SADC and EAC what's better for Tz?

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,003
83
SADC has launched a Free Trade Area among his members, including Tanzania. wanasema makato ya kodi kwenye usafirishaji wa bidhaa umepunguzwa kwa asilimia 75% (kama nimekosea naomba mnirekebishe ili tujadili hii issue). so as for Tz, where is better to choose among these two blocks, sadc or East Africa community? wapi watz wana prefer zaidi?
 
SADC has launched a Free Trade Area among his members, including Tanzania. wanasema makato ya kodi kwenye usafirishaji wa bidhaa umepunguzwa kwa asilimia 75%(kama nimekosea naomba mnirekebishe ili tujadili hii issue). so as for Tz, where is better to choose among these two blocks, sadc or East Africa community? wapi watz wana prefer zaidi?

Mkuu kunalingine kubwa, wameweka mipango ya kuwa na sarafu moja baada ya miaka 10 yaani 2018. Yaani RAND ya South Afrika, Tsh na Z$ nk zote zinakufa na tunakuwa na sarafu moja. Hapo hapo EAC bado inasuasua.

Huenda ni maongezi tu ya maRais wetu baada ya kushiba pisa.
 
hivi sisi watz tunafaidi wapi kati ya EAC na sadc? wapi kwenye faida zaidi kati ya pande zetu hizi mbili?
 
hivi sisi watz tunafaidi wapi kati ya EAC na sadc? wapi kwenye faida zaidi kati ya pande zetu hizi mbili?

Inawezekana kote kukawa na faida, kwa maoni yangu. EAC, COMESA na SADC zote ni njia kuu za kuifanya Afrika ije kuwa chini ya ya muungano mmoja siku za baadaye. Kwa hiyo kila walalofanya, wanafocus Africa intergration bid.

Lakini udhaifu wa Tanzania kuwa EAC ni kuwa kwenye nchi nyingi zilizoko COMESA, na ambazo hazitaki kuheshimu uhuru wa Tanzania kuwa SADC. Kwa sababu zenyewe ziko COMESA, basi zinai bully Tanzania nayo iwe COMESA.

Pia, in terms of trading, Tanzania imekuwa zaidi ni soko la Kenya ambayo private sector ilianza siku nyingi, hivyo kutufanya tuwe koloni la Kenya kiuchumi. Kenya ina tatizo la kuwa dishonest inapokuwa kwenye maslahi, na hili linatokana na ukweli kuwa ina nguvu za kuichumi kuliko jirani zake. Kama kungekuwa na nchi nyingi zaidi kwenye block hii ambazo ama zingekuwa na nguvu au dhaifu, zingesaidia kuneutralize msimamo huu wa Kenya.

Unapopima mafaniko ya EAC, kumbuka pia kuwa kuna focus ya federation. Politically, nchi zote hizi zinatofautiana sana namna ya kutatua political upsets. Of all, Tanzania pamoja na matatizo yake, ndo the most stable one, na wananchi wake wana muundo wa ajabu wa kutatua matatizo yao.

Hii ina maana kuwa Over ambitions za watu kama Museveni inapokuja suala la urais wa EAC, na namna tatizo la akina Kony, tribalism kwenye politics both Uganda na Kenya, vinawaput off wengi wetu katika EAC.

Nikipata wasaa mzuri zaidi nitatafuta takwimu zinazofaa. Bado nadhani sijajiubu swali lako sawa sawa, lakini SADC ilianza kwa political thrust wakati ule ikiwa SADCC, na baadaye ikashift. SADC, kwa kuwa ina member wengi, maamuzi yake yamekuwa thabiti, japo nayo huwa inachemsha sehemu fulani. South Africa huwa inatoa mchango mkubwa kwenye SADC kwa kuwa inataka iwe zaidi ya rival wake COMESA. Na hii ni healthy situation.

Binafsi naona EAC kama utapeli mwingi, huku kila mtu akitolea macho resources za Tanzania. Kumbuka hata namna wazo la kuanzisha EAC lilivyochemshwa: from Up to bottom, badala ya bottom up. Ndo maana kwenye survey ya watu wanaotaka ku fast track federation, imeshindikana.
 
Nilivyofanya utafiti wa siku hizi mbili, naona kama watz wanapenda zaidi SADAC kuliko huu ukoloni wa Kenya na matatizo ya vinchi vingine.

