Safari ya Bara la Ulaya na Asia

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Habari za usiku mabibi na mabwana. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo wote humu ndani. Pia poleni sana kwa majukumu ya hapa na pale katika ujenzi wa taifa letu.

Wana JF, bila kupoteza muda ni kwamba 2007 mpaka 2014 nilipata nafasi ya kutembelea Baadhi ya Nchi za bara la Ulaya na Nchi za Asia.

Kama mjuavyo kuna msemo wa Kiswa hili unasema kwamba "mtu ambaye hajawahi kusafiri anafikiri/ anaamini kwamba mama yake ni mpishi bora" ( the person who has never travelled widely thinks/ believes that his or her mother is the best cook).

Kusafiri siyo anasa bali ni chanzo cha maarifa. Ukisari utakutana na mambo mapya yaani utamaduni wa watu fulani, watu wapya na utapata wasaa wa kujifunza mambo mengi sana.

Nikianza na safari yangu ya Bara la Asia hasa nchini India ambapo nilibahatika kujifunza kuhusu suala la utamaduni wao hasa katika utendaji kaji na suala la kujituma katika kazi kitu ambacho kipo tofauti sana na huku nchini kwetu.

Nchini za wenzetu watu wanajua kuthamini na kuheshimu kaza zao, wafanyakazi wana nidhamu kubwa sana katika katika, wanajua kujali wateja (they do really care their customers). Pia wanathamini na kuzingatia muda wao sana. Hawataki kupoteza muda wao.

Kadhalika utendaji kazi wao ni mkubwa sana ukilinganisha na wafanyakazi wa nchini Tanzania. Unapewa huduma iliyo bora na ya kiwango cha hali ya juu.

Aidha, katika utendaji kazi zao hasa Madaktari wana nidhamu na wanapenda sana kazi zao. Mfano ukiwa katika chumba cha matibabu muda wote umezunugukwa na wauguzi na madaktari. Kila chumba chao cha matibabu kina kengele ambayo ukigusa tu hiyo kengele utaona madaktari, wauguzi na viongozi wengine wanavyokimbizana kuja kuangalia kuna nini. Watakuja watakuzunguka wakikuuliza unataka nini n.k.

Kitu ambacho ni tofauti sana na hapa nchini kwetu ambapo madaktari, wauguzi, na viongozi wengine wana viburi, hawajali wateja wao, wana lugha mbaya kwa wateja wao, utendaji mbovu katika kazi, hawajitumi, hawazingatii maadili taaluma zao mfano hivi karibu katika hospitali kubwa tu hapa nchini walifanya kitu cha ajabu ambapo walisababisha mwana mama kupoteza maisha kwa sababu ya ujinga wa Madakatari wetu.

Ilikuwa hivi kuna mwana mama mmoja alienda hospitali kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. Katika kufanyiwa upasuaji wale Madaktari walikata utumbo wa yule mwana mama. Sijui ilikuwa ni bahati mbaya au ilitokana na uzembe wao.

Kilichofanyika ni kwamba baada ya kukata ule utumbo hawakushughulika tena na tatizo walilolisababisha bali walipotezea na wakamshona kidonda chake na kuacha ule utumbo ukiwa na jeraha kwa ndani. Kitu ambacho kilisababisha mwanamama kuoza utumbo na kupelekea kifo chake.

Kadhalika, nchi za wenzetu wanazingatia sana utendaji kazi, ujuzi na uwezo juu ya kitu fulani hawazingatii sana katika vyeti. Kwa upande wao certificates are just nothing. They don't really care about certificates. Wakati nchini Tanzania tunaangakia vyeti sana badala ya ujuzi na utendaji kazi. Ndiyo maana Leo hii tuna mainjinia wengi ambao wana vyeti vizuri tu lakini hawajui hata kuweka(fixing) kitasa cha mlango ila fundi wa kawaida toka VETA au mwenye utaalamu wake anauwezo wa kutengeneza hicho kitasa vizuri sana. Ila huyu fundi kwa ambaye ana uwezo na ufanisi mkubwa katika kazi atadharaurika kwa sababu hana cheti cha uinjinia. Kitu ambachi ni upuuzi mtu.

Wadau wa JF, kwa machache niliyoelezea hapo juu ni dhahiri kuwa ukitembea utajifunza mengi sana. Hata kama ulikuwa na kasumba fulani kichwani mwako hakika ukifika Nchi za wenzetu ukaona wanavyoishi hakika utabadilika sana. Mfano kwa upande wangu mimi huwa naamini katika utendaji na siyo vyeti kama baadhi ya watanzania wanavyoamini na kuthamini vyeti kuliko ujuzi wa mtu. Na ndiyo maana tu watendaji kazi wa hovyo sana nchini kwetu.

Aidha, Nchini Tanzania waajiri hawana exposure hata kidogo na ndiyo maana wanathamini vyeti kuliko ujuzi. Kadhalika badala ya kufanya practical interview wao wanapenda theory interview ambayo ni upuuzi mtu. Mfano dakatari anataka kazi mpe practical ya upasuaji, mpishi anataka kazi mpe chakula apike uone kama anaweza au la na siyo mahojiano yasiyo na tija.

Ahsanteni na karibuni kwa michango.
 
