Safari ya kwanza ya treni ya umeme kufanyika Novemba 2019

#Magufuli_Effects.

Safari ya Kwanza ya Treni ya Umeme hapa Tanzania itakuwa Mwezi Novemba Mwaka huu wa 2019, itakuwa kutoka Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.

Ikumbukwe hii ni baada ya ujenzi wa reli ya SGR ambayo inatakiwa kufika Mwanza na Kigoma kukamilika awamu ya kwanza ya kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.

Treni hii itakuwa na uwezo wa kutoka Dar-Moro au Moro-Dar zaidi ya mara 8 kwa siku ikitumia dakika 75-80 yaani saa moja na dakika kumi na tano au ishirini kufika Dar au Moro spidi kwa treni ya abiria ni 160km/hr

Wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wazalishaji wa viwandani nk ni fursa kwao kwani gharama zake ni 30% chini ya usafiri wa magari hakika ni nafuu.

Tunapiga Hatua. Tuwe wenye subira.

View attachment 986614

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kwamba hiyo Nov 2019 bado haijafika au mnatafuta sababu ya kupiga hela za walipa kodi?
 
Mabumunda ya Lumumba nawakumbusha tu kuwa kwenye assigment zenu msisahau kulitete na hili. Leo ni June 2020. Safari ya kwanza ilipaswa kuwa Nov 2019.

Kama corona ni sababu mtueleze ili msituchoshe kuuliza.

Cc johnthebaptist

Ni kweli ilikuwa ianze Nov 2019 lakini kutokana na mvua mabazo zilikwamisha ujenzi, ilibidi Mkandarasi ahamie kwenye Reli kutoka Morogoro hadi Makutopora. Ukiangalia kwa kazi ambayo imefanyika utaona kabisa kwamba 77-79% Dar- Moro imekamilika na Morogoro - Makutopora 20-30% imekamilika. Kama ni mtaalam wa mahesabu utaona kwamba kama kungekuwa hakuna changamoto za mvua nyingi Morogoro - Dar ingekuwa live. Usiwe na shaka hiyo itakuwa zawadi ya ushindi wa Kimbunga cha October na Nov-Dec inafunguliwa.
 
Kwa hiyo taratibu za mikataba hazizingatiwi tena mnajali kufungua oct ili mshinde uchaguzi?

Mvua mwaka jana zilianza Sept. Kama ni kuchelewa angechelewa kwa miezi miwili au 3. Mvua zimeacha kunyesha tangu April. Kwa nn reli haikamiliki?

Na vp ile treni ya wonyesho Dsm to Moshi(Arusha?)..bado inafanya kazi? Au ni hadi Oct ndipo mkapige nayo picha tena pale Moshi?
 
Back
Top Bottom