Safari ya kwanza ya Rais Samia nje ya bara la Afrika: Nini manufaa yake kwa nchi?

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
46
125
SAFARI YA KWANZA YA RAIS SAMIA NJE YA BARA LA AFRIKA: NINI MANUFAA YAKE KWA NCHI?

Imeandikwa na Seleman Kitenge na Mhandisi Fatma Rembo

Umuhimu wa Diplomasia kwa Mustakabali wa Taifa

Ulimwenguni kote hakuna nchi ama taifa lolote iwe lililoendelea au linaloendelea ambalo limejitosheleza kwa mahitaji yake yote ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata ya ulinzi na usalama wa raia na mipaka yake bila kutegemea mataifa mengine. Ushirikiano baina ya nchi hutoa fursa kwa nchi husika kushirikiana katika kushughulikia changamoto au hatari mbalimbali zinazoweza kuhatarisha uhai wa mataifa hayo.

Mahusiano ya kidiplomasia ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoyakumba mataifa mbalimbali duniani. Changamoto hizo ni kama vile magonjwa ya milipuko, mabadiliko ya tabia nchi, uhaba wa nishati, uhaba wa chakula na maji, ugaidi, uhamiaji haramu, utoroshwaji wa fedha haramu nje ya nchi, uhalifu wa kuvuka mipaka na migogoro mbalimbali inayohatarisha amani na usalama wa dunia.

Lakini pia, diplomasia haishii tu kwenye ushirikiano wa kutatua changamoto ambazo zinahatarisha maslahi ya pamoja baina ya nchi bali inakwenda mbali zaidi katika kuhakikisha nchi zinapata mahitaji yake muhimu. Mahitaji hayo yanaweza kupatikana kupitia biashara za kimataifa, kubadilishana taarifa na maarifa, misaada ya kisayansi na teknolojia, pamoja na misaada ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa mantiki hiyo, pasipo kuwepo na urafiki na ushirikiano wa uhakika baina ya mataifa si tu itakuwa ngumu kwa nchi kukidhi mahitaji yake bali pia itajihatarishia usalama na nafasi yake kwenye majukwaa ya kimataifa ya utoaji maamuzi juu ya ajenda mbalimbali za maendeleo ya dunia.

Kama ilivyo kwenye familia udugu huimarishwa kwa kutembeleana na kujuliana hali, hivyo hivyo kwenye nyanja ya diplomasia kutembeleana huongeza uhai wa ushirikiano na urafiki baina ya mataifa.

Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia Marekani

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya mabadiliko katika sera yake ya awali ya mambo ya nje ambayo ilijikita zaidi kwenye ukombozi wa uhuru wa kisiasa wa bara la Afrika ili kujikita kwenye ukombozi wa kiuchumi. Ni wazi kwamba nguvu ya kiuchumi sio tu inatuhakikishia usalama wa kisiasa, kijeshi na kijamii ila inatupa fursa pia ya kuweza kulinda tunu na maslahi ya taifa letu kwenye dunia yenye ushindani mkubwa.

Hivyo basi, Rais Samia Suluhu Hassan ametambua fika ili tuweze kufikia dhana ya nchi yetu ya kutekeleza diplomasia ya kiuchumi ni wajibu wetu kama taifa kushirikiana na kutojitenga na mataifa mengine ikiwemo Marekani. Ni wazi kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo hazijasalimika na janga la UVIKO-19 ambalo limeathiri uchumi wa dunia. Hivyo iko haja ya kujumuika pamoja na mataifa mengine katika kutafuta suluhu ya kujikwamua kwenye madhara ya janga hili lakini pia kujipanga kwa pamoja ili magonjwa mengine ya milipuko ya aina hii yasiweze kuleta athari zaidi katika uchumi na jamii zetu hapo siku za usoni.

Kwa sababu hiyo, ziara ya Rais Samia nchini Marekani sio tu imempatia fursa ya kushiriki Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa kama Mwanadiplomasia wa kwanza na Mkuu wa Nchi bali pia itasaidia kuimarisha ushirikiano baina yetu na taifa rafiki la Marekani.