Hivi, kama Tz itakataa kuendelea na fast truck ya EAC, au federation, halafu uganda kenya rwanda na burundi wakajiunga wao tu, sisi tutapata hasara gani? Je, hizi nchi zote hizi zina resources sawasawa? i mean, resources zilizoko Kenya na namna ya umilikaji wa ardhi nk, vivyo hivyo resources zilizoko uganda rwanda na burundi, najua hazilingani, tz ndo tajiri kuliko zote na ndo yenye eneo kubwa kuliko zote...je watz wameshaweka mikakati ya kwamba pale tutakapojiunga hasa kuwa federation, watz wetu watafaidika kidhabiti na utajiri wao huu? manake hatuwezi kufaidi pamoja na watu wa nje wakati wao huko kwenye nchi zao walishazila kwa pupa na hawana....., vinalingana?

Mbona naona kama tz ndo tajiri kuliko wote hapa na hivi vinchi vingine vya east africa vimegutuka na kuona kumbe bongo kule ulaji na wanataka waje wafaidi? kwanini hii fast truck haikuwapo kipindi cha nyuma wakat Tz utalii, madini, mafuta na gesi vilikuwa havijagunduliwa? Mimi naona, ni bora na sisi tuwafanye wenzetu makoloni yetu kwa kuwauzia raslimali zetu...yaani tuchimbe mafuta haya ambayo yamekuwa confirmed kwamba yapo, madini na tushindane kiutalii.

Kama hawataki, basi sisi tutalala mbele na sadc, tutafungua milango nchi hizi za kusini kama tulivyoanza kwa mozambique, malawi zambia na DRC, hadi South Africa kabisa kwasababu uwezo tunao na resources tunazo. Why hawa jamaa wanataka harakaharaka peke yao lakini watz hatutaki? Do they feel that they need us more than we need them? or we need them more than they need us?
 
Katika vyote jambo moja kubwa katika biashara ya kimataifa hasahasa linapokuja kwenye economic blocs kama ilivyo SADC an EAC ni Customs Co-operation. World Customs Union inazuia kabisa mwanachama wake kuwa kwenye Customs Union zaidi ya moja. Sasa tayari tuko kwenye EAC Customs Union na SADC ambition yao ni kuanzisha Customs Union yao, sijui tutafanyaje. Tukumbuke ni Tanzania tu ndio iliyo kwenye hizo blocs mbili (EAC na SADC). Kwa taratibu zilivyo nchi haiwezi kuwa kwenye Customs Union mbili au zaidi. Nina uhakika Tanzania italazimika kujitoa kwenye moja, ama EAC au SADC
 
Tukumbuke ni Tanzania tu ndio iliyo kwenye hizo blocs mbili (EAC na SADC). Kwa taratibu zilivyo nchi haiwezi kuwa kwenye Customs Union mbili au zaidi. Nina uhakika Tanzania italazimika kujitoa kwenye moja, ama EAC au SADC

Congo, kuna nchi kadhaa ziko kwenye SACU (Southern African Customs Union) na ziko SADC pia...na kuna nchi kama nne au tano ambazo ziko SADC na ziko COMESA pia. Licha ya mgongano wa utekelezaji, hakuna inayoamua tu kuacha ghafla. nyingi zina buy time kabla ya kuamua wapi waende. Tanzania iliamua 2000 kutoka COMESA na kubaki SADC. wakenya wanataka itoke SADC iingie COMESA, simply because wao wako huko.
 
Mbalamwezi, nchi zote zilizo SACU ziko pia SADC hivyo ni rahisi sana kuua SACU na ikawa intergrated SADC Customs Union. SACU wanachokifanya ni kupanua mipaka yao ya Customs Union tu. Halafu angalia hiyo speed ya hizo kambi mbili (SADC an EAC) katika kuamua mambo. Utadhani zinashindana. Ya kwangu macho.
 
Mbalamwezi, nchi zote zilizo SACU ziko pia SADC hivyo ni rahisi sana kuua SACU na ikawa intergrated SADC Customs Union. SACU wanachokifanya ni kupanua mipaka yao ya Customs Union tu. Halafu angalia hiyo speed ya hizo kambi mbili (SADC an EAC) katika kuamua mambo. Utadhani zinashindana. Ya kwangu macho.

Na sasa kuna msuguano sana kule south, maana nchi zilizoko SACU, ukiachia South Africa, zinaogopa hata mikataba na Ulaya ya EPA, na Customs UNion ya SADC, kwa sababu kwenye SACU kuna makubaliano ya malipo ya kufidia hasara ya mapato, kitu ambacho kwenye union zingine watazikosa.

Katika EAC, Tanzania imeona kuna kuburuzwa sana, hivyo imeweka ngumu baadhi ya mambo. Wiki hii Nairobi kutakuwa na mkutano wa ambao Tanzania inapeleka agenda zake za mambo kadhaa ambayo haitaki kabisa kuyatekeleza hadi isikilizwe inachoona yenyewe kina unafuu.

Kenya wakati huo inafikiria upya kama kweli inaweza kutekeleza makubaliano ya EAC juu ya standard marks za EAC. ambazo manufacturers wake wanasema too expensive to change, they cant afford.
 
Pia suala la sarafu moja TZ ingelivalia njuga litekelezwe kwanza kabla ya mambo mengine. Kenya inatake advantage ya ubora wa sarafu yao. Utashangaa wanataka uhuru wa kuhamahama kwani wanajua TZ kuna ardhi ya kutosha na bora. Hata EU iliona umuhimu wa kuwa na sarafu moja na Kenya inataka kucheza faul za waingereza kung'ang'ania sarafu yao.
 
napenda kupata mawaidha kutuka kwa jamii forum. Je ni nchi za kusini kama Zambia, Msumbiji, Malawi ndo wanatufaa watanzania kuunda nao community au hawa wenzetu Kenya, Uganda,Burundi, rwanda, na Uganda?

Ili kundi la pili mimi nina wasiwasi nao. Tulishaunda nao Ikafa. Ni Blood thirst mno.Tumeona wakiuwana wenyewe kwa wenyewe bila haya sembuse watanzania watatujali? Tumeona majambazi kibao wanaopora benki zetu ni wakenya.

Tumeona migogoro ya Ziwa victoria, mlima kilimanjaro na mbuga za serengeti, wezi wa mifugo mipakani Tarime n.k. Tumeona vile vile harakati zetu kusaidia Nchi za kusini mwa Afrika kupata uhuru.Tunajua pia muingiliano wa watanzania huko kusini wangoni, wamakonde,(mengine mtaje). Tunajua tunavyoishi nao bila mikwaruzo kwa muda sasa.Tumeona miundo mbinu Kama reli, barabara za lami daraja la mto Ruvuma na zikituunganisha na nchi za kusini.

Tunajua vile vile kuwa rasilimali nyingi tu za Tanzania kama vile, Gesi, makaa ya mawe,chuma, mafuta (inshallah), ardhi zenye rutuba mbuga za wanyama zinapatikana huko kusini. Kama ni kuongeza soko tu nadhani kusini tuna weza kuwaunganisha na masoko ya ulaya na asia kupitia bandari ya Dar es salaam kuliko East Africa ambapo bandari ya Mombasa inatoa ushindani mkali. Ni ipi iliyo strategic plan nzuri je ni kusini au north? Mimi ni mzaliwa wa north lakini hawa watu siwaamini.

Je ni lazima wao tu, hata baada ya kujaribu na kushindikana? Je ni kwa sababu ya kuwa koloni za uingereza au nini? kama taifa tufikirie tena.
 
nakubaliana na wewe EAC halitatusaidia sana kwani kwanza wote hapo maendeleo yetu ni yakusuasua sana...siasa zetu bado hazijatulia hasa burundi na rwanda..sina uhakika na amani yao...uganda anatumika sana na influence ya nje.
 
Sijali mambo ya EAC!Mtu wa kijijini shinyanga,Kigoma au Mtwara hafaidika na huu ujinga wa EAC.Ni bureacrats wa CCM,cost ya bunge la EAC hakuna chochote.
Nchi za Kenya,Uganda Rwanda na Burundi ni matatizo tu kwetu.

Wakenya wametuliza kwenye wizi wa mabenki.Angalia forgery kwenye UDOM!
Tunaweza kufanya biashara kati ya nchi na nchi ,lakini suala la kuwa karibu sana
nalipinga
 
Back
Top Bottom