Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani?

Nape watu wanataka Majawabu Siyo Majibu.... Theme ya mikutano(jangwani,Rukwa na kigoma) yenu ni ipi?

Jibu kwanza maswali yangu kwako ili tuweke kumbukumbu sawa badala ya kurukia swala jingime, by the way ina thread yake hiyo hoja ya ziara mikoani
 
Mtoto wa mjini,
Nani alitoa miezi mitatu ya mtu kujivua UANACHAMA WA CCM?!!?? nashauri take time kulijua jambo vizuri kabla hujakurupuka kuhukumu! Hakuna mahali CCM katika uongozi huu imewahi kuagiza watu wajiudhulu uanachama wa CCM.

Nape nashukuru kwa kushiriki kujibu hoja mbalimbali za wana JF. Ukweli ni kuwa kupinga ufisadi ukiwa ndani ya CCM ya sasa ni kudanganyana tu. Hakuna wa kumfunga kengele mwenzake. Najua nia yako juu ya kupinga ufisadi ilikuwa ya dhati enzi hizo lakini si kwa leo. Ukweli ndio huu.
 
Kwakweli ninasikitishwa na lugha hizi na hasa zinapotolewa na watanzania " ETI VITA YAKO NAPE DHIDI YA UFISADI" hivi kumbe ni vita yangu?!!!! Kwa kuwa mie ndo mwathirika mkubwa wa ufisadi!!!??? Nape wa 2005 ni yupi na Nape wa2012 ni yupi? INAVUNJA MOYO SANA UNAPOJITOLEA KUPAMBANA NA UFISADI KWA FAIDA YETU NA WATOTO WETU NA HATA WAJUU ZETU HALAFU ANATOKEA MTU ANADAI HII VITA NI YANGU KAMA VILE NI KWA FAIDA YANGU, OOOOPS! Watanzania zaidi ya uwajuavyo!

Naona umeamua kunikwepa,naukiza tena ivi unaweza kupambana nu ufisadi ukiwa ndani ya ccm?kumbuka watuhumiwa wananguvu ndani ya chama.Na vipi kuhusu mikutano ya chama inayoendelea pesa zinatoka wapi au nizilezile kodi? hapo kwenye red,Nape wa 2005 alipaza sana sauti juu lasilimali za taifa,Nape wa 2012 ajulikani ni moto au baridi
 
Jibu kwanza maswali yangu kwako ili tuweke kumbukumbu sawa badala ya kurukia swala jingime, by the way ina thread yake hiyo hoja ya ziara mikoani

Swali gani umeniuliza?weka hilo swali nitupie majawabu fasta.
 
Si busara kupotosha ziara ya Mhe. Rais jimboni Monduli, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wafugaji waliopata madhara kwa mifugo yao kufa kwasababu ya ukame.( NIKUMBUSHE KUNA WATU WALIKUWA WANAHOJI HAPA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA RAIS KIKWETE WAKATI WA UCHAGUZI, ANZENI KUHESABU KABISA TUSIJE ULIZANA). Na si ziara yake ya kwanza alishawahi kwenda jimbo la Telele kugawa ng'ombe kama alivyofanya Monduli. Na utekelezaji wa ahadi hizi za kufidia wafugaji unaendelea!

NAPE; rais kugawa ng'ombe walionunuliwa kwa fedha nyingi za walipa kodi nayo ni rushwa.Kumbuka wakati wafugaji wanaomba kuingiza ngombe kwenye hifadhi ya mbuga ya ngorongoro eneo linalomilikiwa na ortelo ltd, mlituma jeshi la polisi na FFU kwenda kuwaondoa na kuchoma mabanda yao, na pia kuna watu walibakwa.taasisi nyingi zililaani kadhia hii , mpaka kufanya watanzania wale kuonekana ni wakenya.Hiki kikuwa chanzo cha mifugo mingi kufa, sababu zilikosa malisho.je kuwaruhusu waingize kuchunga , ili kuepusha mifugo hiyo isife,je kununua hii mifugo ya rushwa au kuruhusu, lipi la maana?hizi fedha zisingetumika kama rushwa bali , zingesaidia kufanya shughuli nyingine.nape kumbuka watu wanapokea mifugo hiyo kwasababu wamepewa, lakini uelewe uovu waliotendewa na serikali hawatausahau.
 
Eeeee nape leo fanya kazi ya yenezi kweli coz naona leo wachangiaji wana staha kweli usichoke:OK umesema hamlengi mtu mnalenga tabia,sasa mmezunguka mikoani mnawatangazia watu kuwa ndani ya siku tisini watu wa tabia hii lazima wajivue gamba either kwa hiari au lazima na hao watu wenye hizo tabia watu wanawafahamu na wanawasema na nyie mnasiki then siku 90 zilishaisha sasa nafikiri tuko karibia 900 wale watu ndo wanazidi kuwa mashujaa kwenye chama unategemea nn?
 
Naona umeamua kunikwepa,naukiza tena ivi unaweza kupambana nu ufisadi ukiwa ndani ya ccm?kumbuka watuhumiwa wananguvu ndani ya chama.Na vipi kuhusu mikutano ya chama inayoendelea pesa zinatoka wapi au nizilezile kodi? hapo kwenye red,Nape wa 2005 alipaza sana sauti juu lasilimali za taifa,Nape wa 2012 ajulikani ni moto au baridi

Sijakwepa swali na si style yangu kukwepa maswali. Ni seme hata huyo nape wa mwaka2005 alikuwa anatukanwa sana humu, so humu hakuna shukurani nami najua isipokuwa kwa wateule wachache wa CDM nasema wachache si wote! Kwahiyo kama wana nguvu tuwaachie Chama? Na unajua maana yake?
 
Eeeee nape leo fanya kazi ya yenezi kweli coz naona leo wachangiaji wana staha kweli usichoke:OK umesema hamlengi mtu mnalenga tabia,sasa mmezunguka mikoani mnawatangazia watu kuwa ndani ya siku tisini watu wa tabia hii lazima wajivue gamba either kwa hiari au lazima na hao watu wenye hizo tabia watu wanawafahamu na wanawasema na nyie mnasiki then siku 90 zilishaisha sasa nafikiri tuko karibia 900 wale watu ndo wanazidi kuwa mashujaa kwenye chama unategemea nn?

Kwanza unajua fika kuwa hatukuwahi kutoa siku tisini kama unavyodai,isipokuwa tulitoa muda wa kutoka kikao mpaka kikao! Nawewe ni shahidi wapo waliotoka na si kama mnavyoeneza eti hakuna aliyetoka kabisa! Na kwakujua kuwa wapo wataogoma kutoka tukasema muda tuliotoa ukiisha tutarudi kuchukua hatua kwenye vikao,muda wa kutoka kwa hiari uliisha na tumeriudi kwenye vikao na wanashughulikiwa baada ya uchaguzi wa ndani ya Chama njooni hapa mniulize
 
NAPE; rais kugawa ng'ombe walionunuliwa kwa fedha nyingi za walipa kodi nayo ni rushwa.Kumbuka wakati wafugaji wanaomba kuingiza ngombe kwenye hifadhi ya mbuga ya ngorongoro eneo linalomilikiwa na ortelo ltd, mlituma jeshi la polisi na FFU kwenda kuwaondoa na kuchoma mabanda yao, na pia kuna watu walibakwa.taasisi nyingi zililaani kadhia hii , mpaka kufanya watanzania wale kuonekana ni wakenya.Hiki kikuwa chanzo cha mifugo mingi kufa, sababu zilikosa malisho.je kuwaruhusu waingize kuchunga , ili kuepusha mifugo hiyo isife,je kununua hii mifugo ya rushwa au kuruhusu, lipi la maana?hizi fedha zisingetumika kama rushwa bali , zingesaidia kufanya shughuli nyingine.nape kumbuka watu wanapokea mifugo hiyo kwasababu wamepewa, lakini uelewe uovu waliotendewa na serikali hawatausahau.

Wanapewa ng'ombe sio hao unaowasema wewe, chunguza kabla ya kutoa shutuma pls
 
Kwanza unajua fika kuwa hatukuwahi kutoa siku tisini kama unavyodai,isipokuwa tulitoa muda wa kutoka kikao mpaka kikao! Nawewe ni shahidi wapo waliotoka na si kama mnavyoeneza eti hakuna aliyetoka kabisa! Na kwakujua kuwa wapo wataogoma kutoka tukasema muda tuliotoa ukiisha tutarudi kuchukua hatua kwenye vikao,muda wa kutoka kwa hiari uliisha na tumeriudi kwenye vikao na wanashughulikiwa baada ya uchaguzi wa ndani ya Chama njooni hapa mniulize

Nape umesema wako waliotoka unaweza kuweka record straight kwa kuwataja maana kama walitoka then huna haja ya kuwaficha lakini kama una maanisha Rostam hakutoka kwa jina la ufisadi bali ni kuzidiana kwenye malipo ya dowans yeye na Mwenyekiti .Hapa ni JF ukibisaha kama kawaida tutaweka ushahidi juu ya hili la Rostam kuacha Ubunge etc .Now tunaomba majina ya walio toka kwa wewe kupiga kelele tafdhali
 
Weka USHAHIDI WA HILO LAKO nami NITAJIUZULU NAFASI ZANGU NDANI YA CCM
 
Wanapewa ng'ombe sio hao unaowasema wewe, chunguza kabla ya kutoa shutuma pls

Nape kwa kuwa unamwaga facts badala kuacha achunguze wewe uko hapa kujibu ukweli basi funguka utueleze si hao basi ni wapi ? Nani kawanunua ? Kwa gharama za kiasi gani?Fedha zimetoka wapi ?

Unasemaje juu ya Issue ya Ortelo na hujuma walio fanyiwa watanzania wafugaji ?
 
Nape nitaweka kama utawataja walio jiondoa kwa kelele zako .Nangojea nimalizie mie

Huna lolote umesema nikibisha unaweka nimebisha, WEKA!! hakuna asiyewajua waliotoka.....kama wewe hujui muulize jirani yako hapo ulipokaa
 
Nape nitaweka kama utawataja walio jiondoa kwa kelele zako .Nangojea nimalizie mie

Nenda kasome hotuba ya aliyetoka unayemjua KANITAJA MARA NGAPI KWENYE HOTUBA YAKE??????!!!!!! kwanini hakukutaja wewe?!?!?!?
 
Hivi na wewe unaamini hayo maneno ya serikali ya wingereza?
Na chama chako kimefanya uchunguzi katika hili au kinaendelea kufanya?
Na nini msimamo wa chama katika hili hasa wewe?.

Hivi hayo maneno umemnukuu nani??? Kwanini tunachukua tafisiri zetu na kuzileta hapa?!!! Alichosema Rais taarifa za mahakama ya Uk zinasema mpaka sasa wameshindwa kuthibitisha Rushwa kwenye sakata la Rada. Hayo maneno yako kwenye hotuba ya Rais yako wapi?
 
Umesema kuna watu walipewa miezi mitatu wajiondoe UANACHAMA WA CCM, nimekuuliza WALIPEWA HUO MUDA NA NANI NA NI KINA NANI WATU HAO?

Hao watu walipewa Muda Huo na Wewe ila Mukama akakupiga Mkwara
 
Back
Top Bottom