Kuongozana kwake na wafanyabiashara kutoka Tanzania na kushiriki kwenye mkutano wa pamoja baina yao na wenzao wa Marekani kumetoa mwanya kwa Rais Samia kuvutia uwekezaji na utalii nchini ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa letu.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Dunia (WB), ukuaji wa Pato Ghafi la Ndani (GDP) wa Tanzania ulishuka kufikia wastani wa asilimia mbili (2%) kwa mwaka 2020. Ambapo kushuka huku kwa ukuaji wa Pato Ghafi la Ndani (GDP) na kuathirika kwa mauzo ya biashara, utalii na usalama wa kifedha ulipelekea kuongezeka kwa idadi ya masikini takribani 600,000 mwaka 2020. Ukuaji wa uchumi umeshuka kutoka wastani wa asilimia saba (7%) kwa mwaka 2019 na 2018, na wastani wa asilimia 6.8 kipindi cha miaka mitano iliyopita hadi kufikia wastani wa asilimia tano (5%) kutokana na athari za UVIKO-19.

Kuongezeka kwa uwekezaji na utalii ambako kutachangiwa na ziara hii kutasaidia kuirejesha nchi kwenye mstari wa ukuaji wake wa kiuchumi na pato la taifa kwa ujumla. Hii itasaidia kuinua maendeleo ya wananchi na kukabiliana na janga la ajira ambalo limeongezeka kwa kasi tangu kuanza kwa ugonjwa wa UVIKO-19 duniani. Kwa mujibu wa Shirika la ILO, soko la ajira liliathirika kwa kiasi kikubwa. Kwa mwaka 2020 takribani ajira milioni 114 zilipotea duniani na Tanzania kwa kuwa ni sehemu ya dunia haikunusurika na athari hiyo.

Vikao vya pembezoni vya ana kwa ana alivyofanya Rais Samia na wakuu wa taasisi muhimu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres na Bw. David Malpass wa Benki Kuu ya Dunia (WB) pamoja na kile alichofanya na Mh.Charles Michael, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU), vilizaa matunda ambapo wamemuhakikishia kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kupambana na athari za UVIKO-19. Upande mwingine, Rais alikutana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand ukizingatia Tanzania imekuwa mwenyeji kwa wakimbizi kutoka nchi jirani kwa muda mrefu. Pia, kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Dkt. Ngozi Okonjo-Iweala nacho kilizaa matunda ambapo naye alimuhakikishia Rais Samia kuwa wataisaidia Tanzania kuweza kufikia malengo yake kibiashara.

Hivi karibuni Tanzania iliridhia mkataba wa soko huru barani Afrika (AfCFTA) ambao utatoa fursa ya nchi yetu kuuza bidhaa zake kwenye soko la ndani la Afrika linalokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani trilioni 3.4. Kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Marekani kwenye sekta muhimu ya viwanda na kilimo ambako kutatokana na ziara hii kutaisaidia nchi yetu kuwa na uwezo mkubwa wa ushindani wa kibiashara. Lakini pia, kutokana na Marekani kuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia kutasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitamudu ushindani katika soko huria na kupunguza kama si kulimaliza kabisa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi nchini.

Umuhimu wa Ushiriki wa Rais Samia Kwenye Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa

Kitendo cha Rais Samia kuhutubia Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa kunamfanya kuweka historia ya kuwa mwanamke wa tano kutoka barani Afrika kufanya hivyo kama Mkuu wa Nchi. Ajenda za mabadiliko ya tabia nchi, UVIKO-19, usalama wa nishati, chakula, usawa wa kijinsia, amani na usalama wa dunia ambazo kwa kiasi kikubwa zimebeba taswira ya mkutano huu ni muhimu sana sio tu Tanzania bali kwa bara la Afrika na dunia kwa ujumla. Hivyo basi, Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa inatoa muelekeo kwa viongozi wa mataifa mbalimbali duniani juu ya matamanio na matarajio ya watanzania.

Matarajio hayo ni pamoja na kufikia Malengo Endelevu ya Dunia na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika ambazo utekelezaji wake umeathirika kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO-19. Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza kwamba hatuwezi kutumia UVIKO-19 kama kisingizio cha kutofanya jitihada za kutosha kufikia Malengo Endelevu. Kauli hii sio tu imedhihirisha utayari wetu kama taifa kwenye kufikia ajenda za maendeleo lakini pia inatoa hamasa kwa wadau na washirika wetu wa kimaendeleo ulimwenguni kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuyafikia Maendeleo Endelevu licha ya changamoto na madhara yaliyotokana na UVIKO-19.