Mbona umeelezea nchi moja na sekta moja tu....nilitumainia ningepata mengi ya kujifunza kutoka baadhi ya nchi za asia na ulaya ka ulivyosema
 
Hao wahindi kwa idadi yao lazima wafanye kazi kama punda la sivyo watakufa njaa.

The good thing ni kwamba umeona utendaji wa kazi na wanatumikishwa kwelikweli sababu ya cheap labor just like China.

Masikini wa India sio wa bongo aisee. There is a big gap kati ya masikini na tajiri. Matajiri wao wanawatumikisha mno kwa ujira wa kishenzi sana. Ndio maana unaona matajiri wanazidi kuwa matajiri maana jamaa hawana utu hata kwa wahindi wenzao especially kama anatoka south India, I hope umenipata.

Sisi kinachotufanya tuendelee kuzubaa ni hii idadi ya watu versus ardhi na resources tulizonazo. Nchi kubwa na Ina kila kitu na bado hatujaweza kuexploit hata robo tatu.
 
Mkuu pamoja na hayo yote ila wanazingatia mambo yafuatayo:-
1. Utendaji kazi.
2. Nidhamu kazini hata kama analipwa mshahara mdogo.
3. Wanazingatia maadili ya kazi.

Aidha, napinga hoja yako kwamba wanafanyishwa kazi kama punda. Bali wale wanafanya kazi kwa kuzingatia na kuheshimu sheria zao za kazi. Ikitokea umefanya kazi zaidi ya masaa yaliyopangwa. Pia unalipwa sitahiki yako. Kitu ambacho ni tofauti kidogo huku Tz.

Huku Tanzania unaweza kupiga kazi zaidi ya masaa hayo na bado muaji wako akakuchukulia poa na asikulipe.
 
Napata mashaka kuhusu daktari kumpasua mama akakata utumbo kisha akaacha kama ulivyo bila kushona...ulikua sehemu ya tukio au ulisimuliwa....maana wakati mwingine watu ni wepesi kutupa lawama bila kujua ukubwa wa tatizo...sidhani kama kuna daktari anaweza fanya jambo kama hilo.
 
Mkuu ni ukweli mtupu. Sina nia mbaya ya kudanganya hapa kwa sababu she was my near relative.

Apart from that, pale Muhimbili 2015 if I'm not mistaken walishitakiwa kwa kosa la uzembe la kumfanyia mtu upasuaji wa kichwa badala ya kufanya upasuaji wa mguu ambao ndiyo ulikuwa na matatizo.

To be honestly fair, madaktari wengi wa nchini Tanzania hawana utulivu wala umakini katika kutenda kazi. BTW, I am not here to undermine your ability but that's the naked truth.
 
Mkuu pamoja na hayo yote ila wanazingatia mambo yafuatayo:-
1. Utendaji kazi.
2. Nidhamu kazini hata kama analipwa mshahara mdogo.
3. Wanazingatia maadili ya kazi.

Aidha, napinga hoja yako kwamba wanafanyishwa kazi kama punda. Bali wale wanafanya kazi kwa kuzingatia na kuheshimu sheria zao za kazi. Ikitokea umefanya kazi zaidi ya masaa yaliyopangwa. Pia unalipwa sitahiki yako. Kitu ambacho ni tofauti kidogo huku Tz.

Huku Tanzania unaweza kupiga kazi zaidi ya masaa hayo na bado muaji wako akakuchukulia poa na asikulipe.
Hao wahindi wanaletwa na wahindi wenzao tembelea hotel zao wanafanyishwa kazi hawaruhusiwi kuzoeana na mtu, na unakuta Hadi passport imechukuliwa na aliyemleta ili asikimbie kutafuta maisha.

Uliza
 
Hao wahindi wanaletwa na wahindi wenzao tembelea hotel zao wanafanyishwa kazi hawaruhusiwi kuzoeana na mtu, na unakuta Hadi passport imechukuliwa na aliyemleta ili asikimbie kutafuta maisha.

Uliza
- Wanawazuia kuzoeana na Watanzania kwa sababu wanaogopa kwamba tutawafundisha uvivu na tabia za wizi wizi na uongo uongo mkuu. Ngozi ile haipendi longolongo hata kidogo.

- Pia kwa tabia zetu zimesababisha tukose uaminifu kwao na ndiyo maana wanawaleta wenzao hata kwa kazi ambazo tunaweza kuzifanya.
 
Sisi wakazi wa kinyampuma, ngalaiwee, njari na mafyeko mbeya ,Tukiongozwa na Osia wa kwa mwasomola , Jirani yake Said mlina Tumbaku.
Tunasema hivi kila mtu abaki kwao na mazuri yao.
Vya mzungu vitakuvua nguo.

Na nyie mnasemaje......
 
- Wanawazuia kuzoeana na Watanzania kwa sababu wanaogopa kwamba tutawafundisha uvivu na tabia za wizi wizi na uongo uongo mkuu. Ngozi ile haipendi longolongo hata kidogo.

- Pia kwa tabia zetu zimesababisha tukose uaminifu kwao na ndiyo maana wanawaleta wenzao hata kwa kazi ambazo tunaweza kuzifanya.
Big NO
 
Back
Top Bottom