SADC ni Mkutano Mkubwa, Ugeni Mkubwa, Jee Mnaonaje Wana JF Tushiriki Kwa Uzalendo?, Tuzungumzie Mema na Mazuri Tuu Kuficha Aibu ya Mabaya Yetu?

Kaka Pascal Mayalla mimi sina baya kuhusu Tanzania ninalolijua, Nina mazuri tu.

Inasadikika Ngorongoro ndiyo ilikuwa Eden na mabaki ya Adam yaligundulika Olduvai George.

Sielewi ni kwanini hizi sehemu hazijawa sehemu za hijja.
Tanzania buana
1. Binadamu wa kale zaidi aligundulika Tanzania...ha ha ha
2. Ngorongoro inapatikana bustani ya kale zaidi

Kuna siku tutaambiwa hata ile nchi ya ahadi waliyoahidiwa waisraeli ipo sehemu ya Tz
 
Pascal jiepushe kuandika pumba. We ni gwiji la mwandishi was habari
Wanabodi,
Huu ni uzi wa wito wa Uzalendo kwa Mkutano huu wa SADC kwa tushiriki kwa kuonyesha Uzalendo. Kwa siku ya kesho na keshokutwa tuzungumzie mazuri tuu ya nchi nchi yetu na kuimba nyimbo za shangwe sifa na mapambio kwa viongozi wetu.

Uzi wenyewe una swali kuu la msingi kuwa SADC ni Mkutano Mkubwa, wenye Ugeni Mkubwa, Jee Mnaonaje Wana JF Tushiriki Mkutano huu kwa kuonyesha Uzalendo Wetu?, Tuzungumzie Mema na Mazuri Tuu Kuficha Aibu ya Mabaya Yetu kwa Wageni wetu?

Nakumbuka tukiwa wadogo, siku kukiwa na ugeni mkubwa nyumbani, kabla ya siku hufanyika fatiki ya usafi, kuondoa utando wa buibui, usafi wa hali ya juu, na sebule kupambwa kwa vitambaa vipya, cushions mpya, carpets na pazia mpya, watoto haturuhusiwi kukaa sebuleni tutachafua!, hata kula tutalia jikoni, dining ni wageni tuu.

Siku hiyo tatavalishwa nguo za sikukuu japo sio sikukuu tena hata soda tutakunywa maana enzi zile soda ni mpaka sikukuu au wakija wageni!.

Watoto tunafunzwa namna ya ku behave mbele ya wageni, kuonyesha heshima, adabu na unyenyekevu, hata kuongea kunabadilika inakuwa ni kwa sauti za chini na kunong'ona na sio kupiga kelele.

Hivyo natoa wito kwa wana jf wenzangu kwa siku hizi mbili za Mkutano huu wa SADC, tuweke mutatizo yetu pembeni, let's behave, kwa kuzungumzia mema na mazuri tuu ya nchi yetu, Mkutano ukiisha turudi kwenye normal ways zetu.

Mkutano huu umeleta ugeni mkubwa sana nchini kwetu haijapata kutokea, mfano hii ndio mara ya kwanza kwa mabalozi wetu wote wanaotuwakilisha nchi za nje, wamerejea nyumbani kuhudhuria Mkutano huu muhimu wa SADC.

Uwanja wetu wa ndege umejaa midege ya majet sijaona pangaboi, hotels zetu zinafurika wageni, hii ni midoleri inaingia, let's celebrate the gains despite kitakachojadiliwa mkutanoni.

Nawaombeni wana jf wenzangu kwa siku hizi mbili za Mkutano huu wa SADC, lets behave tuwe watoto wazuri, tuwe wazalendo kwa nchi yetu, tuache kelele, kulalamika na kuzungumzia shida zetu, tuzungumzie mema tuu mazuri ili kujenga picha nzuri ya nchi yetu mbele ya wageni, halafu tutaendelea na maisha yetu ya ki jf jf baada ya Mkutano huu kama ilivyo kwenye nyumba zetu hata kama baba na mama wamegombana na wamenuniana, akija mgeni watazuga kuongea ili mgeni asijue akishaondoka kununiana kunaendelea. Huu ndio Uzalendo wa ukarimu wa Kiafrika kwa wageni wetu.

Mnaonaje?

Namalizia kwa lile swali la mwanzo
SADC ni Mkutano Mkubwa, wenye Ugeni Mkubwa, Jee Mnaonaje Wana JF Tushiriki Mkutano huu kwa kuonyesha Uzalendo Wetu?, Tuzungumzie Mema na Mazuri Tuu Kuficha Aibu ya Mabaya Yetu kwa Wageni wetu?

