SAFARI YA DODOMA: Ni utashi wa Rais, Chama dola, ama ni SERA ya Taifa?

Lekachonka

Member
Dec 17, 2016
35
95
Huwa najiuliza kama ikitokea uchaguzi ujao akashinda Rais mwingine ndani ya Chama dola ama akitokea Chama cha upinzani. Alafu mtu huyu naye akaja na wazo la kuhamishia Makao makuu ya Tanzania kwenye mkoa anaoufahamu yeye kwa sababu zake mwenyewe. Je,atakuwa sahihi? Hili suala la kuhamia Dodoma linafanyika ili kumuenzi Mwalimu Nyerere ama linafanyika kwasababu linatakiwa lifanyike?
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,252
2,000

Tangu ametangulia jamaa mpaka leo kimyaaaa...
Kuishi ugenini bila mpango noma...
Naanza kuziona dalili za wahusika kusita kuhamia IDODOMYA
 
Kitikiti

JF-Expert Member
Nov 4, 2015
353
250
Mh. Rais yupo sahihi kusisitiza kuhamia Dodoma. Pia sababu za kuhamia ni za msingi. Tatizo watendaji na jamii inaonekana hawapendi mabadiliko mema. Kumbuka hata Wizara nyingi zilisikia na kutangaza kuhamia. Na zingine wakasema watakaa UDOM, mara usanii ukaanza kwa kuwatoa wapangaji wa nyumba za CDA ili waingie watakaokuja Dodoma. Wengine wakasema eti ndani ya siku chache tutahamia.

Leo, hamuuuuuunnnnaaaa hamuna kitu. Wote tupo Dar.

Hii ni sambamba na usafi wa mwisho wa sijui mwezi nao umeota mabawa, wakati Rwanda bado ni kusafi.

Mh. Rais ana nia njema, ila watendaji wana mng'en'gena. Ni waongo na wana msamifu. Nguvu na moyo wa uzalendo anayo mtu mmoja tu, wengine ni wabishi kugeuka.
 
H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,218

Sababu zilizoleteleza wazo hilo wakati wa Nyerere kweli bado zipo nyakati hizi za JF na Mitandao mingine mingi ? Enzi za kutuma barua kwenye gari ili ikadondoshwe kijijini iokotwe hadi kwa mhusika ilikuwa ndio chachu ya maamuzi. Bado tuna sababu kuntu kuhamia Dodona kwa rational thinkers ?
 
Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
2,000
Hii dhana kwamba rais ana nia njema na kwamba watu wengine ndiyo wanaomuangusha inathibitishwa kwa utafiti upi? Kama iko sahihi anashindwaje kuwaondoa hao watu aweke wengine wenye nia kama hiyo ya kwake?
Nadhani bado miongoni mwetu wengi tunaangalia filamu lakini hatuielewi. Hawa watu ni wanasiasa wa Kitanzania wanaotokana na mfumo na mazoea yaleyale ya miaka yote, usijidanganye kwamba huyu yeye ni tofauti.
Kimsingi, ukiangalia hali halisi je, unaona kuna uwezekano wa kufanikiwa kuhamia Dodoma kweli? Hii ni michezo yao ya kutafuta sifa za kisiasa majukwaani lakini hakuna chochote sababu siasa za majukwaani huwa hazina mipango zaidi sana ni lugha za kufurahisha umati tu.
Mh. Rais yupo sahihi kusisitiza kuhamia Dodoma. Pia sababu za kuhamia ni za msingi. Tatizo watendaji na jamii inaonekana hawapendi mabadiliko mema. Kumbuka hata Wizara nyingi zilisikia na kutangaza kuhamia. Na zingine wakasema watakaa UDOM, mara usanii ukaanza kwa kuwatoa wapangaji wa nyumba za CDA ili waingie watakaokuja Dodoma. Wengine wakasema eti ndani ya siku chache tutahamia.

Leo, hamuuuuuunnnnaaaa hamuna kitu. Wote tupo Dar.

Hii ni sambamba na usafi wa mwisho wa sijui mwezi nao umeota mabawa, wakati Rwanda bado ni kusafi.

Mh. Rais ana nia njema, ila watendaji wana mng'en'gena. Ni waongo na wana msamifu. Nguvu na moyo wa uzalendo anayo mtu mmoja tu, wengine ni wabishi kugeuka.
 
Mambaku

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
466
250
Hata historia ya inchi yako huijui. Kwa nini Dodoma ni makao makuu ya serikali. Fanya katafiti kidogo ujue. Nenda ka google basi kiongozi.
 
