Safari ya kujiburudisha mjini Qingdao,CHina

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
Watu wengi duniani wameshuhudia mvuto wa Qingdao kutokana na mji huo kuandaa michezo ya mashua yenye matanga mjini humo wakati wa michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008. Baada ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya Beijing, katika mji huo unaojulikana kwa utalii, zimeongezeka shughuli za utalii za aina mbalimbali pamoja na kutembelea viwanja na majumba ya michezo ya Olimpiki, kupanda mashua yenye matanga na kufanya matembezi kwenye sehemu isiyo na watu ya kisiwani, ambazo zinapendwa na watu wengi. Katika siku za majira ya joto, kucheza kwenye maji ya pwani ya Qingdao ni chaguo zuri.
Kituo cha mashua yenye matanga cha Qingdao kilikuwa ni moja kati ya viwanja na majumba muhimu ya michezo ya Olimpiki, na kinajulikana sana nchini na nje kutokana na kufanyika kwa michezo ya mashua yenye matanga ya michezo ya Olimpiki ya mwaka 2008. Hivi sasa kituo hicho kimefungua mlango kwa watu na kutembelewa na watu wengi zaidi ikilinganishwa na sehemu nyingine za utalii mjini Qingdao.
5144057.jpg

Baada ya kutembelea kituo hicho, watu wanaweza kupanda kwenye meli au mashua kubwa zenye matanga kuona hali ya kufurahisha kwenye bahari, au kutembelea kwenye sehemu isiyo na watu kwenye kisiwa, au kuvua samaki kwa ndoano baharini, ambapo watu wataburudika sana na kupata kupumzika vizuri.
Hivi sasa, klabu ya michezo ya boti ya kimataifa ya Qingdao inafanya juhudi kutayarisha "utalii wa siku moja kwenye kisiwa", baada ya siku chache watu wataweza kufanya matembezi kwenye kisiwa cha Dagong na kisiwa cha Zhucha, meneja mkuu wa klabu hiyo, Bw. Dong Yongquan alisema:"Hivi sasa tunaendeleza utalii wa matembezi kwenye kisiwa, hizi ni shughuli za kushiriki kufurahia mazingira ya kimaumbile, kwa hatua ya mwanzo tunawasafirisha watalii kwa safari nne kwa siku, tunakadiria kuwa matumizi ya kila mtu ni chini ya Yuan za Renminbi 100." Gharama ya usafirishaji ya Yuan 100 inawawezesha watu wengi waimudu, klabu hiyo itajitahidi kufanya shughuli za kukamata samaki kwa ndoano baharini za kuvutia zaidi, ili kuongeza mvuto wa utalii wa baharini. Watu wanaopenda mashua yenye matanga, wataweza kusafiri baharini wao wenyewe baada ya kupewa mafunzo rahisi.

Kwa watalii wanaopenda mambo mapya, wanavutiwa sana na basi linaloitwa "bata wa kubahatisha", ambalo linaweza kusafiri ardhini na majini. Kwenye bahari karibu na kituo cha mashua yenye matanga cha Olimpiki, basi hilo linalofanana na umbo la bata, mara linakwenda kwenye ufukwe, mara linaingia baharini kwa kasi, mtu akitumia Yuan 120 anaweza kujisikia mashtuko na furaha kwenye bahari kwa dakika 45, na kuona mandhari nzuri ya pwani kutoka baharini. Meneja wa mauzo wa kampuni ya utalii ya Shengshi ya Qingdao Bi. Nan Nan alisema: "Safari nzima ni dakika 45 hivi, watalii wanaweza kuona mabadiliko ya safari ya ardhini na majini, vilevile wanaweza kuona mandhari ya mji mzima wa Qingdao."
56.gif

