Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani?

Kwakweli ninasikitishwa na lugha hizi na hasa zinapotolewa na watanzania " ETI VITA YAKO NAPE DHIDI YA UFISADI" hivi kumbe ni vita yangu?!!!! Kwa kuwa mie ndo mwathirika mkubwa wa ufisadi!!!??? Nape wa 2005 ni yupi na Nape wa2012 ni yupi? INAVUNJA MOYO SANA UNAPOJITOLEA KUPAMBANA NA UFISADI KWA FAIDA YETU NA WATOTO WETU NA HATA WAJUU ZETU HALAFU ANATOKEA MTU ANADAI HII VITA NI YANGU KAMA VILE NI KWA FAIDA YANGU, OOOOPS! Watanzania zaidi ya uwajuavyo!
Kiongozi taratibu, sio wote kuna baadhi ambao ni shida kidogo kwa ufahamu wao na mtizamo walio nao, tatizo watu hawasomi yawezekana hata baadhi ya nyaraka a=zianazopatikana hata humu zikizi=ungumzia maswala haya labda hazikuwa katika lugha wanayoielewa.

Unajua pia usisahau hawa ndiyo wanaoshangilia wakisikia mtu anadhalilika au kudhurika, hawa ni hatari sana maana wao tuhuma huzigeuza hukumu haraka haraka, bila kutumia muda kufikiri wanakumbwa na upepo wa kisiasa na wa magazeti yanayojaribu kufanya biashara na mwisho wanakuwa na mawazo ya ajabu kabisa.

Laiti wangeujua ukweli wa haya yote
 
Nape bana, hujibu swali kama ulivyoulizwa unajibu kisiasa tu(Pinda type)

Unaulizwa kwanini JK anakwenda kumsafisha Mramba jukwaani anawaambia wananchi hili ni 'jembe la zamani haliishi makali' wakati Mramba ni mtuhumiwa wa Ufisadi,? toa jibu huna unaanza siasa. Hamna k2 hapo like father like son
 
mpiganaji aliye kwenye chama kibaya anapigania nini? huoni watu wa aina ya nape na sitta ndo wanarudisha nyuma jithada za kuikomboa nchi kutoka kwa wezi???
 
Naitwa OKW BOBAN SUNZU, ila kuhusu Rage hapana, yaani basi ni kwa sababu Mnyama yupo damuni, ingekuwa ni ishi zingine uwepo wa Rage Simba ingekuwa sababu ya mi kusitisha mahaba na hii timu
 
Bashemere,
Kwanza nikushukuru kwa ustaarabu mkubwa katika kutoa hoja! Hili linatoa nafasi ya kujadili hoja badala ya kejeli na matusi!naahidi kushirikiana na wote watakao kuja kwa hoja kuzijibu moja baada ya nyingine! Sitajishughulisha na kejeli na matusi!

Niweke wazi kuwa msimamo wangu dhidi ya ufisadi na rushwa (ambao kwakweli ni matumizi mabaya ya rasilimali)BADO UKO PALEPALE, NA SITAYUMBA KATIKA HILI!

SOMA HAPA ....House of Commons - HC 847 International Development Committee: Written evidence from Global Witness
 
Mtoto wa mjini,
Nani alitoa miezi mitatu ya mtu kujivua UANACHAMA WA CCM?!!?? nashauri take time kulijua jambo vizuri kabla hujakurupuka kuhukumu! Hakuna mahali CCM katika uongozi huu imewahi kuagiza watu wajiudhulu uanachama wa CCM.

mhh hapa kweli wewe nape kiboko umeruka duuu!
ccm chama changu ila mmh hatuna nguvu ya kupambana na wizi!
 
Umesema kuna watu walipewa miezi mitatu wajiondoe UANACHAMA WA CCM, nimekuuliza WALIPEWA HUO MUDA NA NANI NA NI KINA NANI WATU HAO?

Acha unafiki mtoto wa ki-ume, wewe umetoka kwenye kikao chenu umekuja kutangaza mmewapa siku 90 watuhumiwa wa ufisadi la sivyo watafukuzwa chamani halafu leo unakuja hapa kuandika upuuzi wako? Wewe ni fisadi tu kama hao mafisadi wengine unaotembea kutwa kuchwa ukiwataja kwenye majukwaa ya siasa halafau ukija hapa unatuletea unafiki wako.
 
Nape,
Pamoja na kujinasibu kuwa hukimbii maswali na siyo syle yako, kumbu kumbu zinaonyesha kuwa baada ya kauli yako kuhusu muungano, tulikuuliza maswali na ULIKIMBIA. Ushahidi upo hapa JF

Ukisioma bandiko la Mag3 utaona amekuwekea maelezo kwanza kisha akauliza swali.
Hujajibu swali lake kuhusu yaliyojiri Halmashauri kuu,umebaki kujibu tuhuma zisizo na maana ambazo ungeweza kutozijibu bila kuathiri heshima yako katika staili ya mipasho.

Nape, Mwenyekiti wako almesema suala la Rada hakuna mwizi ni kukosea tarakimu tu!! Hata waliokosea tarakimu hawajulikana. Amejichanganya sana kuhusu suala hili nawe unafahamu jinsi anavyowaogopa mafisadi.
Hakuna ubishi na ni uwendawazimu kuweka maneno mengine yatoe tafsiri nyingine zaidi ya kuwa amewasafisha akina Chenge na amekusaliti mchana kweupe. Nitty gritty mheshimiwa

Hata pale umma unapokuwa nyuma yako, inapotokea majemadari wanakusaliti basi ujue umepoteza vita. Hakika unajua fika kuwa wewe na chama chako mumeshindwa kuwaondoa wahalifu wakubwa nchini wa kisiasa na kiuchumi kwasababu nyuma ya pazia majemadari wapo na wahalifu na wakati wa chai wapo na nyinyi.

Tangu ulipoanza sera za kuvua magamba, hakuna chochote unachoweza kusimama katika jukwaa na kukitetea.
Hao mafisadi wanaosemekana wapo mahakani, wapo kule si kwasababu ya kukichafua chama, ni ugomvi binafsi wakati wa harakati za kuwania Urais. Waliokichafua chama wapo na wanapeta, manapishana vikumbo, halafu utudanganye!

Endapo ingekuwa ni kwasababu ya ufisadi, leo akina Chenge, Lowassa wasingekuwa na uongozi achilia mbali sifa za uanachama. Sasa umeshindwa mapapa unahubiri nini? Kuna fisadi gani Tanangozi, kipera, mabokweni au Mkuranga?

Huna sababu ya kukatishwa tamaa na wanaJF , aliyekukatatisha tamaa ni mwenyekiti wako wa CCM ambaye anakutumia wakati huo huo anajisafisha kwa maswahiba zake.

Vita imekushinda na kama kweli unadhamira ya dhati kwa taifa hili na si ulua au VX basi upo sehemu isiyo sahihi.
Hakuna mabadiliko ndani ya CCM, wanamabadiliko kama Sokoine hawapo, hawa hawakupigana vita ya mipasho, walipigana vita ya vitendo.
 
Wale Wote Tunaishindia Vipande vya Mihogo Mibichi tuwe tunashtuana Ikitokea Miniso Kama Hii Jamani siyo Wafaudu Peke Yao akina Nape

Nape nauliza hivi, huko Igunga hakuna inzi? Mbona msosi haukufunikwa? Au kwa vile shida yenu ilikuwa kupata kura tu wakiharisha kivyao.
 
Nape kala kona, kilichonifurahisha ni kuyakana maneno yake mwenyewe ya siku 90 kwa Rostam, Chenge na Lowassa
 
Si busara kupotosha ziara ya Mhe. Rais jimboni Monduli, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wafugaji waliopata madhara kwa mifugo yao kufa kwasababu ya ukame.( NIKUMBUSHE KUNA WATU WALIKUWA WANAHOJI HAPA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA RAIS KIKWETE WAKATI WA UCHAGUZI, ANZENI KUHESABU KABISA TUSIJE ULIZANA). Na si ziara yake ya kwanza alishawahi kwenda jimbo la Telele kugawa ng'ombe kama alivyofanya Monduli. Na utekelezaji wa ahadi hizi za kufidia wafugaji unaendelea!

Mheshimiwa napenda kukutia moyo juu ya wanaokushambulia ni kawaida kwa mti wenye matumda kupigwa mawe hivyo wewe songa mbele mawe yakiisha watatulia
 
Nimefurahi jambo moja kwa Nape, huyu jamaa na ujasiri wa ajabu kama anaweza kupinga hata ukweli ambao kila mtu anaona. Hata ya kutoa siku tisini anapinga basi huyu bwana ana ujasiri wa kipekee nakupongeza bwana mkubwa naamini siku moja utapinga kuwa wewe jina lako si NAPE na kusema wazazi wako walikosea jina sitashangaa nikikusikia.
 
Back
Top Bottom