Safari ya Mama Samia Tanga imejaa fumbo la kiimani?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Natafakari safari ya Mama Samia kwenda Tanga, najiuliza alirejea lini Dar, najiuliza kwanini safari ya Waziri Mkuu ilifutwa ya Makamu ikawepo?

Haya maswali yananifanya niamini nchi inapita kipindi kigumu ambacho ratiba za wanadamu na mipango ya wanadamu haiwezi kutimia bali mipango ya Mwenyenzi Mungu ndiyo inabaki kutimia.

Hata Kama wapo wenye uchu wa madaraka Basi Mungu aliwapa upofu na ametushindia tunasonga mbele na niombe azidi kumpa nguvu mama avuke siku mia baada ya mazishi naamini atakuwa amemaliza kutengeneza safu na kuwawajibisha wale wote waliotumwa na movu shetani kutaka kuharibu jina zuri la Tanzania.

HONGERA Tanzania Mwenyenzi Mungu tupo nawe Sasa na hata milele. Amen
 
Natafaiari safari ya Mama Samia kwenda Tanga, najiuliza alirejea lini Dar, najiuliza kwanini safari ya Waziri Mkuu ilifuta ya Makamu ikawepo? Haya maswali yananifanya niamini nchi inapita kipindi kigumu ambacho ratiba za wanadamu na mipango ya wanadamu haiwezi kutumia bali mipango ya Mwenyenzi Mungu ndiyo inabaki kutimia...
Safari ya mama Tanga haikuwa safari ya kawaida.

Wengine tulichagua kukaa kimya.
 
Natafaiari safari ya Mama Samia kwenda Tanga, najiuliza alirejea lini Dar, najiuliza kwanini safari ya Waziri Mkuu ilifuta ya Makamu ikawepo? Haya maswali yananifanya niamini nchi inapita kipindi kigumu ambacho ratiba za wanadamu na mipango ya wanadamu haiwezi kutumia bali mipango ya Mwenyenzi Mungu ndiyo inabaki kutimia...
Hujaeleza unayapi kichwani mkuu nasi tukakuelewa!

Wewe matukio ya ziara hizo uliyasoma hivyo, au kuna la ziada ulijualo tusilolijua wengine?

Kwa kuwa wengine hatujui uyajuayo, tunaweza tukayaona yaliyotokea kama serikali iliyovurugika akili wasijue lipi la kufanya!

Nchi yetu inayo mifano mingi, mingine mingi imeonekana katika msiba huu: serikali (watendaji), wamekuwa watu wa kufanya tu mambo, hata kama hawafuati taratibu zozote zinazotakiwa kufanywa katika kushughulikia aina fulani ya mambo. Katika kufanya hivyo ndipo panapotokea mikanganyiko wasiyokuwa wanaitegemea kutokea.

Wewe fikiria, hata ratiba tu ya msiba unakuwa na mkanganyiko, kivipi? Mara siku 14, mara 21, mara Zanzibar..., kuna kitu gani kigumu katika kuteua kamati inayoeleweka kiutaratibu na kuweka yote haya sawa kabla ya kuyatangaza?

Hicho ndicho ninachokiona kwenye utendaji wa serikali yetu. Taratibu hazizingatiwi, na kufanya mambo bila taratibu ni uvurugaji.

Naomba serikali walione hili haraka na wafanye juu chini turudi kwenye mstari. Vinginevyo tutaelekea kuwa "Banana Republic" kikamilifu.
 
Mpaka watu wakaanza kupiga kelele ndio wakatangaza, siku waliyotangaza asubuhi yake CHADEMA waliita press, juzi yake ACT waliuliza nani anaongoza nchi. Bado system ina wazalendo walioweka maslahi ya Taifa mbele kuliko uchama, ukabila, ukanda, udini n.k na hili linatupa faraja sana.
 
Mnaotaka Siri hyo nendeni kwenye Uzi wa kudukuliwa pacemaker ya Rais , ndani ndani humo mbona watu wamefunguka mengi.... Why ziara ya VP Tanga ( Kikwete , Mabeyo & Mwamnyange engineering the situation) tangazo la msiba kutumwa toka Tanga to TBC HQ under Army command to escape Majaliwa & Bashiru interference.
 
Wakuu tunasubiri madini hayo, Jiwe halipo tena. Mnaogopa nani mwingine huko?
Kilichoogopesha na kinachoogopesha wengi si jiwe bali waliokuwa nyuma ya jiwe na sasa inawezekana wako nyuma ya bi Tarabushi watu bado hawana hakika
 
Hapana kati ya tarehe 9/32021- 17/3/2021 watu walikuwa wanajipangia safu ya kuongoza nchi bila kufuata katiba , kuiba mabilioni kwanza 96 bilioni, pili 180 Biloini , wangine wamezitumia kuhonga wajumbe wa kamati kuu ili wapate madaraka hasa VP there are more than that .
Wamechota mapesa hata jamaa hajazikwa? Nchi tumekwisha tutamkumbuka JPM, sijui Kama mama atawaweza Hawa majizi. Naona ndo maana yanafurahia kifo Cha JPM.
Sasa nimeelewa kwanini Kuna watu wanafurahi.
 
Hujaeleza unayapi kichwani mkuu nasi tukakuelewa!

Wewe matukio ya ziara hizo uliyasoma hivyo, au kuna la ziada ulijualo tusilolijua wengine?

Kwa kuwa wengine hatujui uyajuayo, tunaweza tukayaona yaliyotokea kama serikali iliyovurugika akili wasijue lipi la kufanya!

Nchi yetu inayo mifano mingi, mingine mingi imeonekana katika msiba huu: serikali (watendaji), wamekuwa watu wa kufanya tu mambo, hata kama hawafuati taratibu zozote zinazotakiwa kufanywa katika kushughulikia aina fulani ya mambo. Katika kufanya hivyo ndipo panapotokea mikanganyiko wasiyokuwa wanaitegemea kutokea.
Wewe fikiria, hata ratiba tu ya msiba unakuwa na mkanganyiko, kivipi? Mara siku 14, mara 21, mara Zanzibar..., kuna kitu gani kigumu katika kuteua kamati inayoeleweka kiutaratibu na kuweka yote haya sawa kabla ya kuyatangaza?

Hicho ndicho ninachokiona kwenye utendaji wa serikali yetu. Taratibu hazizingatiwi, na kufanya mambo bila taratibu ni uvurugaji.

Naomba serikali walione hili haraka na wafanye juu chini turudi kwenye mstari. Vinginevyo tutaelekea kuwa "Banana Republic."
Mara maziko tarehe 25 mara 26!
 
Back
Top Bottom