Safari ya mamajusi kuelekea yerusalemu na safari ya wachungaji kuelekea dodoma

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,447
630
Ukisoma Biblia Takatifu katika injili ya Mt. Mathayo (2:1-12) inaelezea habari ya Mamajusi wakati wa kuzaliwa Bwana Yesu, ambao walitokea nchi zilizopo mashariki mwa Israeli kwa kufuata Nyota na wakakutana Yerusalem kwa pamoja licha ya kuwa walikuwa wakitoka nchi tofauti, ila wote walikuwa na lengo moja tuu lakumwona mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa yaani Yesu . Niliposoma habari hii nimeona inafanana kwa asilimia 20 % na habari ya wachungaji kutoka sehemu mbalimbali za nchi kufika Dodoma kwenda kumuomba Lowasa agombee, walipofika kwa Lowasa wachungaji walisema wamefika Dodoma bila ya kushawishiwa na mtu yeyote na wamejigharamia safari zao. Nasema inafanana kwa asilimia 20% kwa kigezo kimoja tuu, kwamba wachungaji wote waliweza kukutana Dodoma kwa lengo moja na kwa wakati moja kutoka wilaya tofauti kama Mamajusi walivyokutana Yerusalem kwa lengo moja na kwa wakati moja kutoka nchi tofaouti. Lakini tusisahau inatofautiana pia kwa asilimia 80% na habari ya wachungaji kwani tofauti na Mamajusi walioeleza kuwa walifika Yerusalemu kwa kuongozwa na Nyota, wachungaji hawa hawajasema chochote nini kiliwaongoza kutoka Kisarawe, Kiteto, Mleba, Makete, Newala ,Kasulu na wilaya nyingine za Tanzania mpaka wakafika Dodoma kwa pamoja na kwa wakati mmoja. Pia inatofautina na na habari hii ya Mamajusi kwani Mamajusi hawakuwa na mawasiliano kabisa na mwenyeji wao, ndio maana walipofika Yerusalem baada ya mawasiliano ya Nyota kupotea ilibidi wamuulize Mfalme Herode kuhusu wapi mtoto alipozaliwa lakini kwa upande wa Wachungaji inaonekana kulikuwa na mawasiliano kwani walipofika Dodoma wakakutana na Hamisi Mgeja yule Mwenyekiti wa CCM Shinyanga na kuwapeleka mojamoja kwa Mheshimiwa, na walipofika cha ajabu maturubai na chakula kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa ajili yao na waandishi wa habari walikuwa wameshaitwa , na mheshimiwa kwa bahati nzuri alikuwa mlangoni na bahati nzuri siku hiyo na mda huo alikuwa nyumbani na wala hakuondoka, kama si Mheshimiwa kushinda nyumbani wachungaji wetu wangepatwa na karaha. Tofauti ya tatu ni kuwa Mamajusi hawakuwa na sababu ya kuweka utetezi ni kwanini wao wakufika Israeli kumwona Yesu,ila wachungaji licha ya kufika Dodoma na kueleza dhamira yao lakini cha ajabu walianza kutoa utetezi kuwa ,sisi hatujashawishiwa na mtu kufika hapa, mara sisi tumejichangia wenyewe kufika hapa. Kimsingi nafikiri Mamajusi hawakuona sababu ya kutoa utetezi kwa vile jambo walilolifanya lilikuwa ni la heri na lisilo zua shaka la nafsi, ila nafikiri wachungaji waliona ni heri waweke utetezi kwani nafsi zao ziliwasuta hata kabla hawajashutumiwa
 
Back
Top Bottom