Saed Kubenea ataka wabunge wa UKAWA wenye wapenzi wao CCM wawasuse

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375

Sakata la wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson limefika pabaya baada ya baadhi ya wawakilishi hao kuanza kutowasalimia baadhi ya wabunge wa CCM.

Hatua hiyo ilikuwa dhahiri jana baada ya Ukawa kutangaza kuwa hawatashirikiana na wabunge wenzao wa chama tawala katika shughuli za kawaida za kijamii, kama vile michezo na kutumia kantini ya Bunge, wakisema wenzao wameanza kuwabagua.

Mbali na kitendo hicho, wabunge hao pia walitoka kimyakimya bungeni baada ya Dk Tulia kuingia, lakini safari hii hawakufanya mbwembwe za kujiziba midomo kama walivyofanya juzi.

Jana asubuhi, mbunge wa CCM Kangi Lugola alisema kuwa alisikitishwa baada ya kudai kuwa Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu), Lucy Magereli hakumjibu salamu yake wakati akiingia bungeni licha ya kumsalimia mara tatu na kuwa katika umbali mfupi wa kusikika.

“Kusalimia ni jambo la utamaduni wetu. Nilikuwa namsalimia mbunge wa kike wa Ukawa, lakini hakujibu. Lakini, nikajua ni sababu ya wao kufunga mdomo na plasta, nikamtania au kwa sababu ya plasta hujibu ili isije kudondoka hakuitikia,” alisema Lugola.

Alisema ameshtushwa na hali ilipofikia na hajui sababu za msingi za wabunge wa Ukawa kufanya vitendo hivyo, kinyume na udugu na utamaduni wa Watanzania.

Mbunge huyo machachari, alisema Kubenea alimziba mdomo Msigwa kwa mkono ili asizungumze chochote.
Naye mbunge wa Sumve (CCM ) Richard Ndassa alisema jambo wanalolifanya wabunge wa Ukawa siyo jema na halina tija kufanywa na wawakilishi hao wa wananchi.

“Sisi ni wabunge, hivi inapofikia kususa kuongea na wabunge wenzako, hatima yake nini?” alisema.
“Mimi nilienda kuwasalimia kama kawaida ambavyo huwa tunafanya kwa wabunge awe CUF, CCM au Chadema, sasa unavyosusa una maanisha nini,” alilalamika Ndassa.

Alisema kitendo cha kutosalimia ni cha juu sana na kwamba iwapo Ukawa wanashauriwa na mtu basi inawapasa kuchuja mambo mengine, likiwamo hilo la kuwasusa wabunge wenzao.
Juzi Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia wakati anawaongoza wabunge wa Ukawa kutoka bungeni aliwatuhumu wabunge wenzao wa CCM kuwa wanawabagua
Naye Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea alisema; “Leo tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.

“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”

Kubenea alisema hata katika mechi zinazoandaliwa kwa ajili ya timu ya wabunge UKAWA hawatashiriki katika kipindi hiki cha wiki mbili zilizobakia za bajeti.

“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea.

Mytake: Hoja ya wapinzani ni ipi sasa? Mbona wamepoteza mwelekeo ghafla? Huyu Kubenea ndiye aliyezua kuwa wabunge wa UKAWA wanawake wamevuliwa shanga na chupi. Sasa anataka kutuaminisha kuwa wabunge wameamua kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kazi yao ni kufanya ngono tu bungeni. Upuuzi huu hauvumiliki.

Source:
Mpekuzi
 
Sakata la wabunge wa Ukawa kususa vikao vya Bunge vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson limefika pabaya baada ya baadhi ya wawakilishi hao kuanza kutowasalimia baadhi ya wabunge wa CCM.
Hatua hiyo ilikuwa dhahiri jana baada ya Ukawa kutangaza kuwa hawatashirikiana na wabunge wenzao wa chama tawala katika shughuli za kawaida za kijamii, kama vile michezo na kutumia kantini ya Bunge, wakisema wenzao wameanza kuwabagua.

Mbali na kitendo hicho, wabunge hao pia walitoka kimyakimya bungeni baada ya Dk Tulia kuingia, lakini safari hii hawakufanya mbwembwe za kujiziba midomo kama walivyofanya juzi.
Jana asubuhi, mbunge wa CCM Kangi Lugola alisema kuwa alisikitishwa baada ya kudai kuwa Mbunge wa Chadema (Viti Maalumu), Lucy Magereli hakumjibu salamu yake wakati akiingia bungeni licha ya kumsalimia mara tatu na kuwa katika umbali mfupi wa kusikika.

“Kusalimia ni jambo la utamaduni wetu. Nilikuwa namsalimia mbunge wa kike wa Ukawa, lakini hakujibu. Lakini, nikajua ni sababu ya wao kufunga mdomo na plasta, nikamtania au kwa sababu ya plasta hujibu ili isije kudondoka hakuitikia,” alisema Lugola.

Alisema ameshtushwa na hali ilipofikia na hajui sababu za msingi za wabunge wa Ukawa kufanya vitendo hivyo, kinyume na udugu na utamaduni wa Watanzania.

Mbunge huyo machachari, alisema Kubenea alimziba mdomo Msigwa kwa mkono ili asizungumze chochote.
Naye mbunge wa Sumve (CCM ) Richard Ndassa alisema jambo wanalolifanya wabunge wa Ukawa siyo jema na halina tija kufanywa na wawakilishi hao wa wananchi.

“Sisi ni wabunge, hivi inapofikia kususa kuongea na wabunge wenzako, hatima yake nini?” alisema.
“Mimi nilienda kuwasalimia kama kawaida ambavyo huwa tunafanya kwa wabunge awe CUF, CCM au Chadema, sasa unavyosusa una maanisha nini,” alilalamika Ndassa.

Alisema kitendo cha kutosalimia ni cha juu sana na kwamba iwapo Ukawa wanashauriwa na mtu basi inawapasa kuchuja mambo mengine, likiwamo hilo la kuwasusa wabunge wenzao.
Juzi Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia wakati anawaongoza wabunge wa Ukawa kutoka bungeni aliwatuhumu wabunge wenzao wa CCM kuwa wanawabagua
Naye Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea alisema; “Leo tumekubaliana hatutashiriki katika michezo na wabunge wa CCM, hilo tumeanza leo asubuhi kwenye mazoezi katika viwanja mbalimbali, hivi sasa tunatafakari hata kutafuta uwanja wetu.

“Tukikutana katika uwanja mmoja, sisi tutatumia upande mmoja na wao watatumia upande mwingine, hatuchanganyani, hata salamu leo kuna mmoja kanisalimia nimekwepesha mkono wangu,”

Kubenea alisema hata katika mechi zinazoandaliwa kwa ajili ya timu ya wabunge UKAWA hawatashiriki katika kipindi hiki cha wiki mbili zilizobakia za bajeti.

“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea.

Mytake: hoja ya wapinzani ni ipi sasa? Mbona wamepoteza mwelekeo ghafla? Huyu Kubenea ndiye aliyezua kuwa wabunge wa UKAWA wanawake wamevuliwa shanga na chupi. Sasa anataka kutuaminisha kuwa wabunge wameamua kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kazi yao ni kufanya ngono tu bungeni. Upuuzi huu hauvumiliki.

Source: Mpekuzi
Wewe muimbisha taarabu wa TOT endelea na utunzi wa taarabu
 
13524492_1728692130719170_6580229536964216459_n.jpg
 
hivi ukawa napo akina livings... napo wapo
 
“Si katika michezo tu, hata katika mahusiano, tumekubaliana kama kuna wabunge wana mahusiano ya kimapenzi na wabunge wa CCM yasitishwe kwa muda wa wiki mbili mpaka tutakavyoamua vinginevyo,” alisema Kubenea.
Kubenea nafikiri analo tatizo fulani ambalo halijapata dawa.Kwa nini akiongea lazima aongelee mambo ya kike kike?

Mara ya kwanza aliongea kuwa sijui askari walikata shanga za wabunge wanawake sasa hivi anaongelea hili.Naanza kumtilia mashaka jambo fulani.

Akiongelea mambo ya kike unaona anapanda hadi jazba!! MHHHHHHHH
 
mie nilijua yatatokea haya, yanaanza taratibu, hata ubuyu ulianza kama mchicha, na bado mpaka watashinyama hata maji, sijui tunaelekea wapi na nashangaa wanene wanaangalia tu, haya tutafika
 
Kweli kabisa Mkuu. Inabidi UKAWA wampige ban ya kuongea maana kila akiongea anaharibu
 
mie nilijua yatatokea haya, yanaanza taratibu, hata ubuyu ulianza kama mchicha, na bado mpaka watashinyama hata maji, sijui tunaelekea wapi na nashangaa wanene wanaangalia tu, haya tutafika
Wameshindwa bungeni na sasa wanahamia mitaani
 
UKAWA wako sahihi kabisa. Huwezi kushirikiana na mtu anayehujumu demokrasia na maendeleo ya taifa hili. Tena itafika mahali hali hiyo itafika huku mitaani
 
Kubenea anapaswa kutufahamisha ni mbunge gani wa UKAWA ana mahusiano ya kimapenzi na mbunge wa CCM. Na je hayo ndiyo tuliyowatuma bungeni?
 
Mbunge anamchunia waziri halafu bunge likiisha anaenda ofisini kwake kumuulizia ahadi ya maji katika jimbo lake.

Kazi ipo ila kwa wabunge wa aina ya Kubenea wenye elimu ya hapa na pale tutegemee makubwa kuliko haya.
Kubenea na Mbowe wanawapelekesha wanavyotaka akina Ruth Mollel,Mbatia,Mnyika.
Mbatia mwenyekiti wa chama lakini utafikiri na yeye mfuasi wa Mbowe
 
Back
Top Bottom