Sad news kwa watanzania...umaskini si tunautaka wenyewe kweli?

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
WANAFUNZI WAWILI WA KIDATO CHA KWANZA WAACHA MASOMO NA KUAMUA KUOANA.



Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. Abbas Kandoro
*****
Na mwandishi wetu.
Wanafunzi wawili wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Sange iliyopo kata ya Sange wilayani Ileje wameacha masomo na kuamua kuoana ambapo hadi sasa wanaishi kama mume na mke.

Hayo yamebainika baada ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro kufanya ziara maalumu ya kujitambulisha wilayani humo ambapo pia alitembelea kujionea hali ya ujenzi wa shule ya msingi Sange.

Akiwa shuleni hapo Kandoro alielezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Lugano Mwambuja kuwa wanafunzi Joshua Kijalo na Acheni Tete waliacha masomo mwezi Julai mwaka huu na kuamua kuishi maisha ya ndoa.



Mratibu Elimu wa kata hiyo, Joseph Mwanzela amesema wanafunzi wameacha masomo kwa sababu za kiuchumi, ambapo watoto wa kike huamua kuacha shule na kwenda kufanya kazi za ndani mijini wakati wavulana hukimbilia kufanya kazi za mashambani.


Kutokana na taarifa hizo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abasi Kandoro ametoa agizo kwa viongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha watoto hao wanapatikana na kurejeshwa masomo pamoja na wazazi wa watoto hao kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na kushindwa kuwadhibiti watoto wao kufuata masomo.

source:http://mbeyayetu.blogspot.com/2011/11/wanafunzi-wawili-wa-kidato-cha-kwanza.html?spref=fb


 
Sasa wazazi wao wachukuliwe hatua kwa lipi, kama maisha magumu sasa waibe ili wachomwe moto, Kandoro na wewe unaanza kufulia kimawazo mimi nilitegemea unasema unawarudisha shule na serikali itawalipia ada tena wazazi walioshindwa waendelee naona hapo ulichofanya sawa sawa na hakuna. Serikali imekufa na imeua uchumi na wananchi sasa hawawezi hata kuendesha maisha yao. Yaani hii serikali basi tu, ningekuwa na uwezo ningeingamiza yote any way Mungu atuhurumie
 
Mawazo mganzo wazazi wachukuliwe hatua kwa lipi
kama wazazi wanakosa hata pesa ya kununulia chakula cha siku hiyo ya ada itatoka wapi
mkuu sio kwamba umaskini watu wanautaka ila huko vijijini ohali ni mbaya mno
uwezo wa kupata msosi wa siku ni issue sembuse kupata ada ya shule
bora hata hao wameoana wakapambane na maisha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom