Sadaka na zaka za kwenye nyumba za ibada zitozwe kodi

DUMU

JF-Expert Member
Sep 23, 2019
431
577
Mimi ni mzalendo naipenda nchi yangu toka moyoni mwangu na si kwashawishiwa na mtu yeyote .kwakuwa ni mzalendo wa kuzaliwa naomba niwashauri mamlaka ya kodi yaani TRA kuanzisha utaratibu wa kukusanya kodi toka kwenye hizi nyumba za ibada kwa kila misa ama swala ambayo hufanywa na kiongozi wa dini husika. Kwani tumekuwa tunapoteza mapato mengi kama serikali kushindwa kukusanya kodi kutoka kwenye hizo taasisi husika.

Jambo la kufanya ni kutoa maelekezo kwa uongozi wa kidini kutoa taarifa ya ni lini muda gani ibada itafanyika ili mamlaka ya kukusanya kodi itume muwakilishi wake sehemu husika ya tukio ili kodi ukusanywe kikamilifu.

Hizi hela ambazo serikali imekuwa ikiwaachia hawa viongozi wa dini bila kukata kodi wamekuwa wakizitumia kwenye masuala yasiyo ya manufaa kwajamii kwa mfano viongozi wengine wa dini wamekuwa wakizitumia hizi hela kugombanisha ndoa za watu kwa kuingilia mapenzi ya wandoa kwa kuzini na mmoja wa wanandoa kwakutumia hela tunazotoa kama sadaka ama zaka.

Pia wengine wamekuwa walevi wa pombe kupindukia huku wakiiacha jamii waliojitolea hizo hela wakiwa na maisha duni.

Kwakuwa serikali yetu ni sikivu tunaomba wakusanye hizo hela ili watuletee maendeleo kama tuliyoyaona kwenye serikali ya awamu ya tano.

Hongera uongozi wa awamu ya sita kwa kuendelea kukusanya kodi kwa ufanisi mkubwa ili mtuletee mandeleo endelevu kama tunayoyaonda yakifanyika Chato basi kwa hela hizi mtakazokusanya kupitia taasisi za dini mkajenge Tanzania ya kisasa.

Kwa kumalizia katika kufanikisha hizi hela kutoka taasisi za dini zinakusanywa ipasavyo kwa wale wasiotaka kuhudhuria kwenye ibada siku husika serikali iwatoze kodi kubwa mara zaidi ili kuhasisha watu kupenda ibada na kumtumikia Mungu wao huku wakitoa sadaka na zaka kwa maendeleo yao.

Naomba viongozi wa dini mtakaolisoma andiko hili mniunge mkono kwa kuishauri serikali ukusanye hela toka kwenye taasisi zenu ili tupate maendeleo ya jumla kwa haraka kupitia serikali yetu hii ya awamu ya sita.

Kwa pamoja tunaweza hapa kazi tu, kasi zaidi maendeleo zaidi. Mitano tena. Songa mbele jembe kwa pamoja tulitumikie Taifa letu kupitia Mungu wetu.
 
Yule mjinga asiye na hakili, akisikia haya mapendekezo, amini kesho kutwa utaona tangazo😆😆😆Tanzania tunaongozwa na wazr wa Ujenzi, hatuna rais mpk sasa tangia yule mzee aondoke.
 
Hakuna sababu yoyote ya kutoza sadaka kodi.
Kodi ni hela zetu tuna mamlaka nazo kuzitumia. Ila ukishatoa sadaka ama zaka zile hela huna mamlaka nazo kuzihoji ndiomaana ugomvi kwenye baadhi ya taasisi za kidini ni mkubwa kisa hela tulizo wapa ni nyingi tena hazina kodi.
 
Umaskini hauhishi KWA kutoza kila jambo Hadi vijambio kodi aisee. Kodi zimezidi huku maisha yakiwa magumu zaidi
 
Kodi ni hela zetu tuna mamlaka nazo kuzitumia. Ila ukishatoa sadaka ama zaka zile hela huna mamlaka nazo kuzihoji ndiomaana ugomvi kwenye baadhi ya taasisi za kidini ni mkubwa kisa hela tulizo wapa ni nyingi tena hazina kodi.
Ukitoa sadaka unatoa kulingana na imani yako ya kidini. Kodi ni suala la kisheria. Usalama wa taifa hauwezi ruhusu ilo swala ni hatari kwa uongozi wa nchi. Kuna sababu ya kutenganisha dini na siasa miaka mingi nyuma, hazikutenganishwa tu bila sababu.
 
Kodi ya kwenye nyumba za ibada hazituathiri sana sisi waumini badala yake itakuwa neema kubwa sana kwetu. Fikiria kwa wiki zinakusanywa shilingi ngapi kwenye nyumba za ibada. Hivo serikali ikifanikiwa kwa hili ndani ya mwaka mikopo ya mabeberu bye bye na mtaani ni full mafy-over nchi nzima
Utitiri wa Kodi kila corner sio solution ya kuondoa umaskini ka hujaboresha uchumi. Sadaka ni mambo ya kidini na serikali haingii huko. Tumeona mikodi ikizidi Hadi ya birthday umaskini umeisha?
 
Back
Top Bottom