Msisitizo wa Rais Samia wa kuimarisha na kudumisha ushirikiano wa kimataifa katika hotuba yake umetoa picha kwa mataifa rafiki kuwa tuko tayari kama taifa kuendelea kushirikiana nao kwenye ajenda zote muhimu zenye maslahi ya pamoja. Na kama alivyonukuu methali ya kiafrika katika hotuba yake inayosema, “ukitaka kwenda haraka nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako.” Kauli hii imedhihirisha wazi kuwa Tanzania haitajitenga na jumuiya za kimataifa katika jitihada za pamoja za kupata maendeleo bali itashirikiana nao kama wadau muhimu ili kuweza kuipaisha nchi katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa ujumla.

Mwisho, kugusia kwake masuala ya usawa wa kijinsia ambao yeye mwenyewe ameonesha kwa vitendo kwa kuteua wanawake wengi kwenye nafasi mbalimbali zikiwemo wizara nyeti za Ulinzi na Mambo ya Nje kumeitangazia dunia utayari wa Tanzania kulifikia lengo la tano la Maendeleo Endelevu linalojikita kwenye usawa kijinsia. Masuala mengine kama athari za mabadiliko ya tabia nchi, maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya vijana ambayo yalibeba ujumbe wa hotuba yake yametoa mwanga wa vipaumbele vya serikali yake katika kuboresha maisha ya watanzania. Pia yametoa fursa kwa nchi wahisani kupata picha halisi ya maeneo gani washikirikiane nasi ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo.
20210926_114348.jpg
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,124
2,000
Kutokufahamu Lugha ya Kiingereza kwa Marehemu Mwendazake na aina ya teuzi za wajamaa wasiokuwa wazoefu katika diplomasia,uchumi na uongozi kama kina kabudi, Bashiru,Polepole,Bashite,Ndumbaro, n.k kulifanya Taifa lifanye vibaya katika diplomasia na badala yake tukaanza mapambano na Dunia fikirika'
 
Ndombwindo

JF-Expert Member
Nov 23, 2013
664
1,000
Maelezo mengi lakina hakuna hoja ya msingi, mahusiano ya kidiplomasia yanayotaka mataifa fulani pekee kujikomba upande mwingine ndio mnayaita mahusiano sahihi!

Raisi wa USA au Ufaransa akipanga safari yake kuja Africa anaweza kuishia kwenye nchi mbili au tatu tu, cha ajabu na kushangaza ni pale nchi zote 50 na zaidi zilizopo Africa maraisi wake wanataka kwenda Ufaransa au USA, ikibidi hata mara tatu au nne katika mwaka.

Cha kushangaza zaidi, watu wanawasahau wanadiplomasia chungu nzima waliopo kwenye mabalozi duniani kote, wanataka mpaka Raisi aende yeye mwenyewe physically, kwa wenzetu sasa, ukiona manyoya ujue tayari kaliwa nikimaanisha kwamba, ukimuona Obama, Blair au Bush kaja Tanzania tena akiwa madarakani ujue ndio basi tena, kumbuka huwa tunawaondoa mpaka viwete na kudeki lami kwa maana ya kuonyesha hatuna shida (kwa ziara za hapa ndani za raisi ni sawa na kuyakataa mabango yasionyeshwe) ili wakiondoka na dhahabu kama zawadi wasijisikie wanyonge maana wakiona uhalisia ni kama vile kumtembelea mgonjwa baadae unapewa wewe uji wake unywe.

Diplomasia ya maana sana na yakufanyiwa kazi na nchi zetu ni ya EAC, AU, SADC, ECCOWAS n.k. Iwe kama vile wenzetu wanavyo pambania EU, UK, NATO n.k, ndio baadae na sisi sasa tufikilie kujihusisha UN, USA, UK kwa ukaribu baada ya kuwa vizuri nyumbani kidiplomasia. Kumbuka hata adui yeyote akitaka kukuangusha hutumia majirani na mifano mizuri ipo Middle na far East kwenye vita za Iran, Iraq, Kuwait na Korea, Japan, China respectively.
 
Kichwa maji kabisa wewe, unaweza kweli kuongea kiingereza cha kabudi wewe? Unaweza fikia level ya kuaminiwa na kupewa ukufunzi wa chuo hata cha VETA mpaka kufikia kujifananisha na Polepole, Bashiru na Kabudi?

Uandishi tu wa Kiswahili umekushinda unaandika bila kupangilia mada kwa paragraph, kuweka nukta mwisho wa sentensi, kuruka nafasi baada ya alama ya mkato na vitu vidogo kama hivyo ndio uje kuhoji wenye PHD zao na maprofesa! 🤣🤣🤣🤣 Ama hakika wahenga walisema nyani haoni kundule. Mitano tena kwa wahenga.
 
ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
2,996
2,000
SAFARI YA KWANZA YA RAIS SAMIA NJE YA BARA LA AFRIKA: NINI MANUFAA YAKE KWA NCHI?

Imeandikwa na Seleman Kitenge na Mhandisi Fatma Rembo

Umuhimu wa Diplomasia kwa Mustakabali wa Taifa

Ulimwenguni kote hakuna nchi ama taifa lolote iwe lililoendelea au linaloendelea ambalo limejitosheleza kwa mahitaji yake yote ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na hata ya ulinzi na usalama wa raia na mipaka yake bila kutegemea mataifa mengine. Ushirikiano baina ya nchi hutoa fursa kwa nchi husika kushirikiana katika kushughulikia changamoto au hatari mbalimbali zinazoweza kuhatarisha uhai wa mataifa hayo.

Mahusiano ya kidiplomasia ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazoyakumba mataifa mbalimbali duniani. Changamoto hizo ni kama vile magonjwa ya milipuko, mabadiliko ya tabia nchi, uhaba wa nishati, uhaba wa chakula na maji, ugaidi, uhamiaji haramu, utoroshwaji wa fedha haramu nje ya nchi, uhalifu wa kuvuka mipaka na migogoro mbalimbali inayohatarisha amani na usalama wa dunia.

Lakini pia, diplomasia haishii tu kwenye ushirikiano wa kutatua changamoto ambazo zinahatarisha maslahi ya pamoja baina ya nchi bali inakwenda mbali zaidi katika kuhakikisha nchi zinapata mahitaji yake muhimu. Mahitaji hayo yanaweza kupatikana kupitia biashara za kimataifa, kubadilishana taarifa na maarifa, misaada ya kisayansi na teknolojia, pamoja na misaada ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwa mantiki hiyo, pasipo kuwepo na urafiki na ushirikiano wa uhakika baina ya mataifa si tu itakuwa ngumu kwa nchi kukidhi mahitaji yake bali pia itajihatarishia usalama na nafasi yake kwenye majukwaa ya kimataifa ya utoaji maamuzi juu ya ajenda mbalimbali za maendeleo ya dunia.

Kama ilivyo kwenye familia udugu huimarishwa kwa kutembeleana na kujuliana hali, hivyo hivyo kwenye nyanja ya diplomasia kutembeleana huongeza uhai wa ushirikiano na urafiki baina ya mataifa.

Umuhimu wa Ziara ya Rais Samia Marekani

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya mabadiliko katika sera yake ya awali ya mambo ya nje ambayo ilijikita zaidi kwenye ukombozi wa uhuru wa kisiasa wa bara la Afrika ili kujikita kwenye ukombozi wa kiuchumi. Ni wazi kwamba nguvu ya kiuchumi sio tu inatuhakikishia usalama wa kisiasa, kijeshi na kijamii ila inatupa fursa pia ya kuweza kulinda tunu na maslahi ya taifa letu kwenye dunia yenye ushindani mkubwa.

Hivyo basi, Rais Samia Suluhu Hassan ametambua fika ili tuweze kufikia dhana ya nchi yetu ya kutekeleza diplomasia ya kiuchumi ni wajibu wetu kama taifa kushirikiana na kutojitenga na mataifa mengine ikiwemo Marekani. Ni wazi kuwa nchi yetu ni miongoni mwa nchi ambazo hazijasalimika na janga la UVIKO-19 ambalo limeathiri uchumi wa dunia. Hivyo iko haja ya kujumuika pamoja na mataifa mengine katika kutafuta suluhu ya kujikwamua kwenye madhara ya janga hili lakini pia kujipanga kwa pamoja ili magonjwa mengine ya milipuko ya aina hii yasiweze kuleta athari zaidi katika uchumi na jamii zetu hapo siku za usoni.

Kwa sababu hiyo, ziara ya Rais Samia nchini Marekani sio tu imempatia fursa ya kushiriki Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa kama Mwanadiplomasia wa kwanza na Mkuu wa Nchi bali pia itasaidia kuimarisha ushirikiano baina yetu na taifa rafiki la Marekani.

