Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika siku ya Jumatano umeazimia kupeleka wanajeshi nchini Msumbiji kukabiliana na kitisho cha usalama katika jimbo la Kaskazini la Cabo Delgado.
Hatua ya SADC inakuja baada ya vifo vya zaidi ya watu 3,000 huku wengine takriban 800,000, wengi wao wakiwa watoto, kulazimika kukimbia makazi yao tangu kuanza kwa machafuko mwaka 2017.
Baada ya Mkutano wa siku moja uliofanyika katika jijini Maputo, Katibu Mkuu wa SADC, Stergomena Tax amesema nchi 16 zimekubaliana kupeleka wanajeshi bila kutaja idadi ya wanajeshi watakaopelekwa, siku watakayopelekwa na majukumu watakayotekeleza, akibainisha kuwa lazima misaada ya kibinadamu iwafikie wale walio na uhitaji.
Makubaliano ya SADC yanamaliza mgogoro wa miezi kadhaa kuhusu hatua inayotakiwa kuchukuliwa kumaliza mgogoro, baadhi ya nchi wanachama kama Afrika Kusini wakitaka hatua za kijeshi huku wengine, akiwamo Rais Philipe Nyusi wa Msumbiji akipinga wanajeshi wa kigeni nchini kwake.
Mashambulizi ya magaidi wanaojiita al-Shabab yameongezeka siku za hivi karibuni, wakitajwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi duniani la ISIL. Serikali ya Msumbiji imepeleka maelfu ya wanajeshi katika eneo hilo, lakini wachambuzi wameonya udhaifu wa jeshi la nchi hiyo katika mafunzo na vifaa.
Chanzo: Al Jazeera