Nawatakia Mkutano mwema.
Paskali
 
Yaani kuficha aibu kwa sababu ya wageni?Kwa nini tusiondoe hayo matatizo yanayosababisha aibu ?Acha aibu ionekane kama ipo.Maana ndo maisha yetu yalivyo.Mawazo yako hayapishani na wazazi wanaoficha vyombo vizuri kabatini eti mpaka waje wageni! Upumbavu gani huu jamani?Jamani binafsi hata sibadiliki kisa mkutano wa SADC Kama kuna matatizo acha wayaone,kama kuna maendeleo acha wayaone.
ni sawa na ile familia siku wanakuja wageni ndo choo kinasafishwa,vyombo vya chakula siku hiyo vinatumika vya udongo vilivyohifadhiwa kabatini kwa muda mrefu,hata watoto was familia hiyo hawavitumiagi bila wageni,majagi mazuri SKU hiyo yatatumika,glasses nzuri kwa ajili ya maji,yaani siku hiyo hata baba wa mji haamini kama pale ni nyumbani kwake,nyumba itang'aa siku nzima,watoto watakatazwa kuchezea sebuleni siku hiyo kwamba eti watachafua sebule,,,,,,,baada ya ugeni kale ka ustaarab kote kanawekwa kapuni,mazngra yanarud kulekule,uchafu,chakula kwny vyombo vya plastic, sebule inashinda chafu,,,,,,,je,huu ni ustaarabu,ujanja,ushamba,ulimbukeni au ujinga?????
 
Mie nafikiri Pasco kama gwiji la habari ungeshauri waandishi waende kuripoti habari za SADC wakiwa wamefunga plasta midomo yao au wana tisheti zimeandikwa Free Kabendera au We want our Azory ili jumuia ya SADC ielewe MNA matatizo makubwa wewe unataka wafiche machungu yao?
 
Yaani kuficha aibu kwa sababu ya wageni?Kwa nini tusiondoe hayo matatizo yanayosababisha aibu ?Acha aibu ionekane kama ipo.Maana ndo maisha yetu yalivyo.Mawazo yako hayapishani na wazazi wanaoficha vyombo vizuri kabatini eti mpaka waje wageni! Upumbavu gani huu jamani?Jamani binafsi hata sibadiliki kisa mkutano wa SADC Kama kuna matatizo acha wayaone,kama kuna maendeleo acha wayaone.
Haya mqmbo ya vyombo vizuri vinatoka kabatini siku kukiwa na wageni haaaa hakuna kwaninhao wageni ni wazuri wote wale wale tu
 
Ndo
Huenda sijaelewa, tukae kimya kwa muda tusiongelee vitendo vya utekaji na utesaji vinavyofanywa na wasiojulikana au kuhusu kesi ya mwandishi wa habari?
Yani tuonyeshe Uzalendo kwa kuacha lipi kati ya mabaya gani?
Au tusiongelee joto la Membe linalofukuta ndani ya CCM?
Kama kuna aliyeelewa anisaidie
Tumeshaongea
 
Kwenye mahotel yapi ndugu yangu? Wengi hao wamechukua apartment na wamelipa kwa mwezi tu. Ila wanakaa siku hizo 8 wanaondoka.
Kwa bahati mbaya tunajua huo mkutano hauna tija yoyote ya maana zaidi ya kutangazwa kwa hamasa. Ni kweli wenye nyumba za wageni na mahoteli watafaidika, lakini wageni kwa hapa Dar sio kitu cha ajabu. Hivyo sisi tunaendelea kupiga kama kawaida. Hamna mgeni anaingia jf, na hata akiingia atakutana na ukweli tu, tena ambao hawezi kuambiwa na yoyote hapo mkutanoni.
 
Pascal jiepushe kuandika pumba. We ni gwiji la mwandishi was habari
Uko sahihi maana ni suala la Uzalendo tatizo humu utaambulia matusi kutoka kwenye kikosi kilichozea pesa za deal ambacho kipo humu kwa Agenda moja tu kutukana kila jema analofanya Rais Magufuli
 
Mie nafikiri Pasco kama gwiji la habari ungeshauri waandishi waende kuripoti habari za SADC wakiwa wamefunga plasta midomo yao au wana tisheti zimeandikwa Free Kabendera au We want our Azory ili jumuia ya SADC ielewe MNA matatizo makubwa wewe unataka wafiche machungu yao?
Mwambie huyo msaka cheo mayalla
 
Yaani kuficha aibu kwa sababu ya wageni?Kwa nini tusiondoe hayo matatizo yanayosababisha aibu ?Acha aibu ionekane kama ipo.Maana ndo maisha yetu yalivyo.Mawazo yako hayapishani na wazazi wanaoficha vyombo vizuri kabatini eti mpaka waje wageni! Upumbavu gani huu jamani?Jamani binafsi hata sibadiliki kisa mkutano wa SADC Kama kuna matatizo acha wayaone,kama kuna maendeleo acha wayaone.

Unakuwaga mnafiki na mbwabwaji hata huelewi nn unataka!
 
Wanabodi,
Huu ni uzi wa wito wa Uzalendo kwa Mkutano huu wa SADC kwa tushiriki kwa kuonyesha Uzalendo. Kwa siku ya kesho na keshokutwa tuzungumzie mazuri tuu ya nchi nchi yetu na kuimba nyimbo za shangwe sifa na mapambio kwa viongozi wetu.

Uzi wenyewe una swali kuu la msingi kuwa SADC ni Mkutano Mkubwa, wenye Ugeni Mkubwa, Jee Mnaonaje Wana JF Tushiriki Mkutano huu kwa kuonyesha Uzalendo Wetu?, Tuzungumzie Mema na Mazuri Tuu Kuficha Aibu ya Mabaya Yetu kwa Wageni wetu?

Nakumbuka tukiwa wadogo, siku kukiwa na ugeni mkubwa nyumbani, kabla ya siku hufanyika fatiki ya usafi, kuondoa utando wa buibui, usafi wa hali ya juu, na sebule kupambwa kwa vitambaa vipya, cushions mpya, carpets na pazia mpya, watoto haturuhusiwi kukaa sebuleni tutachafua!, hata kula tutalia jikoni, dining ni wageni tuu.

Siku hiyo tatavalishwa nguo za sikukuu japo sio sikukuu tena hata soda tutakunywa maana enzi zile soda ni mpaka sikukuu au wakija wageni!.

Watoto tunafunzwa namna ya ku behave mbele ya wageni, kuonyesha heshima, adabu na unyenyekevu, hata kuongea kunabadilika inakuwa ni kwa sauti za chini na kunong'ona na sio kupiga kelele.

Hivyo natoa wito kwa wana jf wenzangu kwa siku hizi mbili za Mkutano huu wa SADC, tuweke mutatizo yetu pembeni, let's behave, kwa kuzungumzia mema na mazuri tuu ya nchi yetu, Mkutano ukiisha turudi kwenye normal ways zetu.

Mkutano huu umeleta ugeni mkubwa sana nchini kwetu haijapata kutokea, mfano hii ndio mara ya kwanza kwa mabalozi wetu wote wanaotuwakilisha nchi za nje, wamerejea nyumbani kuhudhuria Mkutano huu muhimu wa SADC.

Uwanja wetu wa ndege umejaa midege ya majet sijaona pangaboi, hotels zetu zinafurika wageni, hii ni midoleri inaingia, let's celebrate the gains despite kitakachojadiliwa mkutanoni.

Nawaombeni wana jf wenzangu kwa siku hizi mbili za Mkutano huu wa SADC, lets behave tuwe watoto wazuri, tuwe wazalendo kwa nchi yetu, tuache kelele, kulalamika na kuzungumzia shida zetu, tuzungumzie mema tuu mazuri ili kujenga picha nzuri ya nchi yetu mbele ya wageni, halafu tutaendelea na maisha yetu ya ki jf jf baada ya Mkutano huu kama ilivyo kwenye nyumba zetu hata kama baba na mama wamegombana na wamenuniana, akija mgeni watazuga kuongea ili mgeni asijue akishaondoka kununiana kunaendelea. Huu ndio Uzalendo wa ukarimu wa Kiafrika kwa wageni wetu.

Mnaonaje?

Namalizia kwa lile swali la mwanzo
SADC ni Mkutano Mkubwa, wenye Ugeni Mkubwa, Jee Mnaonaje Wana JF Tushiriki Mkutano huu kwa kuonyesha Uzalendo Wetu?, Tuzungumzie Mema na Mazuri Tuu Kuficha Aibu ya Mabaya Yetu kwa Wageni wetu?

Nawatakia Mkutano mwema.
Paskali

Hao wageni unaosema tufunike mabaya yetu kwa lengo lako kuu la "kuficha madudu" yetu, ndo hawa ambao nchi zao ni Zimbabwe, SA na nyinginezo? Zenye xenophobia? Zenye Kutesa raia zao na za nchi za wenzao kama ya kwetu?

Matatizo ya nchi hizi yanatakiwa yapewe kifurushi cha gb 2000 ili yasikike kila mahali kwa lengo la kupanua ugo wa uwezekano wa kuyatatua.

Waswahili ni ma-genius, walishasema mficha uchi hazai
 
Mtoto ukijua hata hao wageni waliokuja wana watoto watukutu basi utajifunza ustaraabu maana aibu ya nyumba yenu ni aibu familia yenu, hata ukiwambia wqgeni Leo tu tumekunywa soda, ili kumtia aibu baba yako, lakini mgeni mwenye akili atakuona wewe huna adabu, mlafi, mpenda sifa za kijinga, hata alifikilia kale kabinti kake afanye uchumba, utakasikia kwenye bomba. Wenye akili unapozunguza mabaya tu ya familia yako watakudharau, ingawa wewe utaongea kwa misifa ili wasikie mabaya ya familia yako, watakusikiliza kisha wanakung'ong'a kama mtoto uliyekosa adabu.
 
Back
Top Bottom