Kuongozana kwake na wafanyabiashara kutoka Tanzania na kushiriki kwenye mkutano wa pamoja baina yao na wenzao wa Marekani kumetoa mwanya kwa Rais Samia kuvutia uwekezaji na utalii nchini ambao ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa letu.

Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Dunia (WB), ukuaji wa Pato Ghafi la Ndani (GDP) wa Tanzania ulishuka kufikia wastani wa asilimia mbili (2%) kwa mwaka 2020. Ambapo kushuka huku kwa ukuaji wa Pato Ghafi la Ndani (GDP) na kuathirika kwa mauzo ya biashara, utalii na usalama wa kifedha ulipelekea kuongezeka kwa idadi ya masikini takribani 600,000 mwaka 2020. Ukuaji wa uchumi umeshuka kutoka wastani wa asilimia saba (7%) kwa mwaka 2019 na 2018, na wastani wa asilimia 6.8 kipindi cha miaka mitano iliyopita hadi kufikia wastani wa asilimia tano (5%) kutokana na athari za UVIKO-19.

Kuongezeka kwa uwekezaji na utalii ambako kutachangiwa na ziara hii kutasaidia kuirejesha nchi kwenye mstari wa ukuaji wake wa kiuchumi na pato la taifa kwa ujumla. Hii itasaidia kuinua maendeleo ya wananchi na kukabiliana na janga la ajira ambalo limeongezeka kwa kasi tangu kuanza kwa ugonjwa wa UVIKO-19 duniani. Kwa mujibu wa Shirika la ILO, soko la ajira liliathirika kwa kiasi kikubwa. Kwa mwaka 2020 takribani ajira milioni 114 zilipotea duniani na Tanzania kwa kuwa ni sehemu ya dunia haikunusurika na athari hiyo.

Vikao vya pembezoni vya ana kwa ana alivyofanya Rais Samia na wakuu wa taasisi muhimu kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres na Bw. David Malpass wa Benki Kuu ya Dunia (WB) pamoja na kile alichofanya na Mh.Charles Michael, Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU), vilizaa matunda ambapo wamemuhakikishia kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kupambana na athari za UVIKO-19. Upande mwingine, Rais alikutana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bw. Filippo Grand ukizingatia Tanzania imekuwa mwenyeji kwa wakimbizi kutoka nchi jirani kwa muda mrefu. Pia, kikao chake na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), Dkt. Ngozi Okonjo-Iweala nacho kilizaa matunda ambapo naye alimuhakikishia Rais Samia kuwa wataisaidia Tanzania kuweza kufikia malengo yake kibiashara.

Hivi karibuni Tanzania iliridhia mkataba wa soko huru barani Afrika (AfCFTA) ambao utatoa fursa ya nchi yetu kuuza bidhaa zake kwenye soko la ndani la Afrika linalokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani trilioni 3.4. Kuongezeka kwa uwekezaji kutoka Marekani kwenye sekta muhimu ya viwanda na kilimo ambako kutatokana na ziara hii kutaisaidia nchi yetu kuwa na uwezo mkubwa wa ushindani wa kibiashara. Lakini pia, kutokana na Marekani kuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia kutasaidia kuzalisha bidhaa zenye ubora ambazo zitamudu ushindani katika soko huria na kupunguza kama si kulimaliza kabisa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi nchini.

Umuhimu wa Ushiriki wa Rais Samia Kwenye Mkutano Mkuu wa 76 wa Umoja wa Mataifa

Kitendo cha Rais Samia kuhutubia Mkutano Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa kunamfanya kuweka historia ya kuwa mwanamke wa tano kutoka barani Afrika kufanya hivyo kama Mkuu wa Nchi. Ajenda za mabadiliko ya tabia nchi, UVIKO-19, usalama wa nishati, chakula, usawa wa kijinsia, amani na usalama wa dunia ambazo kwa kiasi kikubwa zimebeba taswira ya mkutano huu ni muhimu sana sio tu Tanzania bali kwa bara la Afrika na dunia kwa ujumla. Hivyo basi, Hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa inatoa muelekeo kwa viongozi wa mataifa mbalimbali duniani juu ya matamanio na matarajio ya watanzania.

Matarajio hayo ni pamoja na kufikia Malengo Endelevu ya Dunia na Ajenda ya Maendeleo ya Afrika ambazo utekelezaji wake umeathirika kwa kiasi kikubwa na janga la UVIKO-19. Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza kwamba hatuwezi kutumia UVIKO-19 kama kisingizio cha kutofanya jitihada za kutosha kufikia Malengo Endelevu. Kauli hii sio tu imedhihirisha utayari wetu kama taifa kwenye kufikia ajenda za maendeleo lakini pia inatoa hamasa kwa wadau na washirika wetu wa kimaendeleo ulimwenguni kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuyafikia Maendeleo Endelevu licha ya changamoto na madhara yaliyotokana na UVIKO-19.

Msisitizo wa Rais Samia wa kuimarisha na kudumisha ushirikiano wa kimataifa katika hotuba yake umetoa picha kwa mataifa rafiki kuwa tuko tayari kama taifa kuendelea kushirikiana nao kwenye ajenda zote muhimu zenye maslahi ya pamoja. Na kama alivyonukuu methali ya kiafrika katika hotuba yake inayosema, “ukitaka kwenda haraka nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali nenda na wenzako.” Kauli hii imedhihirisha wazi kuwa Tanzania haitajitenga na jumuiya za kimataifa katika jitihada za pamoja za kupata maendeleo bali itashirikiana nao kama wadau muhimu ili kuweza kuipaisha nchi katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa ujumla.

Mwisho, kugusia kwake masuala ya usawa wa kijinsia ambao yeye mwenyewe ameonesha kwa vitendo kwa kuteua wanawake wengi kwenye nafasi mbalimbali zikiwemo wizara nyeti za Ulinzi na Mambo ya Nje kumeitangazia dunia utayari wa Tanzania kulifikia lengo la tano la Maendeleo Endelevu linalojikita kwenye usawa kijinsia. Masuala mengine kama athari za mabadiliko ya tabia nchi, maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya vijana ambayo yalibeba ujumbe wa hotuba yake yametoa mwanga wa vipaumbele vya serikali yake katika kuboresha maisha ya watanzania. Pia yametoa fursa kwa nchi wahisani kupata picha halisi ya maeneo gani washikirikiane nasi ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo. View attachment 1953517
Ukichambua safari ya kwanza ya Rais Samia nje ya Tanzania hata kama ni ndani ya Afrika basi manufaa yake ni mfanano tu. Yawe yasiwe. Afrika sio nchi na hatuna muunganiko wowote kiuchumi na kisiasa ulio rasmi. It is only boarders.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,411
2,000
Maelezo mengi lakina hakuna hoja ya msingi, mahusiano ya kidiplomasia yanayotaka mataifa fulani pekee kujikomba upande mwingine ndio mnayaita mahusiano sahihi!

Raisi wa USA au Ufaransa akipanga safari yake kuja Africa anaweza kuishia kwenye nchi mbili au tatu tu, cha ajabu na kushangaza ni pale nchi zote 50 na zaidi zilizopo Africa maraisi wake wanataka kwenda Ufaransa au USA, ikibidi hata mara tatu au nne katika mwaka.

Cha kushangaza zaidi, watu wanawasahau wanadiplomasia chungu nzima waliopo kwenye mabalozi duniani kote, wanataka mpaka Raisi aende yeye mwenyewe physically, kwa wenzetu sasa, ukiona manyoya ujue tayari kaliwa nikimaanisha kwamba, ukimuona Obama, Blair au Bush kaja Tanzania tena akiwa madarakani ujue ndio basi tena, kumbuka huwa tunawaondoa mpaka viwete na kudeki lami kwa maana ya kuonyesha hatuna shida (kwa ziara za hapa ndani za raisi ni sawa na kuyakataa mabango yasionyeshwe) ili wakiondoka na dhahabu kama zawadi wasijisikie wanyonge maana wakiona uhalisia ni kama vile kumtembelea mgonjwa baadae unapewa wewe uji wake unywe.

Diplomasia ya maana sana na yakufanyiwa kazi na nchi zetu ni ya EAC, AU, SADC, ECCOWAS n.k. Iwe kama vile wenzetu wanavyo pambania EU, UK, NATO n.k, ndio baadae na sisi sasa tufikilie kujihusisha UN, USA, UK kwa ukaribu baada ya kuwa vizuri nyumbani.

Nimependa hoja zako ulizojibu za bandiko kuu.

Demokrasia ya Uchumi haina maana kama hatuna cha kubadilishana na wengine, hasa mataifa yaliyoendelea, zaidi ya kutembeza bakuli la misaada.

Kimsingi hotuba ya Rais SSH ilikuwa yenye lugha ya ombaomba. Ameonesha tofauti kubwa na mtangulizi wake ambaye alihimiza kujitegemea kama alivyostaka Baba wa Taifa katika falsafa yake ya Ujamaa na Kujitegemea (yaani, kwa pamoja tujenge nchi).
 
Ni kweli kabisa mkuu, imagine kwenye hotuba yake neno Covid 19 limejirudia zaidi ya mara kumi kana kwamba Tanzania hatuna matatizo mengine, au kabla ya Covid basi nchi yetu ilikuwa kama Dubai.

Nchi hii inarasilimali nyingi na ni tajiri kwa hilo, histori yenyewe inajieleza, scarcity ya raw materials ulaya ndio chanzo cha wao kuja Africa kutawala maeneo yetu hapo awali, leo mama anashindwa kutumia utajiri huo kwenda kifua mbele kutafuta mahusiano yanayoweza kutufaa pande zote mbili kwa usawa badala yake anaenda kulia lia.

Hiyo sio diplomasia, zaidi zaidi naweza sema ameamua kuburuzwa, na kuburuzwa kwake ni mzigo kwa taifa zima, hilo hataki kuliona.
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
6,124
2,000
Kichwa maji kabisa wewe, unaweza kweli kuongea kiingereza cha kabudi wewe? Unaweza fikia level ya kuaminiwa na kupewa ukufunzi wa chuo hata cha VETA mpaka kufikia kujifananisha na Polepole, Bashiru na Kabudi?

Uandishi tu wa Kiswahili umekushinda unaandika bila kupangilia mada kwa paragraph, kuweka nukta mwisho wa sentensi, kuruka nafasi baada ya alama ya mkato na vitu vidogo kama hivyo ndio uje kuhoji wenye PHD zao na maprofesa! 🤣🤣🤣🤣 Ama hakika wahenga walisema nyani haoni kundule. Mitano tena kwa wahenga.
Braza,

Ndugu, hao watu nimeanza kuwafahamu hata kabla ya Magufuli kuwaleta kwenye siasa. Bashiru amenifundisha miaka 2, najua misimamo yake ya siasa za kijamaa. Ni Mwalimu mzuri wa Siasa na utawala (Political science and Public Administration) lakini siasa na uongozi hajui.

Ndumbaro namfahamu vizuri toka yupo TAZARA. Huyo Pole pole alishawahi kutapeli fedha za semina kipindi hiko anajishughulisha na asasi za kijamii, ni mweupe kichwani. Anakula kwa mdomo. Kabudi alikuwa Mshereheshaji kwenye hafla,makongamano na sherehe za UDSM. Kiingereza chake cha kawaida sana. Wote hawana uzoefu katika uongozi na siasa. Endelea kuhakiki maandiko ya watu (eti hapo ndio unapima elimu na akili ya mtu!)
 
Wewe unawazimu, unajichanganya mwenyewe kwenye maelezo yako.

Mosi, unasema kwamba Bashiru ameletwa kwenye siasa na magufuli at the same time unasema amekufundisha chuo na unaijua misimamo yake kisiasa, which is which? Hiyo misimamo na hiyo elimu yake ya siasa haitishi kumfanya mwanasiasa mpaka umuone jukwaani?

Pili, unataka kumdanganya nani? na kwa faida ya nani? Polepole kweli kaletwa kwenye siasa na Magufuli! Umemaliza chuo? Inawezekana bado upo chuoni mwaka wa kwanza maana binafsi polepole nimemuona kwenye medani za siasa kabla hata ya Magufuli kuwa Raisi awamu yake ya kwanza.

Kuhusu hoja yako ya kutapeli na vitu kama hivyo nilitegemea ungeweka ushahidi wa vielelezo badala ya kuleta mali kauli ingali ukijitanabaisha kuwa msomi tena wa ngazi ya chuo kikuu. By the way, criteria gani umetumia kuhitimisha kuwa Bashiru ni mwalimu nzuri wa Political Science and Public Administration lakini sio kiongozi mzuri? Nasubiri ushahidi wa hoja.

Ushauri wangu wa bure kwako, kama huwezi kuandika lugha ya kiswahili kwa kufuata sheria Zake ndogo ndogo usithubutu kukosoa vitu vikubwa na vizito usivyoviweza maana imeandikwa, wa moja havai mbili.
 
...
 
Felix

JF-Expert Member
Mar 9, 2014
797
1,000
Maelezo mengi lakina hakuna hoja ya msingi, mahusiano ya kidiplomasia yanayotaka mataifa fulani pekee kujikomba upande mwingine ndio mnayaita mahusiano sahihi!

Raisi wa USA au Ufaransa akipanga safari yake kuja Africa anaweza kuishia kwenye nchi mbili au tatu tu, cha ajabu na kushangaza ni pale nchi zote 50 na zaidi zilizopo Africa maraisi wake wanataka kwenda Ufaransa au USA, ikibidi hata mara tatu au nne katika mwaka.

Cha kushangaza zaidi, watu wanawasahau wanadiplomasia chungu nzima waliopo kwenye mabalozi duniani kote, wanataka mpaka Raisi aende yeye mwenyewe physically, kwa wenzetu sasa, ukiona manyoya ujue tayari kaliwa nikimaanisha kwamba, ukimuona Obama, Blair au Bush kaja Tanzania tena akiwa madarakani ujue ndio basi tena, kumbuka huwa tunawaondoa mpaka viwete na kudeki lami kwa maana ya kuonyesha hatuna shida (kwa ziara za hapa ndani za raisi ni sawa na kuyakataa mabango yasionyeshwe) ili wakiondoka na dhahabu kama zawadi wasijisikie wanyonge maana wakiona uhalisia ni kama vile kumtembelea mgonjwa baadae unapewa wewe uji wake unywe.

Diplomasia ya maana sana na yakufanyiwa kazi na nchi zetu ni ya EAC, AU, SADC, ECCOWAS n.k. Iwe kama vile wenzetu wanavyo pambania EU, UK, NATO n.k, ndio baadae na sisi sasa tufikilie kujihusisha UN, USA, UK kwa ukaribu baada ya kuwa vizuri nyumbani kidiplomasia. Kumbuka hata adui yeyote akitaka kukuangusha hutumia majirani na mifano mizuri ipo Middle na far East kwenye vita za Iran, Iraq, Kuwait na Korea, Japan, China respectively.
Mtoa mada ameuliza swali arafu amejijibu mwenyewe. Kwa kumuongezea majibu yake, safar hii Ina manufaa kwamba

1. Mkuu amekutana na mapokez mazur ya heshma akiwemo mangi kimambi

2.Marais wote walio kuwemo kwenye ukumbi, wamegundua Tanzania tulifiwa na magufuri kupitia hotuba yake na hivyo wametuonea huruma....

3.kupitia hotuba yake, dunia imejua kuwa Tanzania Haina wataalam wa afya wenye kutengeneza chanjo zetu, hivyo ameomba tupewe nyongeza ya chanjo ya nje siku zote

4. Safar yake, baada ya rais wa Zambia kupokelewa Ikulu ya marekan, yeye mpaka amerud Ikulu ya Biden hakuingia. So amejifunza na ss tumejifunza kitu jins wamerekan na dunia wanavyo tuchukulia...

5. Makamo wake amesema alipo achiwa nchi aliogopa Sana. Hivyo mkuu amegundua kwamba makamo kumbe mwogaaaaa. Akiwa rais lasm arafu Gaid waliyemkamata ...., Akitishia tu, mzee BP inaweza kumpanda n.k

So faida ziko nyingi tumemuonzea mtoa mada
 
Hahahahaha hiyo namba mbili umeua kabisa mkuu ukiachilia ya Mange na hizo nyinginezo, yaani hicho kitu kimenikera sana hata mimi, mpaka saizi tunaenda kuumaliza mwaka bado raisi anatoa salamu za rambirambi za msiba wa mwezi wa tatu! Aisee!

wenyewe watakuambia protocol, ilhali mwendazake mwenyewe ndio kwanza hakuwa hata na shobo na hivyo vikao. Tena nahisi angemaliza ten years bila kuhudhuria wakaona wamkatishe safari ya matumaini ya kweli.
 
Ndo vizuri jaman tuonewe huruma..Ila tu amejitahidi Kaz iendeleeeeee
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,719
2,000
Tatizo upinzani nao hawajitambui...
Huu ugomvi wa ndani kwenye kuta za ccm ungewanufaisha sana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom