Safari ya kwanza ya Rais Samia Ulaya ni vizuri iwe Ujerumani

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Binafsi nimeshaanza kuuona mwanga kupitia mboni za macho ya Rais Mama Samia. Ninamuona Rais Samia akizifuata nyao za Angel Makel wa Ujerumani.

Kama Rais mwanamke ni vizuri covid 19 ikipungua aombe kwenda kumtembelea chancellor wa Ujerumani Mama Angel Makel kwa uzoefu na pengine kubadilishana mawazo juu na namna ya kukabikiana na changamoto za kiongozi mkuu mwanamke na ikibidi apate uungwaji mkono na Ujerumani katika kutatua changamoto za Watanzania.

Kama Mwanamke mwenzake ni heshima sana kama ziara yake hata kama ikiwa moja ya ulaya iwe Ujerumani na ya pili Marekani akakutane na makamu wa Rais wa Marekani kwasababu hizohizo za viongozi wanawake kupeana joto na support katika kutatua changamoto za watu wao.

Ni mawazo yangu tu.
 
Wewe ndege zetu zitazidi kupata hasara, Mana mama anatumia Gari ndani ya mkoa tu
Mama yetu yuko makini ba kila step moja anayosonga mbele. Anataka kuliunganisha taifa kwanza kisha taifa na dunia. Anayafahamu makosa na mazuri ya watangulizi wake bara na visiwani.
 
Hatuna Rais, tuna mzurulaji Ikulu, hajatembelea hata mradi mmoja wa kimkakati kila saa yupo kwenye mapambio na safari zisizo na tija kwa watz wengi.
 
Hatuna Rais, tuna mzurulaji Ikulu, hajatembelea hata mradi mmoja wa kimkakati kila saa yupo kwenye mapambio na safari zisizo na tija kwa watz wengi.
Miradi imejaa wapigaji wacha uhakiki ukamilike kwanza ili akienda huko ni safari ya kuni na mboga.
 
Nayakubali mawazo yako
Tuitumie kikamilifu hii karata ya kuwa na Kiongozi mwanamke. Kama huyu Rais wetu Samia angekuwa wa nchi kama Kenya sasa hivi tayari mbiombio angeshafika Ujerumani kwa Angel Makel na kunywa kahawa pamoja na kujipanga wiki ijayo kwenda kuonana na Kamara kule US
 
Akimaliza hizo za wanawake wenzake ni zamu ya Ubelgiji kumfata Mzalendo wa Kweli TL
 
Kuwa na Rais mwanamke kuna faida kubwa sana katika kukuza uchumi katika kuongeza ushawishi wa uwekezaji kwa kila Sekta nchini. Naomba sana atafute wawekezaji watakao wekeza viwanda vya kuchakata mazao kutoka sehemu yanapolimwa kwa wingi.Mfano kilimo cha mananasi Kiwangwa Bagamoyo na sehemu nyingine. Hii itasaidia kuongeza ajira na mzunguko wa pesa na wakulima kunufaika zaidi. Kuliko mazao kuozea shambani kwa kukosa soko
 
Tuwaruhusu wajerumani watoe hazina zao tufaidike sote kuliko zitakavyopotea baada ya kuanza kupotea kwa baadhi ya alama
 
Back
Top Bottom