Mambaku

JF-Expert Member
Sep 11, 2016
466
250
Nchi Haina Vipaumbele Kwasasa, Tunaenda Tu Kwa Matamko Ya Mkuu
Mnaongea bila kutafiti. Kutokusoma kwako ndio kunakuaminisha inchi haina Mipango. Kamuulize hata mnyika ama mbunge yeyote atakuambia kila mwaka wanapitisha mpango wa serikali kwa mwaka husika unaoenda kuandaliwa bajeti na kuwasilishwa bungeni. Kila serikali inapoanza lazima iwasilishe bungeni mpango wa miaka mitano. Sasa wewe uko dunia gani. Kutokujua kwako ndio kunakuaminisha hivyo ama umejitoa akili
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,636
2,000
Huwa najiuliza kama ikitokea uchaguzi ujao akashinda Rais mwingine ndani ya Chama dola ama akitokea Chama cha upinzani. Alafu mtu huyu naye akaja na wazo la kuhamishia Makao makuu ya Tanzania kwenye mkoa anaoufahamu yeye kwa sababu zake mwenyewe. Je,atakuwa sahihi? Hili suala la kuhamia Dodoma linafanyika ili kumuenzi Mwalimu Nyerere ama linafanyika kwasababu linatakiwa lifanyike?
Limefanywa kukimbia harufu ya samaki na fujo za wavuvi na wateja wao pia kiusalama wanahisi Adui anaweza kuja na Nyambizi usiku akaleta hujuma kupitia baharini maana JWTZ hawana nyambizi ambayo ni gharama kuimiliki ndipo akaona bora aende Dodoma wapeleke misafara huko angalau foleni ipungue jiji Dsm ,lakini bajeti ya kuhamia Dodoma bado inawasumbua kwani pesa nyingi za maendeleo kapewa Lipumba azitumie kudhoofisha Ukawa na zingine wamenunulia ndege.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,636
2,000
watu waliamua kufungua mirija mingingine ili wazitumbue
Mkuu pesa za Dodoma zimepigwa kuanzia siku nyingi sana na CDA kila mwaka wa pesa ilitoka pesa ya kuijenga Dodoma tokea kipindi cha Nyerere mpaka awamu zote zilizofuata lakini pesa ilipigwa na Wajanja baada ya kugundua kuwa serikali hawakuwa tayari kuhamia huko,hata sasa Wajanja wameshapenya Dodoma dili lazima ziwepo watanzania ni wepesi wa kutumia fursa.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,090
2,000
Tatatizo mnaongea kama mpo kijiweni
Kuhamia Dodoma ni sera ya ccm tokea miaka ya 70.
Watu wanahamia kweli,juzi kuna mjomba wangu kaondoka rasmi jijini.
Nyie pigeni soga watu wapo kazini
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
12,914
2,000
Nchi Haina Vipaumbele Kwasasa, Tunaenda Tu Kwa Matamko Ya Mkuu
Mkuu wazo la kuhamia Dodoma ni la miaka ya sabini, pengine mimi na wewe tulikuwa hatujazaliwa.

Ni kipaumbele kilichokuwepo lakini urasimu wa wanasiasa na maslahi binafsi ya wachache yakachangia kisitekelezeke.
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,595
2,000
Mkuu pesa za Dodoma zimepigwa kuanzia siku nyingi sana na CDA kila mwaka wa pesa ilitoka pesa ya kuijenga Dodoma tokea kipindi cha Nyerere mpaka awamu zote zilizofuata lakini pesa ilipigwa na Wajanja baada ya kugundua kuwa serikali hawakuwa tayari kuhamia huko,hata sasa Wajanja wameshapenya Dodoma dili lazima ziwepo watanzania ni wepesi wa kutumia fursa.
mmhhh.... kaaazi kweli kweli
 
Lekachonka

Member
Dec 17, 2016
35
95
Tatatizo mnaongea kama mpo kijiweni
Kuhamia Dodoma ni sera ya ccm tokea miaka ya 70.
Watu wanahamia kweli,juzi kuna mjomba wangu kaondoka rasmi jijini.
Nyie pigeni soga watu wapo kazini
Swali langu limeelekezwa kutaka kujua kama ni mpango wa Taifa,Chama au Rais? Umejibu vyema kuwa ni mpango wa Chama toka miaka ya 70. Vp kitakapoingia Chama kingine madarakani na kikawa na wazo la kuhamishia mji mkuu wa Nchi labda Mtwara kutokana na sababu zao wenyewe. Haoa kama Taifa tumejipangaje? Nahisi suala hili lisingeishia kuwa wazo la Chama ama mtu mmoja(Rais). Kama linakubaliwa na wote basi liwe ni suala la Kitaifa.
Kwamfano unaweza angalia mambo yanayotekea Marekani kwa sasa...Obama sera yake kuhusu Mashariki ya kati inapingana na Trump, msimamo wa marekani kuhusu Iran wakati wa Obama tunauona wote unavyokwenda kushindwa chini ya Trump....mifano ipo mingi sana. Lkn kwa mfano..kwasababu suala la kupambana na Ugaidi ni sera ya Marekani (Taifa) na si chama ama Rais aliyepo madarakani.....wote wanasimamia kile Marekani inachoamini kuhusu ugaidi.
Nasisi kama Taifa ni lazima suala hili tulivushe kwenye level ya Chama..liwe la Kitaifa...ili hata Rais wetu huyu akishindwa basi tujue atakaye kuja bila kujali ni wa Chama gani lazima alisimamie.
Mfano mwingine tunaoweza jifunza ni suala la KATIBA MPYA...tumeona na kushuhudia mengi...lkn leo hii suala hili limesimama maana kuanzishwa kwake lilitokana na Utashi wa Rais aliyekuwepo madarakani.
Asante
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom