Safari ni ndefu. Angalia Barua hii

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Nimeondoa jina lake na chuo alichosoma...chuo kina jina kubwa sana na kipo hapa Dar

DIRECTOR/MANAGER
KAHAMA FM
P.O BOX
SHINYANGA
TANZANIA

DEAR SIR/ MADAM

RE: REF: APPLICATION FOR RADIO PRESENTER

Reference is made from the above mentioned tattle
Iam pleased to inform you that, Iam a bonafide citizen to the United Republic of Tanzania aged 24 years old, who currently is living her in dar-es-salaam.
I have pursued diploma education in journalism and mass communication at >>>>>>>>>>>college Tanzania in 2012 and awared certificate of diploma in journalism and mass communication.
I have a great honour to write this Application letter to your highly reputable organization applying for the post of RADIO PRESENTER because I have all requirements and Iam knowledgeable to work in this post for the organization development.
Hopefull I will work with all my effort together with your instruction as well as the office rule and regulation that will be given to me in every day tasks
I hope purposely attached a Curriculum Vitae [CV] as real verification of the above explanations given.
I hope my application will be consideration in positive manners and Iam looking forwarder from your Skillful Consideration.

YOURS FAITHFULL

………………………………
 
Mulugo ni mwalimu, tena akawa mwalimu mkuu, baada ya hapo akaanzisha (miliki) shule, na sasa ni waziri naibu wa elimu, je kweli elimu wanayoipata wanetu inawatosheleza kuhimili mikikimikiki ya soko la ajira (hasa challenges la sekta isiyo rasmi kama ujasiriamali na kujiajiri?)
 
alafu unakuta mtu kama huyu anaijua fitina hivyo akishaomba anakwenda na kimemo alafu analamba kazi. Sasa unatarajia atawajaza nini hao wasikilizaji wake!? Kazi ipo sio utani
 
Kuandika tu barua ya maombi ndio hawezi ila ana kipaji cha utangazaji mwenzenu, mkuu ungeweka na chuo ili kisaidie wengine wasije kukosea njia wakaingia hapo.
 
Mbona hicho kidhungu ni kizuri tuu kwa level yake ya diploma, kina kasoro ndogondogo tuu! kuna watu humu ndani na masters zao hawawezi kuandika kizungu hicho.msiponde sana nanyie hebu changieni kwa kizungu tuzione level zenu kabla ya kuponda wengine.Kingereza ni 2nd Language bana tusitishane.
 
Kweli ni hatari tupu na si jambo la mzaha! Juzi kati alinijia kijana mmoja na application yake ya kazi benki. Alikuwa anahitaji certification ya kopi za vyeti vyake. Katika CV ameonesha mie ni referee wake. Nikaisoma barua ya maombi ya kazi, loooo, sikuweza hata kuisahihisha zaidi ya kumuonesha jinsi gani haifai nikampa draft application letter aigizie na hapo hapo nikajieleza ni kwa nini siwezi kuwa referee wake.

Nilibaki najiuliza, mbona hata sie wa mwaka 47 tulisoma shule hizo hizo za kiswahili na kukutana na kiingereza sekondari? Shida iko wapi?
 
bujibuji mulugo alianzisha shule gani? unataka kusema anamiliki shule sio, maana ninachokijua mimi mulugo amekuwwa mwl. pale Southern Highland sec. Mbeya baada ya kumalizi form six kule Songea, na baadaye kuwa mkuu wa shule hiyo huku akisoma OUT na baadaye kugombea jimbo la songwe, kama si hivyo nieleweshe.
 
Wana JF,
Tuache haraka zetu, kijana huyu anabebeka. Kizungu ndiyo kina kasoro but Iam sure akikaa muda ni rahisi ku-gain na anaweza ku-improve kizungu chake. Jamani angekuwa ni mzungu kaandika broken kiswahili hata msingehoji ila kwa vile ni mswahili kaandika broken english midomo kama vuvuzela
 
Kweli ni hatari tupu na si jambo la mzaha! Juzi kati alinijia kijana mmoja na application yake ya kazi benki. Alikuwa anahitaji certification ya kopi za vyeti vyake. Katika CV ameonesha mie ni referee wake. Nikaisoma barua ya maombi ya kazi, loooo, sikuweza hata kuisahihisha zaidi ya kumuonesha jinsi gani haifai nikampa draft application letter aigizie na hapo hapo nikajieleza ni kwa nini siwezi kuwa referee wake.

Nilibaki najiuliza, mbona hata sie wa mwaka 47 tulisoma shule hizo hizo za kiswahili na kukutana na kiingereza sekondari? Shida iko wapi?

Wanafunzi wa miaka hii wanapenda njia za mkato. "Twishen" kwa sana! Ukiwapa vitabu vya kiada (textbooks), unapoteza pesa tu kwani hawavihitaji. Wanapenda kutafuniwa na kulishwa -- wao wameze tu!

Wanasoma ili tu wapate vyeti. Wanapenda kujua Kiingereza lkn hawapendi kujifunza! Funny! Wanataka kufika peponi lkn hawataki kufa!
 
Teh! teh! teh! They want to go to heaven but they don' want to die!! huyu alikuwa nani mkuu Peter Tosh au??
 
Back
Top Bottom