Lukansola
JF-Expert Member
- Sep 5, 2010
- 5,435
- 1,597
Ninapoandika habari hii, nipo safarini nikitoke Igunga, hii ndio imekuwa mara yangu ya kwanza kutembelea wilaya hii.
napenda ku-share nanyi ndugu zangu kuhusu machache niliyojifunza katika siku mbili nilizoishi hapo. Nikianzia na hali ya hewa kwa sasa Igunga kuna joto kiasi. Jambo ambalo nimeliona pia ni kwamba maisha ya wananchi wa Igunga hayana tofauti sana na maisha ya wakazi wa wilaya zingine za nchi hii. Umeme upo lakini mgao ni kama sehemu zingine. Maji ya Igunga ni ya visima na ni meusi kusema kweli.
Nimekuwa nikisikia mara nyingi kuwa RA amewapa Igunga maisha bora na hata Mkapa kwenye kampeni alisema Igunga iko juu katika mkoa wa Tabora. Mimi napinga kwa sababu wananchi wa Igunga wamechoka tu, mji umejaa vumbi jekundu. Stendi mpya ya mabasi ni mavumbi matupu.
Jambo lililonishanga ni kusikia kuwa kumbe Rostam hana nyumba Igunga na kuna sehemu nyingi za vijijini ambazo hawamji wala hawakuwahi kumwona Rostam, mwenyeji mmoja aliniambia Rostam hajawahi kulala Igunga hata siku moja, huwa analala Mwanza.
Nikiwa nasubiri basi, nimepata fursa ya kupiga story na vijana pale stendi, inaoneka safari hii ccm haikatishi maana kusema kweli watu wamebadilika, wanasema wamechoka kudanganywa na hawaitaki ccm. wanasema ccm imeleta watu ili kuwapeleleza na kuwashawishi vijana kuichagua ccm lakini wamekuwa wakiwaambia waziwazi kuwa wameshachoka na wasipotezewe muda wao.
Kuhusu Dr. Kafumu ni kuwa amejenga nyumba chapchap wakati wa kura za maoni ili kujionesha ni mwenyeji wa huko.
Pembeni yangu nilimsikia mzee mmoja wa kike akiwauliza wazee wenzie wa kiume wawili aliokuwa akizungumza nao kwamba wao ni vyama gani? Yeye aliwaambia ni chadema hata wale wazee walimjibu hivyohivyo.
Kwa mtazamo wangu kutokana na experiance yangu ya muda mfupi ccm huenda wakalikosa jimbo hilo. I've got some pictures of Igunga but can't attach them cause am using a phone.