Sabodo: Sina mpango wa kuhama CCM; Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo: Sina mpango wa kuhama CCM; Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  THURSDAY, 20 OCTOBER 2011 19:27 NEWSROOM


  * Awakana CHADEMA, awaonya Watanzania

  MFANYABIASHARA maarufu nchini, Jaffer Sabodo, amesema hajahama na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho amekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40.

  Sabodo alisema baadhi ya kauli kali ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya CCM, hazina maana kuwa anaichukia, isipokuwa zinalenga kukikosoa Chama ili kiendelee kuwa imara katika kuwaongoza Watanzania na kuharakisha maendeleo yao. Hayo aliyasema jana alipozungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati nyumbani kwake, Upanga, Dar es Salaam na kuwataka wana CCM na wananchi kwa jumla wasimwelewe vibaya.

  "Siwezi kuondoka CCM ambako nimekuwa mwanachama kwa zaidi ya miaka 40, CCM bado Chama kizuri, kina uzoefu wa kuongoza, isipokuwa ndani yake kuna baadhi ya viongozi hawaitakii mema, ndiyo maana wakati mwingine nakemea kwa kuwa siko tayari kuona Chama changu kikiteketea," alisema Sabodo. Alisema haoni chama mbadala cha CCM ambacho kinaweza kushika dola na kuongeza kuwa, "Vyama vyote vya upinzani havina uzoefu wa kuongoza nchi."

  Alitoa toa wito kwa wananchi kutofanya makosa ya kufanya majaribio ya kuwapa ridhaa wapinzani kuunda serikali. "Nawaomba Watanzania wenzangu, tusifanye majaribio ya kuwapa CHADEMA au chama kingine chochote zaidi ya CCM kuongoza serikali kwa kuwa havina uzoefu, hatuwezi kufanya majaribio ya kuliweka rehani Taifa," alisema mfanyabiashara huyo.

  Kuhusu msaada wa sh. milioni 100 alizotoa hivi karibuni kwa CHADEMA za kuchimba visima vya maji, alisema ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kuwa visima vitakavyochimbwa vitasaidia wananchi wote bila kujali itikadi zao za siasa.

  Alisema amepanga kuchimba visima 200 katika majimbo yote nchini, bila kujali wabunge wa majimbo hayo wanatoka vyama gani kwa kuwa lengo lake ni kuwasaidia Watanzania na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya CCM.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Chiligati alimshukuru Sabodo kwa kutoa msimamo wake huo kwa kuwa unamaliza minong'ono ya baadhi ya wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla juu ya msimamo wa mfanyabiashara huyo ndani ya Chama.

  "Nitawajulisha wanachama wenzako wa CCM na wananchi kwa jumla, kwamba bado uko nao kwa hali na mali ndani ya Chama chetu kwa ajili ya ustawi wa taifa letu, kauli yako imemaliza minong'ono kwamba umehama au una mpango wa kuhama CCM," alisema.
  .
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  inavyosemekana huyo chiligati alikwenda kwa sabodo huku amevalia bastola kiunoni -- magamba style!
   
 3. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Hili ni gazeti gani? Naona hii habari imeandikwa kiushabiki. Na linaonekana kama gazeti linalo promote CCM. Hatasemaje kuwa ametoa mil 200 kwa ajili ya kuchimba visima bila kujali wabunge wanatoka chama gani,wakati alitoa kwa ajili ya maeneo wanayotoka wabunge wa CHADEMA.
  Alafu anaposema hakuna chama kingine kinachoweza kuongoza zaidi ya CCM,wakati juzi alisema CHADEMA kinaweza. Waandishi wengine wa Habari wanaandika habari ambazo ni kwa ajili ya kupindisha ukweli tu.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mbona hajaongelea kuhusu kum-support mgombea urais wa chadema?au chiligati alisahau kuuliza?
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wadau msihangaike SOURCE ni gazeti la UHURU.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,079
  Trophy Points: 280
  Gazeti la Uhuru?kha!..ni bora likaitwa gazeti la 'UTUMWA'..ni mtizamo tu.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sabodo ni moja ya watanzania wanaofaa kuigwa, wapenda maendeleo ya taifa lao bila kujali itikadi na nafikiri kuna akina SABODO wengi sana. Hakuna haja ya kukichukia chama kisa wewe siyo mwanachama wake na nadhani CDM wanatakiwa kupata picha halisi kuwa siyo kila anayebeba bango na kuwashangilia basi ni mfuasi wao na ndiyo maana hata wakati wa chaguzi mbalimbali matokeo huwa kinyume na matarajio yao kwani kwa mfano huu wa SABODO watakuwa wanaamini kwamba walipata kura yake katika uchaguzi mkuu uliopita kumbe sivyo. Tunahitaji akina SABODOwengi kuiunga mkono serikali katika kuwaeletea wananchi maendeleo , wale wanaoendeleza U-CHADEMA na U-CCM let them undergo a nature death sisi tutaendelea kudunda.
   
 8. J

  Jesse kt New Member

  #8
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaogopa kufilisiwa.bt ye ni pipo damudamu
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umekua sasa eeh!!!!!!!!!??????
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ilikuwa amuue mzee wetu kama asingebadili msimamo wake huo mkali.
   
 11. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Naona dalili za 'U ndumila kuwili hapa' Kuuma na kupuliza. Haya sie yetu macho na masikio.
   
 12. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  kUMBE NI GAZETI UCHWALA!!!! HIVI SIKU HIZIHILI GAZETI LINANUNULIWA AU ANALINUNUA JK NA NAPE WAKE MAANA KILA NIKIENDA KWENYE VIBANDA VYA MAGAZETI NAKUTA MAGAZETI KAMA MWANANCHI, TZ DAIMA, MWANAHALISI, NIPASHE YAMEISHA ILA HILI UHURU NAKALA ZIMERUNDIKANA ,,,NADHANI HATA WAUZAJI WATAKATAA KUYANUNUA MAANA NAJUA YANAWAPA HASARA,, VIVAAAAA
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Chaga development manifesto [CDM]
   
 14. K

  Kamura JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sabodo naye mnafiki. Unakuwaje mwanachama mwaminifu wa CCM halafu unatoa msaada wa kuimarisha CHADEMA?
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kama kawapa maeneo yanayotoka Wabunge wa CHADEMA basi yeye kisha kuwa magwanda? na hayo maeneo ya wabunge wa magwanda hakuna watu wasio na vyama? au wa vyama vingine> au mtawabaguwa wasiteke maji kwa kuwa wabunge wa hayo majimbo ni wa magwanda? Unanshangaza!
   
 16. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Acha upuuzi wewe. Wakati watu wanaongea mambo serious usilete mambo ya ukabila ambayo kwa namna yoyote hayawezi kutujenga. Hizi mbinu za kijinga za baadhi ya wana ccm za kugawa watu kwa dini, kanda na makabila hatuwezi kuziruhusu. Kama huna cha kuchangia soma za wenzako.
   
 17. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  agh, kumbe!
   
 18. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,723
  Trophy Points: 280
  Ametoa kauli hiyo at gun point, mzee kaogopa kuuliwa kama alivyouawa Kombe. CCM ni Chama Cha Magaidi.
   
 19. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Chiligati alienda nyumbani kwa Sabodo kufanya nini?
  Alialikwa au alijipeleka?
   
 20. F

  FUSO JF-Expert Member

  #20
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,336
  Trophy Points: 280
  sabodo ni mwerevu sana, sisi wenye akili tumeshajua ana maana gani kutoa hii statement.
   
Loading...