Safari na posho kwa wafanyakazi wa serikali zina wateule? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Safari na posho kwa wafanyakazi wa serikali zina wateule?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Inanambo, Jul 7, 2011.

 1. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  Wanajamii mie nashindwa kuelewa inakuwaje huku serikalini wafanyakazi wanaopewa Safari na Masurufu/posho ni wale wale tu kila siku. kuna safari ambazo ni technical kwa wenye fani fulani kuhudhuria semina au workshop nje ya kituo cha kazi hizo sina neno nazo. ila kuna zile ambazo kila mfanyakazi anaweza kufanya akitumwa lakini wakuu wamejenga mazoea kwa watu fulani kwa kuwa ni ndugu zao, wapenzi na marafiki waende wajiongezee kipato nje ya mshahara au kuosha macho. miaka inapita mfanyakazi ana miaka 30 kazini hajawahi hata kutumwa hapo kunduchi beach hotel akajipatia naye posho. kuna waliojenga na kununua magari kwa fedha ya safari wakati wengine wamejikatia tamaa ya kufanya kazi kwa sababu hawakumbukwi na wakubwa. pesa ya PIF ya mwaka 2004 wapo waliogawana mamilioni wengine wakaishia kupewa kozi ya siku 4 kwa gharama ya elfu kumi kila siku ikaisha. Pesa ya mafunzo ya UKIMWI kazini wamegawana wakubwa na kadhalika. naomba mniambie sisi tutatumwa lini nje ya kituo cha kazi na sisi tujue perdiem ya mfanyakazi ni shilingi ngapi. safari za majuu ndio usiseme hata kwa wasiostahili semina hizo hupelekwa tuu ili kuendeleza nepotism na loyality!
   
 2. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  unafanya kazi gani?
   
 3. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  kazi yangu afisa utumishi
   
 4. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  ombi lako limefika, ntalifanyia kazi. nipe miezi miwili utaanza kuona matokeo...ila usije kulalamika safari za mikoani zimekuwa nyingi
   
 5. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,147
  Trophy Points: 280
  nitashukuru sana bosi wangu angalau na mimi nione wenzetu wanafanya nini huko. maana majirani wamezidi kuniuliza wewe mbona hatujakuona umesafiri kikazi kama yule baba fulani ambaye hata waoto wanaanza kumsahau vile mara nyingi yuko nje ya ofisi na home kwake?
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  lol, sasa kwani hao wateule ina maana hizo posho wamezichoka!
   
Loading...