SABODO sasa ashauri fedha zibadilishwe, ampongeza Rais asema hakuna haja ya upinzani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
5e347fc6d95c91d622171887cfb5be19.jpg

Wakati wananchi wakilia ukata mifukoni kwa madai fedha zimetoweka kwenye mzunguko, mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, huoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalum nyumbani kwake Dar es salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi

"Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi waliofikwa fedha nyumbani, watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha

Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na 10,000 hatua hiyo itasaidia kubadili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania mpya," alisema Sabodo

Aliongeza:"Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na nusu, watabainika wengi waliofikwa fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika".

Alifanunua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama ilivyo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao

"Watu wanaiba fedha nyingi, wanaficha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi". alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka waliofikwa fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahala pa kuzipeleka

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogapa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Chanzo: JamboLeo
 
Wanauchumi Tusaidiane. Ni kweli hatua hiyo ita work Kwa nchi na zama zetu.. Mambo mengine wataalam tuache wachangie
 
Sasa hao walio ficha wakibadili Fedha zao kwenda Dollar, Utawakamatia wap Basi kuna haja ya Kubadilisha na dollar pia.. Ila kama Dollar ni hela Ya Tanzania hahaha Akili za kuamka.
akibadili kwenye dola si anauza shilingi ananunua dola nadhani itakuwa imerudi kwenye mzrunguko akili yangu inawaza hivyo... sababu wanao ficha hawataki kuonekana wanapesa,.. ila ngoja wachumi waje
 
Naunga mkono hoja hela zibadilishwe, ila watoe wiki moja badala ya mwezi
Hao wahindi wote washapeleka hela zao Canada na UK.
Sasa nyie badilisheni mtapata mnachokitafuta.

Siku hizi watu wanaangalia sheria, kanuni na msimamo wa nchi yako ukoje then WAKIVUTIWA watakuja nchini kwako kuwekeza na kufanya mengineyo.
Lkn hii ya kulazimishana ktk dunia hii ya leo ni ngumu.
Kuna watu wanakwenda hapo Kenya tu kuhifadhi hela zao tena kwenye mabenki kwa sababu pale pako salama but not Tz.
 
Back
Top Bottom