Juma Karwani Dreva wa Nyerere katikati ya tishio la kukamatwa na Mzee Sued Kagasheki hawakutishika hata walipoitwa na DC (Mkuu wa Wilaya).

Yapo mengi na hata picha za niliyoyaandika zipo kama imperical evidence.

Tanganyika nzima tukimwondoa Baghdellah, Wazee wawili Ayoub Rubai na Ally Migeyo ndio wafungwa wa kisiasa pekee kutokana na TANU kama ilivyokuwa kwa ANC na Mandela.
 
Mwalimu kweli alikuwa kiongozi wa kipekee. Sishangai pamoja na kuwa na mbari, makabila na dini kadhaa bado tukabaki wamoja.

Nyakati flani wakaja Watu na ajenda zao kumfitinisha Mwalimu tena kwa hotuba na makala chungu nzima (baadhi hata jina Mwalimu wakilitenga) lakini leo wamepita na waliobaki sasa hivi wakimwita Baba wa Taifa!

Kulifinyanga Taifa hili na kujihisi wamoja haikuwa kazi rahisi
 
Back
Top Bottom