Sabodo unatakiwa kumuiga Dr Mengi ili upewe sifa sahihi !!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo unatakiwa kumuiga Dr Mengi ili upewe sifa sahihi !!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by greenstar, May 5, 2012.

 1. g

  greenstar JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pongezi za dhati kwa Dr.MENGI kwa kujikita katika kusaidia jamii bila ubaguzi wa kidini,kisiasa,kikabila na kikanda ndiyo maana leo hii unatambuliwa na asasi mbalmbali za kimataifa na kupewa tunzo stahiki kwa mchango wako.

  Napenda ndugu SABODO aige mfano huo kama kweli anamapenzi ya dhati katika kutoa misaada yake kwa CHADEMA, pia na wafanyabiashara wengine watoe misaada yenye tija kwa jamii badala yakutaka kusifiwa tu na vyombo vya habari na kutajwa tajwa ovyo kwenye miziki ya dansi a.k.a SIFA za KIJINGA.
   
 2. S

  Small Master Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona alipokuwa anatoa CCM hamkupiga kelele? kwani jamii haikuwepo?, mbona hujamwambia Manji naye atoe kwenye jamii?
   
 3. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,854
  Likes Received: 4,235
  Trophy Points: 280
  Why do people help, it's too psychological, the reasons can not be generalized, kwa hiyo Sabodo na Mengi kila mmoja ana sababu zake za kusaidia na mahali pa kusaidia
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ungejiuliza mpaka sasa CHADEMA imewasaidia vipi Watanzania? Hapo ndo utaujua umuhimu wa Sabodo kuisaidia au kutokuisaidia Chadema
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hili ndio jibu sahihi kabisa,nimeipenda saaaaaana hii Comrade na ndio maana unadreem na unasound na upo CDM
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Mengi anaposaidia wasiojiweza na misaada mingine ya kijamii anapenda aonekane na ndio maana utumia vyombo vyake vya habari kutangaza hayo kwa muda mrefu lakini pia ukae ukijua Mengi utoa misaada mingi na mikubwa kwa CCM ambayo haionyeshwi kwenye vyombo vya habari. Pia SABODO hana nia ya kupata tuzo kwani lengo lake ni kusaidia ukombozi wa nchi hii na ndio maana anasaidia chama ambacho anaona kitalikomboa taifa hili na taifa likikombolewa hata umasikini utapungua na hao wanaosaidiwa na Mengi wataweza kujisaidia kutokana na mfumo mzuri wa kiutawala utakaoletwa na CDM
   
 7. g

  greenstar JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina tatizo na misaada yake kwa CHADEMA ,lakini imekaa kinafiki na sifa za kijinga ati yeye ni KADA wa CCM??????????? kwa hiyo CCM ndiyo sehemu yakupatia ujiko? ajiunge na CHADEMA ili tuweza amini hana ajenda za NDUMILAKUWILI...Nitaishauri kamati kuu ya CCM imfukuze uanachama kama hataamua kwa hiari yake.

  Inakuwa vigumu kuamini kama huyu SABODO ana nia njema na CCM au anataka kuwagombanisha viongozi wake? DSM kuna tatizo SUGU la MAJI lakini hajachimba visima,kuna wagonjwa pale MOI hawana fedha za kulipia wakisubiri msaada toka SERIKALINI...lakini yeye ana PESA zakutosha kwanini asisaidie maeneo hayo pia anaweza kuwasiliana na vyombo vya habari vikamtangaza badala yakutumia mikutano ya CHADEMA.....Mh.SHIBUDA mnasema ni mnafiki ,Je huyu SABODO kwenu ni mtu safi???????? hata NYIMBO naye ni msafi kwenu???????????????

  NDIYO maana CHADEMA haitatawala kamwe kama inafanya mipango ya kubeba screpper za CCM...kwani watu makini ni hazina ya CCM...Mabadiliko ya kweli yamewadia.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watu bwana SABODO akiisaidia CDM amewasaidia watanzania wengi kuliko ata Mengi ambaye huwalisha menu wale ndugu zetu pale Diamond na vimichango vya apa na pale ambavyo huishia DSM most of the time.
  Chain impact ya msaada wa SABODO ni kubwa jamani huwezi fananisha na Mengi.
  Popote ambapo M4C imefika ni kwa hisani ya uyu mzee in one way or the other
   
 9. n

  naroka Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na hivi visima vya maji anavyochimba Sabodo zaidi ya 800 nchini,ni vyake vya CHADEMA au wananchi!!?
  :israel:
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  As far as I am concerned Mzee Sabodo ametoa mchango mkubwa kwa taifa hili kuliko Mengi. Mchango wa Mzee Sabodo unalenga kurekebisha mfumo wa utawala (siasa), mfumo ambao ndio chanzo cha umasikini wa watu wanaolishwa na Mengi! Anachofanya Mengi ni kumpa mtu samaki, lakini Mzee Sabodo anampa mtu nyavu ili avue samaki leo na kesho.

  Hakuna mtu anayependa kuunga foleni ili apate sahani ya ubwaba (tena kwenye camera) lakini wanafanya hivyo kwa kwa sababu mfumo tulionao unageuza watu ombaomba. Mengi anatakiwa amuige Mzee Sabodo kwa kuchangia mabadiliko ya mfumo.
   
 11. n

  naroka Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kweli tupu!!!
   
 12. W

  Wenger JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Greenstar wewe unachuki binafsi na chadema nimekusoma jinsi unavyo mponda nyimbo anavyohamasisha ukombozi njombe wewe hupendi kwavile ni gamba unaona faraja kuendelea kupewa TShs 3000 na kofia, hofu yako pia sabodo ataijenga CDM na magamba watakuwa na wakati mgumu.
  Nadhani hata elimu yako itakuwa duni sana kama unaona watu kama Jahi people wamaana na Bibi Kidude kweli wewe mchovu.
  Sabodo anafanya kazi kubwa sana kuimarisha ukombozi wewe baki kuwa gamba usubiri kupewa kofia na buku 2
   
 13. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,486
  Likes Received: 477
  Trophy Points: 180
  Sabodo ni zaidi ya Mengi katika suala zima la kusaidia, hizo hela anazowapa CDM ni ndogo mno katika misaada yake. Sema siyo mtu wa kujitangaza na siyo mnafiki aliposimamia huwezi ukambadilisha kwa misifa ya kijinga. Hana shida ya tuzo na haihitaji kubebwabebwa katika biashara zake.
   
 14. M

  Moony JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si sahihi kusema hivyo.
  Kama ni sifa za kijinga jinga labda ungemsema Mengi. Kuwapa vyakula walemavu si njia ya kuwasaidia. Angejenga VETA moja ama chuo ama anything tangible amabayo ni long lasting kama SABODO afanyavyo. lakini lengo la Mengi kama ulivyosema ni kupata SIFA STAHILI.
  Sabodo sidhani kama anataka masifa unayotaka ayatafute.
   
Loading...