Safari ya kwanza ya treni ya umeme kufanyika Novemba 2019

#Magufuli_Effects.

Safari ya Kwanza ya Treni ya Umeme hapa Tanzania itakuwa Mwezi Novemba Mwaka huu wa 2019, itakuwa kutoka Jijini Dar es salaam kuelekea Mkoani Morogoro.

Ikumbukwe hii ni baada ya ujenzi wa reli ya SGR ambayo inatakiwa kufika Mwanza na Kigoma kukamilika awamu ya kwanza ya kutoka Dar es salaam hadi Morogoro.

Treni hii itakuwa na uwezo wa kutoka Dar-Moro au Moro-Dar zaidi ya mara 8 kwa siku ikitumia dakika 75-80 yaani saa moja na dakika kumi na tano au ishirini kufika Dar au Moro spidi kwa treni ya abiria ni 160km/hr

Wafanyabiashara, wajasiriamali, wakulima, wafugaji, wafanyakazi, wazalishaji wa viwandani nk ni fursa kwao kwani gharama zake ni 30% chini ya usafiri wa magari hakika ni nafuu.

Tunapiga Hatua. Tuwe wenye subira.

View attachment 986614

Sent using Jamii Forums mobile app

Ingia uedit haraka hii propaganda mfu. Tena usiweke tarehe ya kuanza bali sema siku Mungu akipenda.
 
Huu mradi wa SGR naona ulikuwa ni usanii wa kwenye majukwaa tu. Utajengaje reli mpya kwa gharama kubwa kihivyo huku hata reli ya zamani umeshindwa kuitumia..!!

Hii reli ya SGR haina Economic Viability kwani volume ya mzigo unaolenga kusafirishwa na hiyo reli ni ndogo hata kwa hii reli ya Metre Gauge hivyo ingegeuka kuwa Another White Elephant Project kama Tazara.

Hata ile ya Kenya pamoja na kushusha gharama ili watu waachane na malori lkn bado ina-struggle kupata mizigo.

Hii SGR Rail Frenzy iliyopo ktk haya mataifa ya East Africa haina mantiki yoyote kiuchumi zaidi ya sarakasi za kisiasa tu zitakazoacha haya mataifa na madeni makubwa huko mbele.
 
Large-scale infrastructural projects ndiyo rahisi kwa wanasiasa kupiga pesa za wanyonge.
 
We jamaa sijajua ni mods mnaleta huu uzi hamjui kuwa mnafanya uchochezi. Wenzenu tulidhani Nov 2019 bado.
 
Back
Top Bottom