Safari ya JK kwenda kutembelea timu ya Sunderland inamnufaisha nani?

JK kwa sasa yupo Sunderland kuangalia uwezekano wa kuzungumza na wamiliki wa Club ya Sunderland ya UK ili waanzishe Academy ya mpira Tanzania.

Mh Rais awaombe Pia wasaidie Kutoa mafunzo kwa makocha na viongozi namna ya kuendesha soka kisasa pasipo wanachama migogoro
 
Sasa Waziri wa michezo afanye kazi gani ikiwa kuomba club isaidie michezo anakwenda Rais ambako kwake kumeripuliwa bomu na hana habari. Ukiona hivyo ni dalili za mfa maji haachi kutapatapa
 
Wewe unataka afanye nini kumbuka akili yake si yako na unajua slaa ametembelea maeneo gani huko ujerumani au unakimbia kimbia tu.
 
Sasa Waziri wa michezo afanye kazi gani ikiwa kuomba club isaidie michezo anakwenda Rais ambako kwake kumeripuliwa bomu na hana habari. Ukiona hivyo ni dalili za mfa maji haachi kutapatapa
Waziri wa michezo yupo bungeni.
 
Cha msingi Mh Rais angewaalika makocha wote wa ligi kuu kisha Serikari iwalipie nauli watembelee vilabu vyote vikubwa vya ulaya wakutane na makocha wakubwa wapigwe msasa mkali angalau wajifunze live jinsi soka la kisasa linavyoendeshwa wajifunze mpaka lishe za wachezaji namna ya kudumisha nidhamu nje ya uwanja kwani mapungufu Haya Ndio tatizo sugu kwenye soka letu na endapo yatafanyiwa kazi Hakika soka letu litakuwa kwa kasi sana
Mkuu ndiyo maana akili ni nywele kila mtu anazake.
 
wakati mwengine akili zake zinamtosha yeye mwenyewe na genge lake, sasa raisi mzima uende ugenini ukatie nanga sunderland kisa kupata ushauri wa academy jamaa wa TFA wanashughuli gani sasa.

Duh! Kweli aisee,yaani huyu jamaa ni zero kabisa.
 
JK kwa sasa yupo Sunderland kuangalia uwezekano wa kuzungumza na wamiliki wa Club ya Sunderland ya UK ili waanzishe Academy ya mpira Tanzania.

Kikwete ana a very wrong mentality ya kufikiria kuwa misaada ndio solution ya matatizo yetu. Sunderland wakianzisha Academy itakuwa ni kwa mahitaji yao na sio kwa ajili ya Taifa. Zaidi ya hayo, Academy itachukua sana sana vijana wasiozidi 50. Kwa nini hiyo pesa aliyoitumia kwenda kuomba-omba asingeitumia kuimarisha michezo kama ya UMISETA? Ndio maana watu wanamsifia Kagame licha ya udikiteta wake.

Ellis%20Short%20and%20President%20of%20Tanzania.jpg

SOURCE: SAFC - New Academy announced
 
JK kwa sasa yupo Sunderland kuangalia uwezekano wa kuzungumza na wamiliki wa Club ya Sunderland ya UK ili waanzishe Academy ya mpira Tanzania.

Majanga matupu. Alianza na propaganda za kuwaleta Real Madrid Tz na sasa anamalizia na episode II ya Sunderland halafu akiulizwa kwa nini TZ ni masikini anasema hajui...
 
Halafu yeye si aliwahi kujinadi kuwa ni shabiki wa Newcastle Utd? Jinsi alivyo kilaza hajui Tyne-Wear derby ilivyo!
Si atulie kidogo, yaani hizi aibu mpaka basi. At best and very-top angeenda waziri wa wizara husika.
 
Sidhani football academy ni kipaumbele cha nchi hii.Kama hili lilikuwa ni moja ya malengo ya safari yake.MUNGU tunusuru maana tunapotea.
 
JK kwa sasa yupo Sunderland kuangalia uwezekano wa kuzungumza na wamiliki wa Club ya Sunderland ya UK ili waanzishe Academy ya mpira Tanzania.

Wewe hutaki team zetu zishinde? Go go prezzida. Go!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sidhani football academy ni kipaumbele cha nchi hii.Kama hili lilikuwa ni moja ya malengo ya safari yake.MUNGU tunusuru maana tunapotea.
Ni kipaumbele cha rais hata kama hutaki. Rais wetu ni askari, mchumi, mwanasiasa na mwanaspoti. Upo hapo?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom