Sackur: Good to see my interview with Tundu Lissu has stirred passionate debate!

Itachukua muda mrefu sana kwa watz kuelewa propaganda na namna zinavyofanywa. Mnadhani ni bahati mbaya Lissu kwenda kuhojiwa hapo BBC, tena HardTalk? Clue: Mataifa ya magharibi yanajua kwa undani kinachoendelea Tanzania. Hawamuhitaji Lissu kujua yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika (hili hata Lissu kaligusia kwenye interview). Kwa kifupi wenzetu wapo mbele sana kwenye kukusanya intelligence.... zaidi kwa faida yao.

Kama mnatizama hiyo interview kama ni ya Lissu tu, mnapotea sana. Jiulizeni "agenda" iliyopo nyuma ya mahojiano hayo na hasa maswali yaliyoulizwa.
Point yako ni nini sasa? Kwamba lisu anatumika tu kama kisemeo siyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni mazoea kwa hawa wanasiasa wanaoshinda kuchangia kwenye mitandao ya kijamii au kwenye audiences ambazo watasifiwa tu; matokeo yake wengi ni wavivu wa kujenga hoja (that is kuweza kuja na evidence) or at least being able to produce convincing deductive arguments to back their claims.

BBC kama taasisi moja ya nguzo yake ni kuwa impartiality (na wanakaguliwa by regulators), isitoshe wananchi pia wanaweza peleka malalamiko yao kuhusu kipindi kama kilikua cha upande mmoja; na audience ya 'Hard Talk' ni ya wasomi wanajua mbivu ni mbichi maswali ya Sacur yalilenga kupata details zaidi ya hoja kutoka kwa Lissu kujenga dhana anayotaka iwasilisha.

Tatizo Lissu mwenyewe ni mwanasiasa wa Tanzania kwa uelewa wa audience zetu many get away easily kwa hoja nyepesi sana wakati ukitoka nje ya bara ni hoja weak sana kwa standards zao. If anything ata kwenda kumtwanga risasi kwa sababu ya makelele yake ya MIGA sijui nini wakati kiualisia hakuna mtu kwenye dispute ataanzia huko wakati anataka kulinda siri ya mkataba wake wa kinyonyaji ni yale yale ya Lissu kwa upande wa usalama uelewa mdogo wa mambo hakukuwa na sababu.
 
SAFI SANA TUNDU THE GREAT! Kwa alichoandika MTU maarufu Stephen sasa kila media kubwa itatamani kufanya mahojiano na Lissu maana hata lugha anaeleweka sio mambo ya "intaperenyuwa'.
Na kuonyesha hamkufuatilia mauzui ya mahojiano nyie mliangalia muonekano wa nywele tuu.
Ingekuwa dunia akili ni hizo za Lumumba basi Trump na wa Korea isingekuwa kujadili nyuklia bali kiduku cha jamaa!
Akili za Intaperenyuwa utazijua tuu. Mjadala kujadiliwa ujue uko hai sio mjadala mfu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna freedom of expression mbona Snowden na Assange ni wakimbizi? Kama kuna freedom of expression mbona trump anawaita feki news kila siku?
Weee maandazi " snowden ni jasusi aliyekula kiapo cha kutunza siri za usalama wa taifa lake ... so inapo tokea akazitoa siri hizo ni lazima awajibishwe .... ila sio mwanasiasa " mwana siasa " haswaa mpinzani yupo kwaajili ya kuikosoa serikali dhidi ya utendaji wake mbaya " ili iweze kurudi kwenye mstari mnyoofu " na wananchi waweze kupatiwa haki zao ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjadala kuhusu mahojiano ya Tundu Lissu katika kipindi cha Hard Talk umekuwa moto kwenye mitandao ya kijamii kiasi cha kupelekea mwendesha kipindi hicho, Stephen Sackur kupata mentions za kutosha mpaka akalazimika kutoa neno;

"Nimefurahi kuona mahojiano yangu na Tundu Lissu yamesababisha mjadala murua"

View attachment 1001613

Mtangazaji wa BBC anayeongoza kipindi maarufu cha mahojiano cha HardTalk, Stephen Sackur, ameitoa kauli hiyo kupitia mtandao wa Twitter mapema leo ikiwa ni saa chache kupita tangu kuruka hewani kwa mahojiano yake na Tundu Lissu nchini Uingereza.

Kufuatia mahojiano hayo, mjadala mkali umeibuka baina ya pande mbili ambapo kuna wanaodhani Tundu Lissu ameshindwa kuyajibu ipasavyo maswali magumu ya Stephen, huku wengine wakisimamia kwamba Lissu ametumia vizuri fursa hiyo kueleza kwa undani sakata la yeye kushambuliwa na risasi na kueleza kuwa Serikali inahusika moja kwa moja na tukio hilo.

Hiyo ndiyo nguvu ya mitandao ya kijamii. Watanzania wametisha sana!
Nimeipenda retweet ya huyo bwana Ngomakisi The 3rd hapo juu. Wapinzani wameumuliwa hakika. Teh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom