Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari ya JK Monduli, Nape una maoni gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bashemere, Aug 4, 2012.

 1. b

  bashemere Senior Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hoja unayo Nape, sema umeiweka kifasihi sana kiasi cha kwamba wasomaji wengine hatukuelewi. Na huenda kosa la msingi limefanywa na mtoa hoja ambaye amekimbilia kukushambulia badala ya kutoa hoja.

  Angeuliza hivi, Nape unajiskiaje kutokana na maendeleo ya siasa ndani ya chama chako hasa baada ya mwenyekiti kuuthibitishia umma kuwa Mh. Chenge ni safi na juzi kwenda Monduli kukabidhi ngombe kazi ambayo hata waziri wa mifugo angeifanya, na tafsiri ya wengi ni kuwa ameenda kuuonesha umma kuwa Mh. Lowassa ni safi.

  Je, matendo haya ya mwenyekiti wako yatakubadilisha mtazamo wako juu ya watu hawa? Nini maoni yako. JAMANI NAOMBA TUSIKIMBILIE KUTOA LUGHA CHAFU AMBAZO MWISHO WA SIKU ZINATUFANYA TUKOSE KUPATA TAARIFA NA KUWAPA WATU HAKI YAO YA MSINGI YA KUJIELEZA.

  Nape ningeomba unijibu maswali yangu.
   
 2. b

  bashemere Senior Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG][/h]
  ​sasa hayo makundi ni mtaji mzuri sana mmemsema san rosatam lowasa chenge sasa mtajiju tuliwaambia kikwete si wa kuaminika
   
 3. I

  Iramba Junior Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kwa hili ni haki yetu wa TZ kujua msimamo wako Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Tawala
   
 4. H

  Honey K JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bashemere,
  Kwanza nikushukuru kwa ustaarabu mkubwa katika kutoa hoja! Hili linatoa nafasi ya kujadili hoja badala ya kejeli na matusi!naahidi kushirikiana na wote watakao kuja kwa hoja kuzijibu moja baada ya nyingine! Sitajishughulisha na kejeli na matusi!

  Niweke wazi kuwa msimamo wangu dhidi ya ufisadi na rushwa (ambao kwakweli ni matumizi mabaya ya rasilimali)BADO UKO PALEPALE, NA SITAYUMBA KATIKA HILI!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Nape,

  ..Anna Kilango amemsafisha Lowassa na kusema bunge lilikurupuka kumsulubisha.

  ..JK naye amemsafisha Chenge kwa kudai kwamba hakukuwa na rushwa ktk ununuzi wa rada.

  ..Chama chako pia kilimpitisha Basil Mramba, mwenye kesi ya ufisadi, kugombea ubunge, na JK akashiriki kumpigia kampeni.

  ..Kwa mwendo huu hivi mnategemea wananchi wawaamini kwamba mnapiga vita ufisadi??
   
 6. H

  Honey K JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Si busara kupotosha ziara ya Mhe. Rais jimboni Monduli, ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kwa wafugaji waliopata madhara kwa mifugo yao kufa kwasababu ya ukame.( NIKUMBUSHE KUNA WATU WALIKUWA WANAHOJI HAPA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA RAIS KIKWETE WAKATI WA UCHAGUZI, ANZENI KUHESABU KABISA TUSIJE ULIZANA). Na si ziara yake ya kwanza alishawahi kwenda jimbo la Telele kugawa ng'ombe kama alivyofanya Monduli. Na utekelezaji wa ahadi hizi za kufidia wafugaji unaendelea!
   
 7. ELFU-ONEIR

  ELFU-ONEIR Senior Member

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ok usizunguke hebu sema na hili la chenge kusafishwa na mwenye nyumba unalizungumziaje? Hasa ukizingatia kuwa mtandao wa wiki-leaks uliweka bayana kilichotokea. Je wewe unalipi la kusema?
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nape ana avoid maswali aliyoulizwa hapo juu... kwanini apokelewe na mtu ambaye yeye mwenyewe JK alimpa miezi mitatu awe ameshajivua uanachama wa ccm?? jibu swali sio kuzuga
   
 9. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Nape kumbuka wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi bado wana nguvu ndani ya chama,swali,je unaamini mapambano yako juu ya ufisadi yatafanikiwa ukiwa ndani ya ccm au unatupaka mafuta kwa mgongo wa chupa?Nape mi nakukumbuka sana ulivyokuwa mstari wa mbele kupambana na ufisadi,lkn Nape wa 2005 si Nape wa 2012.
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,749
  Trophy Points: 280
  Je kuhusu chenge na ile kashfa ya rada umepokeaje taarifa kuwa ni mtu safi kabisa.
  Je nawewe una ungana na mwenyekiti kuwa chenge ni mtu safi?
  Naomba ujibu moja kwa moja na kwa ufupi!

   
 11. H

  Honey K JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ##La Anna Kilango umesema wewe, ni uzushi mnajaribu kuwalisha watu kwa sababu mzijuazo nyinyi.
  ##. La Rais kumsafisha Chenge, nayo ni tafisiri yako. Alichosema Rais kwa mujibu wa taarifa za kimahakama nchini Uingereza "wanadai" hawajafanikiwa kupata ushahidi wa rushwa!(kwa akili ya kawaida UK wangefanyaje zaidi ya kulinda heshima ya nchi yao na kampuni yao kubwa kabisa duniani ya uuzaji silaha?) lLakini hivi tuhuma zilikuwa rada pekeake?! Na ikumbukwe hata Chama kilisema tuhuma na wala hatuhitaji ushahidi wa mahakamani.....

  .
   
 12. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kuna thread humu ilikuwa inajadili 2015 rais ni CHADEMA ama Lowasa.....nafikiri ni katika kumtengenezea njia Lowasa.....
   
 13. H

  Honey K JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwakweli ninasikitishwa na lugha hizi na hasa zinapotolewa na watanzania " ETI VITA YAKO NAPE DHIDI YA UFISADI" hivi kumbe ni vita yangu?!!!! Kwa kuwa mie ndo mwathirika mkubwa wa ufisadi!!!??? Nape wa 2005 ni yupi na Nape wa2012 ni yupi? INAVUNJA MOYO SANA UNAPOJITOLEA KUPAMBANA NA UFISADI KWA FAIDA YETU NA WATOTO WETU NA HATA WAJUU ZETU HALAFU ANATOKEA MTU ANADAI HII VITA NI YANGU KAMA VILE NI KWA FAIDA YANGU, OOOOPS! Watanzania zaidi ya uwajuavyo!
   
 14. H

  Honey K JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi hayo maneno umemnukuu nani??? Kwanini tunachukua tafisiri zetu na kuzileta hapa?!!! Alichosema Rais taarifa za mahakama ya Uk zinasema mpaka sasa wameshindwa kuthibitisha Rushwa kwenye sakata la Rada. Hayo maneno yako kwenye hotuba ya Rais yako wapi?
   
 15. m

  mosagane Senior Member

  #15
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok,zidi kutiririka Nape,kwa moyo wako wa dhati na MUNGU unaye mwamini akikushuhudia,unaweza kukanusha kuwa mlipoasisi ajenda ya kujivua gamba pamoja na utetezi wenu kuwa ni ktk ngazi zote,unaweza kukanusha kuwa hamkuwalenga Rostam,chenge na Lowasa? eee baadae ikawaje?......
   
 16. H

  Honey K JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa mjini,
  Nani alitoa miezi mitatu ya mtu kujivua UANACHAMA WA CCM?!!?? nashauri take time kulijua jambo vizuri kabla hujakurupuka kuhukumu! Hakuna mahali CCM katika uongozi huu imewahi kuagiza watu wajiudhulu uanachama wa CCM.
   
 17. H

  Honey K JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huwezi kutaka kusafisha Chama kwa kuwalenga watu, unalenga tabia au matendo machafu sasa kama kuna watu wanayatenda hilo si lako ulie asisi usafishaji ni la mtendaji. Kwahiyo sio sawa kutaja watu wachache, NIMEKUWA NIKISISITIZA NI CHAMA KIZIMA,INAWEZEKENA KUKAWA NA WATU WANATAJWA TENA NA NYINYI KAMA MIFANO LAKINI SI TAASISI KULENGA WATU KADHAA BALI KULENGA VIONGOZI WENYE TABIA ZINAZONYOOSHEWA VIDOLE NA WANANCHI.
   
 18. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Vipi Nape kuhusu suala la JK kumteka na kumpa kichapo cha mwaka Dr. Ulimboka eti kwasababu anaowaongoza wenzake kugoma? Nashukuru sana kwa majibu utakayotoa Ndugu Nape.
   
 19. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nape watu wanataka Majawabu Siyo Majibu.... Theme ya mikutano(jangwani,Rukwa na kigoma) yenu ni ipi?
   
 20. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Nashukuru upo kujibu hoja zetu, swali, unazungumziaje kauli za CHADEMA kwamba polisi inatumika kudhoofisha au kuzuia ukuaji wa upinzani. Mfano, hivi juzi tu mikutano ilikatazwa Morogoro kwa sababu ambazo mantiki yake ni ndogo kama kuna mgomo wa walimu na kuhatarisha amani. Mbona mikutano ya CCM huwa hawapewi sababu kama hizi?
   
Loading...