Sadaka za Jumapili moja Ml 40-60, ubunge sh Ml 10 kwa mwezi, bora siasa ama Imani?

NewPage

JF-Expert Member
Mar 22, 2021
1,281
2,020
Askofu Mbunge hupata sadaka za kuanzia Ml 40 hadi Ml 60 kwa Jumapili moja. Amekuwa Mnafiki kwa sababu biashara anayofanya hataki kupoteza waumini wake.

Huyu hana tofauti na Kibwetere kwa sababu mahubiri yake ni mipasho na kutisha watu kuombewa hadi kufa.

Jumapili ijayo ni lazima atampasha Mbunge mwenzake Elibariki Kingu na kumtishia kifo! hii yote ili asipoteze sadaka.

Mapato ya Bishop Mbunge huyu kwa Jumapili baada ya kuingia bungeni yaliongezeka sana na kumfanya ajitahidi kubalance kote.

Akipoteza ubunge na mapato yake ya Jumapili yatapotea au kupungua sana. Anacheza na siasa na imani za watu papo. Mjanja sana Bishop Mbunge huyu.

Wanasiasa wameanza kumshtukia - sasa tuone atakujaje Jumapili.

Lakini pia - wabunge nao kwa unafiki wao wameamua kumwadabisha na Jerry Silaa ili wasionekane na double standard - Jerry Silaa hapa ametoka HERO wetu.

Eti Elibariki Kingu unadai Jerry ataenda kumwomba msamaha Ndugai - msamaha gani sasa wkt wameshamwadhibu? Sisi tunajua JS ndiyo mwakilishi wetu wa kweli ni shujaa wetu kati ya wabunge wote wa sasa!

Elibariki Kingu ninavyokufahamu! hebu kiri tu kuwa umemnafiki Spika Ndugai kwa kujaribu kumwonesha indirectly kuwa JS yupo sahihi.

Haya wawakilishi wetu - endeleeni kula miposho hiyo isiyokatwa kodi ambayo ni kodi zetu 100%!
 
Back
Top Bottom