SADC: Ushindi wa kishindo CCM unapatikanaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SADC: Ushindi wa kishindo CCM unapatikanaje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Oct 28, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mwangalizi wa SADC ashangaa CCM inashinda kwa kishindo
  S


  Thursday, 28 October 2010 08:10
  Elias Msuya

  MWANGALIZI mmoja wa uchaguzi mkuu kutoka kundi la SADC ECF, jana alionyesha kushangazwa na taarifa kuwa CCM imekuwa ikishinda kwa kishindo kwenye chaguzi.

  Mwangalizi huyo, ambaye hata hivyo alikaata kujitambulisha jina na nchi anayotoka kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa waangalizi wa SADC, alisema hayo alipokuwa akiuliza swali katika semina kati ya waangalizi hao na vyama vya kiraia. “CCM ni chama tawala kwa muda mrefu hapa Tanzania, kuna kitu gani hasa imewafanyia Watanzania hata kiwe kinashinda hivi,” alihoji mwangalizi huyo. Sswali lake lilitokana na maelezo ya mwezeshaji wa semina hiyo, Mussa Billengeya kutoka katika asasi ya Ondoa Umasikini Tanzania, ambaye alielezea historia ya uchaguzi nchini tangu nchi ilipopata uhuru hadi sasa. Katika maelezo yake, alisema kuwa tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995, CCM imekuwa ikishinda kwa tofauti kubwa ya kura. “Ushindi wa CCM umekuwa ukiongezeka tangu mwaka 1995 hadi 2005.

  Mwaka 1985 ulikuwa wa asilimia 61, 2000 asilimia 71 na asilimia 85 mwaka 2005. Kumekuwa na malalamiko mengi kila baada ya chaguzi huku wagombea wachache wakionyesha kuridhika,” alisema Billengeya. Akijibu swali hilo, Billengeya alisema ushindi mkubwa wa CCM unawezekana kutokana na uelewa mdogo wa Watanzania na akatoa mfano kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wanadhani kuwa muasisi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere bado yuko hai. “Hilo ni swali gumu kwangu, lakini ni wajibu wetu kujiuliza CCM imetufanyia nini. Inawezekana ni uelewa mdogo tu wa kisiasa unaowafanya wachague chama walichokizoea kila wakati wa uchaguzi bila kujali kimefanya nini.

  Wapo hasa huko vijijini wanadhani bado Nyerere yuko hai,” alisema Billengeya. “Hivi karibuni nilikuwa Korea Kusini... ni nchi ambayo tulikuwa sawa miaka ya sitini hata kwa pato la taifa, lakini sasa Korea ni kati ya nchi 11 tajiri zaidi duniani, huku Tanzania ikiwa kati ya nchi 11 masikini zaidi duniani,” alisema. Akizungumzia masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Billengeya aliyataja kuwa ni udini akidai kuwa Wakristo wanaonekana kuwaunga mkono wagombea wa dini yao hali kadhalika Waislamu.

  Kuhusu usawa katika vyombo vya habari nchini, Billengeya alisema kuwa vyombo vinavyoendeshwa na serikali vimekuwa vikikibeba chama tawala huku mamlaka za serikali zikikemea vyombo vinavyoonekana kuandika habari za vyama upinzani. “Hivi karibuni tumeshuhudia gazeti la Mwananchi likipewa onyo kwa madai ya kuandika habari za uchochezi bila kutoa mifano ya habari hizo. Uongozi wa gazeti hilo uliwajibu kuwa hawajawahi kupata malalamiko kutoka kwenye vyama vya siasa, bado serikali ikasisitiza kuwa waache kuandika habari hizo,” alisema Billengeya.

  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alisema wakati akifungua semina hiyo kuwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi imewekwa kama hatua ya kupambana na rushwa. Tendwa alibainisha kuwa chama chochote kitakachoshindwa kuonyesha matumizi yake ya uchaguzi wa mwaka huu, hakitaruhusiwa kushiriki chaguzi zitakazofuata. Alisema kwa sasa nchi za SADC hazina sheria hiyo ndio maana amelazimika kuwafafanulia ili wajifunze. "Kama wataona upungufu, watatushauri lakini kama wataona ni nzuri wataiga kutoka kwetu,” alisema

  MY TAKE
  Katika zama izi haiwezekani ushindi wa CCM uwe unapanda badala ya kushuka.
  Kuna walakini apo most probably wizi wa kura za wapinzani.
  Its a shame kwa democrasia ya kweli kuwapokonya wananchi haki yao ya kuwa na kiongozi wampendae

   
 2. N

  Nyumbu- JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 969
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mwangalizi wa SADC ashangaa CCM inashinda kwa kishindo
  Thursday, 28 October 2010
  Elias Msuya


  MWANGALIZI mmoja wa uchaguzi mkuu kutoka kundi la SADC ECF, jana alionyesha kushangazwa na taarifa kuwa CCM imekuwa ikishinda kwa kishindo kwenye chaguzi.

  Mwangalizi huyo, ambaye hata hivyo alikaata kujitambulisha jina na nchi anayotoka kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa waangalizi wa SADC, alisema hayo alipokuwa akiuliza swali katika semina kati ya waangalizi hao na vyama vya kiraia. "CCM ni chama tawala kwa muda mrefu hapa Tanzania, kuna kitu gani hasa imewafanyia Watanzania hata kiwe kinashinda hivi," alihoji mwangalizi huyo. Sswali lake lilitokana na maelezo ya mwezeshaji wa semina hiyo, Mussa Billengeya kutoka katika asasi ya Ondoa Umasikini Tanzania, ambaye alielezea historia ya uchaguzi nchini tangu nchi ilipopata uhuru hadi sasa. Katika maelezo yake, alisema kuwa tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995, CCM imekuwa ikishinda kwa tofauti kubwa ya kura. "Ushindi wa CCM umekuwa ukiongezeka tangu mwaka 1995 hadi 2005.

  Mwaka 1985 ulikuwa wa asilimia 61, 2000 asilimia 71 na asilimia 85 mwaka 2005
  . Kumekuwa na malalamiko mengi kila baada ya chaguzi huku wagombea wachache wakionyesha kuridhika," alisema Billengeya. Akijibu swali hilo, Billengeya alisema ushindi mkubwa wa CCM unawezekana kutokana na uelewa mdogo wa Watanzania na akatoa mfano kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wanadhani kuwa muasisi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere bado yuko hai. "Hilo ni swali gumu kwangu, lakini ni wajibu wetu kujiuliza CCM imetufanyia nini. Inawezekana ni uelewa mdogo tu wa kisiasa unaowafanya wachague chama walichokizoea kila wakati wa uchaguzi bila kujali kimefanya nini.

  Wapo hasa huko vijijini wanadhani bado Nyerere yuko hai," alisema Billengeya. "Hivi karibuni nilikuwa Korea Kusini... ni nchi ambayo tulikuwa sawa miaka ya sitini hata kwa pato la taifa, lakini sasa Korea ni kati ya nchi 11 tajiri zaidi duniani, huku Tanzania ikiwa kati ya nchi 11 masikini zaidi duniani," alisema. Akizungumzia masuala yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Billengeya aliyataja kuwa ni udini akidai kuwa Wakristo wanaonekana kuwaunga mkono wagombea wa dini yao hali kadhalika Waislamu.

  Kuhusu usawa katika vyombo vya habari nchini, Billengeya alisema kuwa vyombo vinavyoendeshwa na serikali vimekuwa vikikibeba chama tawala huku mamlaka za serikali zikikemea vyombo vinavyoonekana kuandika habari za vyama upinzani. "Hivi karibuni tumeshuhudia gazeti la Mwananchi likipewa onyo kwa madai ya kuandika habari za uchochezi bila kutoa mifano ya habari hizo. Uongozi wa gazeti hilo uliwajibu kuwa hawajawahi kupata malalamiko kutoka kwenye vyama vya siasa, bado serikali ikasisitiza kuwa waache kuandika habari hizo," alisema Billengeya.

  Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa alisema wakati akifungua semina hiyo kuwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi imewekwa kama hatua ya kupambana na rushwa. Tendwa alibainisha kuwa chama chochote kitakachoshindwa kuonyesha matumizi yake ya uchaguzi wa mwaka huu, hakitaruhusiwa kushiriki chaguzi zitakazofuata. Alisema kwa sasa nchi za SADC hazina sheria hiyo ndio maana amelazimika kuwafafanulia ili wajifunze. "Kama wataona upungufu, watatushauri lakini kama wataona ni nzuri wataiga kutoka kwetu," alisema

  JIBU NI MOJA: CCM Wanaiba kura bila aibu.......
   
 3. LOGARITHM

  LOGARITHM JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Mh. NYUMBU, hilo ni jibu sahihi kabisa. Natamani wote wanaomsapoti JK NA CCM yake wangekuwa na UTASHI hata ROBO tu ya huyu muliza swali.
  Lakini aaaaaaaaaaaah......wote hao si riziki......hasara tupu! Ingekuwa ni mayai ya kuku, basi ni yale yasiyototoleka.

  TANZANIA MPYA.......FIKRA CHANYA...................UONGOZI MPYA.
   
Loading...