Michezo ya mashua yenye matanga iliyofanyika mjini Qingdao inaufanya mji huo uwe mji maarufu duniani siku hadi siku, watalii wengi wanatembelea mji wa Qingdao kwa kuvutiwa na sifa zake. Baada ya kutembelea viwanja na majumba ya michezo ya Olimpiki vya kisasa na kufurahishwa na utalii wa baharini, watalii wanaweza kuburudika kwa chakula kitamu cha sehemu ya Qingdao. Chakula maarufu zaidi cha Qingdao ni bia na chakula cha baharini, watu wakitaka kunywa bia ya asili ya Qingdao na kula chaza waliokaangwa kwa mafuta na pilipili, hawana budi kufika kwenye mtaa wa bia wa Qingdao. Kila siku giza linapoingia, mtaa wa bia ulioko kwenye barabara ya Dengzhou ya mjini Qingdao huwa na pilikapilika zaidi, mikahawa yote ya mtaa huo hujaa wateja wanaovutiwa na utamaduni wa bia wa zaidi ya miaka mia moja na mila na desturi za huko, ambapo wanaburudishwa na bia iliyotoka kiwandani siku ile ile. Bw. Zhang ni mwenyeji wa Qingdao, yeye na marafiki zake wanakutana huko mara kwa mara. Alisema: "mawasiliano ya hapa ni rahisi, bia na vitoweo vya hapa ni vizuri na bei zake ni nafuu, tena mazingira ya hapa ni mazuri sana, sisi tunafurahi sana kukutana hapa".

Kuhusu shughuli motomoto za biashara kwenye mtaa wa bia wa Qingdao, mkurugenzi wa usimamizi wa mtaa huu Bw. Cheng Jun alisema: "Mtaa wa bia ni mahali kilipo kiwanda cha bia cha Qingdao chenye historia ya miaka mia moja, wakazi wa Qingdao wana hisia nyingi maalum juu ya mtaa wa bia, kwa wakazi wa Qingdao, mtaa wa bia ni kama nyumbani, ambapo watalii kutoka sehemu nyingine wanaweza kuona hali ya kuungana kwa historia na mambo ya kisasa."
Baada ya kunywa bia na kula kitoweo cha chaza kwenye mtaa wa bia, watu wanaweza kwenda kutembelea sehemu mpya iitwayo "Mji wa Tianmu", ambayo ilijengwa kwenye eneo lililojengwa kiwanda hapo zamani, katika sehemu hiyo watu wanaweza kuona vivutio vingi, michezo ya sanaa na kupumzika. Watalii wanaweza kuona mandhari nzuri ya anga ya buluu, mawingu meupe, mbalamwezi na nyota zinazometameta wakati wa usiku pamoja na majengo mengi yenye mitindo ya nchi mbalimbali.
57.gif

Shughuli zilizoendelezwa baada ya michezo ya Olimpiki zimeongeza uhai kwa shughuli za utalii mjini Qingdao na kuvutia watalii wengi kutoka sehemu nyingine. Kwa wakazi wa mji wa Qingdao, licha ya kupata urahisi katika utalii, wameanzisha harakati kubwa ya kuimarisha afya kutokana na ushawishi wa michezo ya Olimpiki na michezo ya taifa ya China, hivi sasa mji wa utalii wa Qingdao umekuwa na mazingira bora ya mapumziko. Kituo cha michezo cha Qingdao, ambacho kilikuwa mahali pa kufanyika michezo ya kuteleza kwenye barafu katika michezo ya 11 ya taifa ya mwaka 2009, sasa kimefunguliwa kwa watu wote, uwanja wa barafu iliyotengenezwa unavutia idadi kubwa ya wakazi wa Qingdao, katika asubuhi ya siku moja kiasi cha watu 500 wamepata uzoefu wa kucheza michezo kwenye barafu ya kweli. Mkazi Bw. Li alisema: "Tunafurahi sana kuweko kwa uwanja wa barafu mjini Qingdao, tunaweza kuwaleta watoto kuja kucheza michezo na kuimarisha afya zetu." Michezo ya aina mbili za mbio ya kuteleza kwenye barafu na wachezaji wanateleza kwenye barafu huku wakifanya miondoko mbalimbali, imewavutia watu wengi ambao sasa wamekuwa mashabiki wa michezo ya kuteleza kwenye barafu. Tunaamini kuwa Qingdao itawaonesha watu wa dunia kwa sifa zake za "mji mkuu wa mashua yenye matanga na Qingdao wenye mvuto"
 
Back
Top Bottom