Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani?

Ndo shida ya kushindia kipande cha muhogo mbichi!!! unajitungia tu maneno.
huoni kama kitendo cha mtu kushindia muhogo mbichi ni kwa sababu ya maisha magumu ambayo ccm imewasababishia watanzania? unafurah mtu kushindia muhogo ili hali mnaendelea kuitafuna nchi na kuwaacha asilimia kubwa ya watz hoi?
 
huoni kama kitendo cha mtu kushindia muhogo mbichi ni kwa sababu ya maisha magumu ambayo ccm imewasababishia watanzania? unafurah mtu kushindia muhogo ili hali mnaendelea kuitafuna nchi na kuwaacha asilimia kubwa ya watz hoi?

Mkuu Waache waendelee Kufurahia Baga na Piza on the expense ya sisi kushindia Vipande vya Mihogo. Mwisho wao u karibu
 
Nape tueleze, je wewe ni mtoto wa kigogo wa CCM mwenye mtambo wa sms-proofing, mana baada tu ya Marando kufunguka huku mtajwa akiwa motto wa kigogo (na sio CCM) wewe kama kawaida yako ukakurupuka,
 
Nape tueleze, je wewe ni mtoto wa kigogo wa CCM mwenye mtambo wa sms-proofing, mana baada tu ya Marando kufunguka huku mtajwa akiwa motto wa kigogo (na sio CCM) wewe kama kawaida yako ukakurupuka, sisi tunaoshindia mihigo mibichi nani mtetezi wetu, maana katibu mwenezi anatukejeli
 
Kombajr,
KUANDIKWA NA KUWEPO KWENYE AKILI ZA WATU HAKUMAANISHI TUMESEMA. HEBU MWENYE USHAHIDI WA HAYA MANENO KUTOKA KWENYE KINYWA CHA HAO ULIOWATAJA AWEKE HAPA ILI TUMKOME NYANI HADHARANI

Nape hata yale mnayoyasema mkishindwa kutekeleza mnayakana?Unataka udhibitisho wa namna gani?wananchi wawamini kwa lipi?
 
Nnauye Jr Kwa Nini Kila anapohusika Mwigulu Nchemba Mauaji kwa Makada wa Vyama Vya Upinzani au Ugomvi ni Lazima Utokee? Tumeona Igunga, Tumeona Arumeru Mashariki je Hizi ndio Mbinu mnazotumia sasa kuwatisha Wapinzani wenu? Jamani hii damu ya watanzania ina Thamni kubwa acheni Kuimwaga kama Mnamwaga Mbege au Wanzuki au Gongo
 
Last edited by a moderator:
Bashemere,
Kwanza nikushukuru kwa ustaarabu mkubwa katika kutoa hoja! Hili linatoa nafasi ya kujadili hoja badala ya kejeli na matusi!naahidi kushirikiana na wote watakao kuja kwa hoja kuzijibu moja baada ya nyingine! Sitajishughulisha na kejeli na matusi!

Niweke wazi kuwa msimamo wangu dhidi ya ufisadi na rushwa (ambao kwakweli ni matumizi mabaya ya rasilimali)BADO UKO PALEPALE, NA SITAYUMBA KATIKA HILI!

Nape tumechoka kusubiri siku 90, ukasema mpaka kikao cha NEC bila mafanikio je NEC bado haijakaa mpaka Leo? Kama bado je kitakaa lini? Na Kama tayari maamuzi ni yapi?


Ulituahidi hivi nanukuu hapa chini.


By Nnauye Jr
Nimeamua kuja mwenyewe. Nashangaa wakati mwingine maana ni hapa ndo watu walisema Nape kashazibwa mdomo kama vile yale ni maamuzi ya Nape binafsi.
Jana nimewakumbusha tu watuhumiwa na wapambe wao si busara kujifariji kuwa maamuzi yatabadilishwa nje ya vikao, na vikao vyenyewe ni lazima iwe ama NEC au Mkutano Mkuu(Congres) na si vinginevyo.
Kuna hoja hapa eti kwamba Nape anabwabwaja tu, hakuna vitendo, let's be objective,hivyo vitendo ni vipi? Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi haya itatolewa kwenye kikao kijacho cha NEC na si siku 90 kama wanavyojaribu kueleza hapa. Tumelieleza sana hili la siku,WAANDISHI TENA BAADHI ndo walitafsiri siku tisini kutoka kwenye ratiba ya vikao vya NEC ambavyo Dodoma tulikubaliana tentively tunaweza kukutana July ndo wakahesabu na kusema siku tisini. Lakini hakuna kikao kinakutana exactly kwa muda ulopangwa,kuna flexibility.
Ushauri subirini NEC ikutane mtuseme tukishindwa kufukuza.
 
Nape ameishakula kona , maswali yamelenga ukweli zairi, albedo punguza maswali umemkimbiza jembe la ccm
 
nape, hebu tuambie nini hatima yako ndani ya CCM baada ya katibu mkuu wako kuomba kujiuzulu?,

wewe unatumiwa na m/kiti wako, kama kawaida yake ikifika wakati wa uchaguzi atakutosa tu.
jikumbushe yaliyojili siku za nyuma
1.wakati wa kampeni za uchaguzi 2010 m/kiti wako aliwapigia kampemi mramba,rostam, chenge huku wakituhumiwa kwa ufisadi na kuhujumu uchumi,huyo huyo akakutuma uzunguke nchi nzima ukihubiri dhana ya kujivua gamba, ukiwatuhumu hao hao, hivi kweli kaka nape kwa akili ya kawaida unamwamini m/nyekiti wako
 
CCM NA KUJIVUA GAMBA

Tisini Zimeisha, Uamuzi bado Mgumu










Msomaji Raia

Toleo la 194
13 Jul 2011
















SIKU 90 tisini zilizolengwa na uongozi wa Chama cha Mapinduzi kuwa zingetumika kufanya maamuzi magumu ya kujivua gamba au kulazimishana kujivua gamba, zimekwisha.
Mambo makuu matatu yanaweza kuwa yamechukua nafasi katika kutafakari suala hili. Kwanza, katika siku ya 91, mmoja wa watuhumiwa watatu waliolengwa na maamuzi ya NEC ya CCM amezungumza katika Televisheni ya Taifa (TBC) kuwa yeye kama yeye amesaidia kuibua mjadala unaoendelea.
Mjadala huo unahusu hoja yake bungeni kuwa Serikali imepoteza uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Amehitimisha kwa kusema, muda si mrefu wananchi wataamua wenyewe nani mkweli kati yake na Serikali.
Pili, watendaji wa CCM, na hasa, Sekretariati yake wamejikanyaga sana katika kipindi cha siku 90. Ilifika mahali sisi watazamaji tukadhani uamuzi wa kujivua gamba ulikuwa umetolewa ndani ya vikao vya CCM bila maandalizi ya kutosha kiasi cha kusababisha mkanganyiko wa hatari kwa utendaji wa chama hicho.
Kimsingi, kulikosekana msisitizo unaofanana kuhusu ni nini hasa maana ya kujivua gamba, nani anavuliwa au kujivua gamba, lini kazi hiyo ifanyike na ni nani hasa anasimamia kazi hiyo ikiwa hata gamba lenyewe halifahamiki, likifahamika linashtua. Itakumbukwa kuwa iliwahi kusemwa huko nyuma kuwa hata Mwenyekiti wa CCM anaweza kuwa gamba!
Tatu, siku 90 zikiwa zimeyoyoma, kitendawili kinaibuka ikiwa CCM na Serikali yake inakabiliwa na tatizo la kufanya maamuzi magumu au kuna tatizo la msingi katika dhana inayoitwa "ugumu wa maamuzi"?
Katibu Mkuu Wilson Mukama ambaye namfahamu kwa udhati wake wa kuchambua masuala anaweza kukisaidia CCM kupambanua dhana hii.
Kwa upande wangu, nieleze kwa kifupi. Kufanya maamuzi magumu ni jambo linaloeleweka. Hata pale Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alipotamka bungeni kuwa Serikali inapata kigugumizi cha maamuzi magumu alimaanisha kwa lugha ya kawaida, tabia ya Serikali kufanya maamuzi yenye maslahi kwa nchi hata kama kwa kufanya maamuzi hayo, maslahi binafsi ya watu na taasisi yanaweza kuwa yameathirika.
Kwa maneno mengine, ni maamuzi ambayo yanaweza hata kuharibu maslahi ya muda mfupi ya Serikali yenyewe lakini yakiwa yamelenga maslahi ya muda mrefu kwa taifa na watu wake wengi.
Ni maamuzi ambayo huweka tofauti za kiitikadi na nyinginezo pembeni na kuamua kulitanguliza taifa na watu wake. Ni maamuzi yaliyojengwa katika ujasiri wa kivitendo badala ya nadharia ya kutumia "hekima", hata kama ndani ya maamuzi magumu kuna hekima pia.
"Ugumu wa maamuzi" ni tofauti kabisa na maamuzi magumu. Dhana ya "ugumu wa maamuzi" imejengeka katika tabia ya mtu na taasisi vyenye tabia ya kufanya uamuzi wowote, uwe mwepesi au mgumu. Ni tabia si ya kuzaliwa nayo, bali inayojengeka katika haiba ya mtu kutokana ama na makuzi au mazoea tu.
Inapotokea mtu huyo akapewa majukumu ya kuongoza kundi, tabia ya kiongozi huyu huliathiri kundi hilo na lenyewe kwa kujua au kutojua huakisi tabia ya kiongozi huyo.
Tabia yenyewe inayozungumziwa hapa ni ile ya kusitasita kufanya maamuzi na kuishia kutofanya maamuzi bila kujali kama maamuzi ni magumu au mepesi.
Kiongozi wa namna hii au taasisi yake hupenda kuwauliza watu wanapenda nini ili aweze kufanya maamuzi hata kama kimsingi watu hawa waliishampa madaraka na mamlaka ya yeye kuamua kwa niaba yao. Kiongozi wa namna hii, hata katika maamuzi yanayomhusu yeye binafsi, hufurahia sana ikiwa uamuzi fulani unasogezwa mbele au kuyeyuka wenyewe bila yeye kulazimika kufanya huo uamuzi.
Kwake yeye, kila kitu ni sahihi na kizuri na hapo hapo kinaweza kugeuka kuwa kibaya kutegemea watu wanasemaje bila hata kumpa sababu ya mabadiliko hayo ya mtizamo.
Katika medani za masuala ya uongozi wa taasisi, tabia hii huzaa dhana ya "ugumu wa kufanya maamuzi". Ni uongozi unaoshamiri endapo hakuna maamuzi ya kufanya.
Tukirudi katika sakata la CCM kujivua gamba, nalazimika kuamini kuwa CCM inakabiliwa na magonjwa yote mawili, yaani kushindwa kufanya maamuzi magumu kunakotokana na tabia ya uongozi wake kushindwa kufanya maamuzi hata bila kujali kama ni magumu au mepesi.
Kwa taasisi ya chama cha siasa tena kinachoongoza dola, haya ni magonjwa ya hatari sana maana yameshika pabaya. Uimara wa chama huangaliwa katika uwezo wake wa kufanya maamuzi mepesi na magumu.
Chama kisichokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kinageuka kuwa kijiwe cha "mazuzu" kama alivyosema Baba wa Taifa. Dalili za CCM kuwa kijiwe cha mazuzu tumeziona na ziko wazi.
Ndani ya Bunge, ni wabunge wa CCM wanaoongoza kwa kuunga mkono kila jambo linalosemwa na Serikali. Imefikia mahali hata mawaziri wanaona aibu wanavyoungwa mkono na wabunge wa CCM hata kwa mambo ambayo hawajasema rasmi au wameyasema kwenye vijiwe vya wakubwa tu.
Hii ni dalili ya chama kusahau wajibu wake na kujisalimisha kwa Serikali. Katibu wa Siasa na Itikadi wa NEC, Nape Nnauye hivi majuzi alinukuliwa akisema chama kiko juu ya Serikali lakini sikusikia ubishi wowote juu ya hili. Kinadharia alikuwa sahihi, katika vitendo alikosea sana.
Chama cha Mapinduzi kilikwishakupoteza hatamu zake kwa Serikali na hakuna dalili kuwa kitazipata tena. Serikali nayo imezipoteza hatamu hizo ikiwa haiwezi kufanya maamuzi magumu au hata kufanya maamuzi yoyote yawe mepesi au magumu.
Hatamu za Serikali zilipokonywa na ushabiki ulioshamiri ndani ya chama na kuunda mitandao yenye nguvu kuliko chama chenyewe. Ndiyo maana haishangazi leo hii, chama kinatokea mbele ya wananchi na kuahidi kuwa kitajivua gamba ndani ya siku 90, au zaidi kidogo, na baada ya hapo kazi inayofuata ni kubishania nini maana ya gamba kana kwamba dhana hiyo imetolewa na mtu aliye nje ya chama.
Uongozi wa Serikali ulipochukuliwa na watu kwa misingi ya kimitandao, waliochukua madaraka walipoteza hatamu zao mikononi mwa waliounda na kuendesha mitandao hiyo. Na wenye mitandao waliwakabidhi Serikali mambo yote isipokuwa uhuru wa kuamua na kutenda.
Kwa wenye akili hatushangai kuwa anatokea mtu anahoji uwezo wa Serikali kufanya maamuzi na Serikali yenyewe inanywea au inatuma watu wa kuijibia ambao hata ukiwaangalia usoni unaona wazi kuwa hawaamini kile kile wanachokitetea.
Msanii wa CCM John Komba aliwahi kuimba wimbo uitwao "Mgeni" akimaanisha ukimwi ulivyoingia katika nyumba zetu. Wimbo ule ukadai kuwa kinachoshangaza juu ya ugeni huu ni kuwa amemwaga ***** kwenye kitanda cha baba na mama na sasa hawaelewani.
Ndani ya CCM ni wazi sasa kuwa hatushughuliki na dalili bali tunashughulika na ugonjwa uliokomaa. Na kwa kuwa kuna mgeni aliingia ndani ya chama chetu mpaka chumbani; na kwa kuwa sasa humo ndani hatuelewani hata katika dhana nzima ya kujivua gamba, tukubali kuwa maafa yanatunyemelea.
Na lililo kubwa kuliko yote ni pale waliolengwa kuvuliwa gamba, watakapowavua gamba wale waliodhani wao hawana magamba. Hilo likitokea ujue mwanzo wa mwisho umeanza maana katika mchezo wa kuwinda sungura, ukiona sungura kamgeuka mbwa na kuanza kumfukuza, inabidi waitwe waganga na waganguzi.










 
By Nnauye Jr
Nimeamua kuja mwenyewe. Nashangaa wakati mwingine maana ni hapa ndo watu walisema Nape kashazibwa mdomo kama vile yale ni maamuzi ya Nape binafsi.
Jana nimewakumbusha tu watuhumiwa na wapambe wao si busara kujifariji kuwa maamuzi yatabadilishwa nje ya vikao, na vikao vyenyewe ni lazima iwe ama NEC au Mkutano Mkuu(Congres) na si vinginevyo.
Kuna hoja hapa eti kwamba Nape anabwabwaja tu, hakuna vitendo, let's be objective,hivyo vitendo ni vipi? Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi haya itatolewa kwenye kikao kijacho cha NEC na si siku 90 kama wanavyojaribu kueleza hapa. Tumelieleza sana hili la siku,WAANDISHI TENA BAADHI ndo walitafsiri siku tisini kutoka kwenye ratiba ya vikao vya NEC ambavyo Dodoma tulikubaliana tentively tunaweza kukutana July ndo wakahesabu na kusema siku tisini. Lakini hakuna kikao kinakutana exactly kwa muda ulopangwa,kuna flexibility.
Ushauri subirini NEC ikutane mtuseme tukishindwa kufukuza.



Hiyo ilikuwa kauli yako na inatofautiana na ya Leo mkuu
 
There are currently 144 users browsing this thread........Nnauye Jr............ajabu naona umezubaa zubaa tu, umeganda au? hakika akili ndogo zinaongoza akili kubwa, amejisemea Mch. Msingwa......Nape kama Nyerere akirudi na kucharaza wanafiki wote, basi wewe utapata mboko nyingi sana
 
Hii Ilikuwa ni Mwaka 2011

Wiki iliyopita, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilimuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kuwaandikia barua viongozi wanaotakiwa kujiuzulu kuwafahamisha kwamba, kama hawatafanya hivyo kikao kijacho cha NEC kitawafuta uongozi.

Watuhumiwa hao wa rushwa na ufisadi wakiwemo wajumbe wa NEC taifa, wamepewa muda wa miezi mitatu sawa na siku 90 wapime uzito wa tuhuma zinazowakabili, wajiuzulu wenyewe.

Halafu wanajifanya kukana Kauli zao hapa
 
Mkuu Waache waendelee Kufurahia Baga na Piza on the expense ya sisi kushindia Vipande vya Mihogo. Mwisho wao u karibu

kwetu piza na baga huwa tunasikia tu hata zinafananaje hatujui ila mda utafika nape hatatofautiana na chokoraa.
 
Nape aliwataja Rostam, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kuwa ni miongoni mwa wanaotakiwa kujivua gamba.
Pia Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara,Pius Msekwa, lithibitsha baada ya ku§kutana na Chenge, Lowassa na Rostam na kwamba taarifa ya matokeo ya mazungumzo itawasilishwa katika vikao vikuu vya chama.

Soma Zaidi hapa

Hatma ya waliosalia kujivua gamba leo | Maskani ya uchambuzi yakinifu
 
Bashemere,
Kwanza nikushukuru kwa ustaarabu mkubwa katika kutoa hoja! Hili linatoa nafasi ya kujadili hoja badala ya kejeli na matusi!naahidi kushirikiana na wote watakao kuja kwa hoja kuzijibu moja baada ya nyingine! Sitajishughulisha na kejeli na matusi!

Niweke wazi kuwa msimamo wangu dhidi ya ufisadi na rushwa (ambao kwakweli ni matumizi mabaya ya rasilimali)BADO UKO PALEPALE, NA SITAYUMBA KATIKA HILI!
goodone...........
 
Hii Ilikuwa ni Mwaka 2011 Halafu wanajifanya kukana Kauli zao hapa
Pamoja na kutubakisha shule za kata sisi washindia mihigo, na kutudhalilishia walimu wetu na kututekea madokta wetu lakini bado tunawazidi akili...........yuko wapi huyu msemaji wa Mabwepande
 
Back
Top Bottom