Safari ya Mabana

Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
5,149
4,674
Kwa wenye kumbukumbu vizuri, february 2011 tulikuwa na kikao pale Lunch time Hotel. Moja ya maazimio ilikuwa ni kupata shamba kubwa kwa ajili jf members wanaopenda kilimo.

Kwa upande wa misitu mambo yanaenda vizuri, upande wa mifugo pia tumeanza na mguu mzuri, soon tutakuwa na kijiji chetu cha wafugaji Mkuranga. Kwa upande wa nafaka,ilitulazimu kwenda Mabana, mbigiri hatimaye Chamtama huko Mvomero. Huko kuna ardhi kubwa sana ambayo bado haijaguswa na iko kando ya mto, inarutuba sana na haina wakulima. tatizo nililoliona ni namna ya kufika wakati wa masika,hakuna njia. Tulipita na gari kwa kufuata njia za ng`ombe.

Mbigiri kuna nyanya nyingi sana,ila hakuna wakulima wazuri wa nyanya, tuliona shamba kubwa sana la nyanya( nikiweza nitatuma picha), mpunga huko ndio kwenyewe,alizeti/mahindi/mtama/migomba. Wanyama wanastawi sana, tatizo wizi wa mifugo, na nyani.

Tunahitaji nguvu ya pamoja ili kufanya mambo makubwa huko Chamtama, mtu mmoja mmoja ni kazi kubwa hasa kwa sisi tunaotegemea mshahara. Option ya pili, ni kuchukua upande wa Vidunda ili kupunguza taabu ya njia. Ni karibu sana na barabara kuu. Plan ya kwenda tena Vidunda ipo ili tuweze kuwa na uchaguzi sahihi
 
Vidunda ipo wapi mkuu? Nadhani naweza kujiunga nanyi kama opportunity ipo!
 
Ipo Morogoro, unachepuka kutoka barabara kuu iendayo Dom kabla hujafika Wami Dakawa kuingia kushoto along the Wami plain.

Fursa zipo, mkakati ni kupata timu nzuri ili tupate kuanzisha kijiji cha uzalishaji wa kisasa kwa gharama nafuu.
 
Kwa wenye kumbukumbu vizuri, february 2011 tulikuwa na kikao pale Lunch time Hotel. Moja ya maazimio ilikuwa ni kupata shamba kubwa kwa ajili jf members wanaopenda kilimo.

Kwa upande wa misitu mambo yanaenda vizuri, upande wa mifugo pia tumeanza na mguu mzuri, soon tutakuwa na kijiji chetu cha wafugaji Mkuranga. Kwa upande wa nafaka,ilitulazimu kwenda Mabana, mbigiri hatimaye Chamtama huko Mvomero. Huko kuna ardhi kubwa sana ambayo bado haijaguswa na iko kando ya mto, inarutuba sana na haina wakulima. tatizo nililoliona ni namna ya kufika wakati wa masika,hakuna njia. Tulipita na gari kwa kufuata njia za ng`ombe.

Mbigiri kuna nyanya nyingi sana,ila hakuna wakulima wazuri wa nyanya, tuliona shamba kubwa sana la nyanya( nikiweza nitatuma picha), mpunga huko ndio kwenyewe,alizeti/mahindi/mtama/migomba. Wanyama wanastawi sana, tatizo wizi wa mifugo, na nyani.

Tunahitaji nguvu ya pamoja ili kufanya mambo makubwa huko Chamtama, mtu mmoja mmoja ni kazi kubwa hasa kwa sisi tunaotegemea mshahara. Option ya pili, ni kuchukua upande wa Vidunda ili kupunguza taabu ya njia. Ni karibu sana na barabara kuu. Plan ya kwenda tena Vidunda ipo ili tuweze kuwa na uchaguzi sahihi

Chonde tusiingie maeneo ya mafisadi tu... Mvomero wameigawana ka mbwa mwitu wanavyomgawana sungura..
 
Hilo nalijua vizuri,huko kunahitajika ujasiri kwenda, hakuna barabara kabisa, hata uendaji ni lazima uwe na mwenyeji halafu ww mwenyewe uwe ngangari,mafisadi wamejazana Dakawa Nafco/Matombo/Turiani/Mvuha. Ukikaa mbali nao nani atakuletea miundombinu wewe(kuna moja limevuta umeme km kadhaa mpaka walala hoi tunakaribia kuupata huko huko porini)kaa nao karibu, banana nao humo humo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom